Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 4,748
- 7,061
Teh! Teh! Teh! Teh!Wakuu nipo kijiweni,kuna muda naamua kuangalia tu comments za wadau,marafiki na ndugu zangu wa JF nabaki kufurahi tu[emoji23][emoji23].
Yaani kama unahasira za kijinga JF haikufai maana unaweza mrushia mtu ngumi ingawaje niya upepo[emoji23][emoji23][emoji23].
Humu kuna watu wanakera
Humu kuna watu wanaudhi
Humu kuna watu wanachukiza
Humu kuna watu wanafuhisha
Humu kuna watu wanajua kila kitu.
Yaani ukitaka kupata raha na karaha wewe tembelea JF [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
All in All nawependa sana ndugu zangu na tuonane muda si mrefu!
Umenikumbusha mwaka 1999 October, tupo kwenye maombolezo ya Mwalimu Nyerere. Wakati huo, watu wenye TV walikuwa ni wachache sana.
Sasa, nipo Shinyanga, kwenye baa moja, maeneo ya Stand mpya hapo SHY mjini. Kwenye baa hiyo, Ilikuwa inatolewa TV nje, na watu wanajaa kufuatilia matangazo live yaliyokuwa yanarushwa,yakihusu hicho kifo cha Nyerere, hata njia ya wateja kuingia ndani, haipo. Ilikuwa ni saa 12 jioni, mwenye hiyo baa alikuja hapo, na kutaka aingie ndani, lakini hakuna njia ya kupita. Akaomba watu wampishe apite, lakini ikawa kama hajasikika.
Wengine wakawa wanamrushia maneