Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Daah umenikumbusha mbali sana! Igunga nimekaa sana na nimezaliwa sehemu moja inaitwa "Mwanzugi"! Kulikuwaga na msukuma mmoja hapo mwanzugi alikua anaitwa Ngokoyaza alikua na ng'ombe nyingi enzi za utoto kwenda kutafuta ubuyu na mifuru, matoborwa/matoboro tulikua tukipita eneo lile tunatoka nduki alisifika kwa uchawi so tukawa tunaogopa sana!
Nitarudi kutembea tena sehemu niliozaliwa!
Ngokoyaza aka kuku mwekundu, mbitiyaza aka fisi mwekundu haya majamaa hayaumizagi kabisa vichwa kuhusu majina ya watoto 😆😆
 
Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 15.

Nilifungua ule mlango ulokuwa umefungwa kwa komeo nikatoka nje na kuanza kukimbia kama mwendawazimu.Niliingia kwenye shamba la jirani na hapo kwao Monica lililokuwa na mahindi madogo saizi ya magoti kisha nikalala chini!.Nilishindwa kuelewa mpaka muda huo binti Monica atakuwa yupo wapi maana mlango haukufunguliwa na yeye ndani hakuwepo!.Sasa nilinyamaza kimya ili kuona ni kitu gani kilikuwa kinaendelea.

Baada ya kama dakika 20 hivi,nikawa nasikia sauti ya Monica ikiniita kuashiria kunitafuta,mimi niliendelea kukaa kimya huku nikichukua tahadhari na nilidhani uenda asiwe Monica nikaingia chaka!.Kwa mbali niliona ule mlango wa ile nyumba unagunguliwa mtu akaingia ndani kisha akatoka tena akawa anaita.Baada ya kujiridhisha kwamba alikuwa Monica ndiye aliyeniita,niliamua kusimama na kujipangusa mchanga uliokuwa umenijaa kwenye tumbo na magoti na hii ilikuwa ni baada ya mimi kulala chini!,mpaka wakati huo nilikuwa kama nilivyozaliwa maana nilipokurupuka sikukumbuka hata nguo nimeziweka sehemu gani!

Monica "Uko wapi?"

Monica alijifanya kuniuliza niko wapi kana kwamba alikuwa hanioni,ila nilichoamini mimi ni kwamba alikuwa akiniona tu vizuri!.Niliondoka kuelekea ule uelekeo alokuwa amesimama Monica.

Monica "ulikuwa wapi?"

Mimi "Nilikuwa pale"

Monica "Sasa huku nje umefata nini!?"

Mimi "Wewe ulienda wapi?"

Monica "Mimi mbona nilikuwepo?"

Mimi "Ulikuwepo wakati nimekutafuta sikuoni!?"

Monica "Kuna mjinga mmoja nilikuwa namshikisha adabu"

Mimi "Mjinga gani?"

Monica "Hukusikia napigana na mtu"

Mimi "Mimi sijasikia,nilichosikia ni kishindo kikubwa nyuma huko nageuka nakuangalia na wewe hauonekani,ndiyo nikatoka kukimbia"

Monica "Nilikwambia umughaka nitakulinda usiku na mchana,kuna mjinga alikuja kutaka kunijaribu,nimepambana nae alitaka kunishinda nikamuita mama"

Mimi "Kwahiyo mama yupo ndani!"

Monica "Mama amemchukua amempeleka wakamtengeneze vizuri!"

Basi baada ya kuniambia maneno yale ilibidi tuingie ndani,kiukweli nilikuwa nina hofu sana na nilijilaumu kwanini nimeingia kwenye mahusiano na yule binti,kibaya zaidi siku zilivyokuwa zikienda ndivyo na mimi nilikuwa siambiliki wa kuelezeka kwa yule binti!,ilifikia pointi ambayo nisipokuwa nikimuona nilikuwa ninapata mawazo sana.
Mida hiyo ilikuwa yapata saa 9 usiku na tangia hapo sikupata usingizi tena,ilipofika mida ya saa 10 kuelekea saa 11 ambapo niliona kabisa kama kuna miale ya mapambazuko,nilimwambia anisindikize kurudi nyumbani.

Monica "Mbona unawahi hivyo?"

Mimi "Nadhani unamjua Ema alivyo muongo,na najua kama aliamka kwenda chooni akakuta sipo sijui itakuwaje,lazima tu amwambie Ba'mdogo"

Monica "Yule hawezi kuamka mpaka wewe ufike"

Mimi "Wewe yule humjui vizuri!"

Monica "Basi tufanye kidogo halafu ndiyo uende"

Kiukweli sikuwa kabisa na hamu tena ya mizagamuano ila kwakuwa alitaka sikuwa na namna,ikabidi tulianzishe tena!.Fimbo ziliendelea mpaka sasa nikawa nasikia majogoo yanawika huko nje kuashiria kumepambazuka!.Nilivaa zangu nguo na yeye pia akavaa na safari ya kunisindikiza kwetu ikachukua nafasi.Monica hakutaka kabisa kuniacha njiani,alihakikisha mpaka naingia ndani ndipo na yeye anarudi kwao.

Ilikuwa ni kama kuonekana kwao ni mbali lakini nilipokuwa nikitembea na yeye sikuwahi kuona wala kuhisi umbali wowote,hebu fikiria umbali wa zaidi ya kilometa 6 lakini ndani ya dakika kama 10 mnajikuta shafika!,haya yalikuwa ni maajabu ya binti wa kisukuma Monica.Basi baada ya kuhakikisha nimefungua mlango na kuingia ndani na yeye aliondoka kurudi kwao.
Nilisukuma mlango nikaingia ndani nikakuta Ema bado amelala,sasa sikufahamu aliamka wakati mimi sipo ama la!.Kwakuwa kulikuwa kumepambazuka sikutaka kujiegesha maana niliona ningepitiwa na usingizi,nilijifanya namuamsha jamaa ili nione!.sasa baada ya kumpiga piga na mkono,jamaa alishituka sana!.

Mimi "nimekushitua?"

Ema "Maanangu nilikuwa naota"

Mimi "Ooh,jana ulichoka sana nini!"

Ema "Yaani sijawahi kulala usingizi mtamu kama wa leo"

Mimi "Kumekucha kijana jiandae uende skonga"

Ema "Leo sidhani kama nitaenda"

Mimi "Shida nini?"

Ema "Nahisi kuchoka tu"

Sasa jamaa alikuwa ananieleza huku akiendelea kupiga miayo ya kufa mtu!.Nilipoendelea endelea kumdodosa ndipo nikagundua tangu ule usiku nilipotola hakuwa ameamka hata kidogo!.

Basi kulipopambazuka zaidi nilielekea lamboni kuchota maji ya kuoga na kurejea nyumbani,basi baada ya kumaliza kila kitu niliingia ndani kumsalimia Headmaster na mkewe na kisha mimi kuelekea kwa mzee masumbuko kuchukua miwa ya kwenda kuuza.Sasa wakati unatoka hapo kwa mzee masumbuko ili uikamate njia ya kuelekea Senta,kulikuwa kama na makutano ya njia,njia moja ndiyo njia ambayo ilikuwa inatoka kwenye uwanja unapofanyikia mnada na ukipandisha nayo inakupeleka moja kwa moja kwa kina Monica kule Masairo,njia nyingine ni njia ambayo ilikuwa inakupeleka mpaka lamboni ambako unatokea mpaka shuleni,na njia nyingine ndiyo njia ambayo nilikuwa naipita mimi kuelekea senta kila ninapotoka kuchukua miwa!.

Sasa wakati naikamata njia ambayo ilinipaswa kupita kwa mbele kuna kina mama walikuwa wakija wakiwa wawili,mmoja wapo nikama nilimuona kwenye zile ngoma pale kwao Monica ule usiku!,sasa walizungumza kisukuma halafu wakawa wananitazama sana,nikama walikuwa wananiteta!,waliponipita nilihisi kabisa wanaendelea kunitazama,sasa nilipofika kwa mbele nikautua ule mzigo wa miwa nikajifanya kama naufunga kwa kukaza,nikawaangalia kwa kuibia ndipo nikaona wananitazama na nikama wakawa wanazungumza kwa kubishana!,walipoona nawaangalia wakaondoka huku wakionekana kama kunishangaa!.

Sasa nikabaki namuangalia yule mama ambaye nilimuona ule usiku nikabaki kushangaa tu,kiukweli ukikutana naye hivi kwa mara moja na ukiambiwa mambo anayoyafanya huwezi kabisa kuamini!.Nilijitwisha zangu zigo la miwa na kuondoka huku nikishindwa kuelewa kwanini wale kina mama walikuwa wakiniangalia kwa makini sana!.

Siku hiyo biashara ya miwa ilikuwa mbaya sana,kiukweli tangu asubuhi hadi jioni niliuza pingili tatu tu za muwa,basi kwakuwa nilijua biashara siku zote haifanani sikutaka kujipa presha kabisa,nilipanga Headmaster akiniuliza nitamaambia ukweli ya kwamba biashara imekuwa ndivyo sivyo,basi ilipofika jioni nilienda kupeleka miwa kwa yule mama aliyekuwa akinifadhia na mimi kuondoka kueleke nyumbani,wakati wote nilikuwaga naondoka hapo senta mida ya saa 12 jioni na kufika nyumbani mida ya saa 1 kuelekea saa 2.

Sasa nilipotembea kwa umbali mrefu,huku nikiwa naendelea kuitafakari siku,mara ghafla mbele yangu akatokea yule mzee Makono ambaye pia alikuwa mmoja aa wale watu waliokuwa wakicheza ngoma ule usiku,nilishangaa sana kwasababu eneo nililokutana nae,ndilo aneo ambalo siku ile nilikutana nae na akanitaka nikamsalimie Headmaster,safari hii nilishituka sana mpaka akashangaa!.

Mzee makono "Unishituka nini wewe!"

Mimi "Mzee shikamoo"

Mzee makono "Kwahiyo hujashituka jana leo ujifanye kushituka!"

Kiukweli nilishangaa sana na ghafla uoga mkuu ukaniingia,nilishindwa hata kukimbia nikabaki nimepigwa na bumbuwazi,sasa nilibaki kushangaa kwasababu iliwezekana vipi jana kuniona na wakati Monica aliniambia sababu ya yeye kunipaka ile dawa ni kusudi nisionekane na wacheza ngoma kama adui na wahisi mimi ni mmoja wao!,pili nikajiuliza yeye mzee makono alinionaje?,Sasa wakati naendelea kutafakari nisijue cha kufanya,akaendelea kuniambia kwamba

Mzee makono "wewe na kale kakondefu mmeshirikiana kunitesea mwanangu!,si ndiyo?"

Akaendelea "Nataka leo unitambue mimi ni nani!"

Sikutaka kabisa kumjibu yule mzee nikawa nimebaki kimya kwa bumbuwazi,basi baada ya kuniambia maneno hayo akasonya kwa kufyonza kisha akaondoka!,kiukweli ongea ya yule mzee alionekana kabisa amechukizwa sana na alikuwa na hasira mno!.
Sikufahamu kwa haraka haraka ni kitu gani kilikuwa kimemkasirisha na ni nani aliyekuwa amemtesa mwanaye!.

Basi kutokana na uoga niliyokuwa nao,nikaanza kukimbia ili kuwahi nyumbani,safari hii nilipofika pale kwenye miembe nilipita kwa spidi kali mno kama kipanga na sikutaka hata kugeuka nyuma!.

Sasa nilipofika karibu na nyumbani nilimkuta Monica akiwa amesimama anaongea na Ema.

Ema "Haya huyo hapo ongea nae"

Baada ya kusema hivyo Ema akawa anaelekea ndani!.

Mimi "Kwani kuna nin?"

Monica "Tuondoke hapa"

Mimi "Nakupenda umughaka,nakuomba tuondoke,utajua huko huko"

Basi Monica akanishika Mkono tukaongozana kuelekea nisipopafahamu.Mpaka muda huo hata ndani sikufika kabisa.

Mimi "Tunaenda wapi?"

Monica "Nilikwambia nitakulinda kwa gharama yeyote,huyo mjinga anajifanya mjanja muache".
Umughaka!! umeyakanyaga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kijiji tulihamia mwaka 1996 huo ujinga wa ukikutana na mchawi kabeba mzigo hata kama ni mchana anakubebesha pasipo wewe kufahamu na unamfikishia mpaka kwake pasipo wewe kujua,zaidi na zaidi baadae utahis kama shingo inakuuma tu
 
Asee, tunguri zinakulinda UMUGHAKA

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nani kakudanganya wanyantuzu sio wasukuma? Hiyo ntuzu ni chiefdom tu (utawala wa kitemi) lakini ni wasukuma walewale. Ni sawa na kusema Badaka, Bakwimba, Banantuzu nk. Hizo ni koo au utemi fulani lakini pia kuna tofauti katika utamkaji wa maneno ya kisukuma lakini wao wanaelewana. Msukuma wa Ntuzu au Bariadi anasikilizana na kuelewana vizuri tu na msukuma wa Balaturu Igunga. Ni sawa na kiswahili cha Bara na Pwani au kiingereza cha Uingereza na Marekani.
Nimekuelewa
 
Back
Top Bottom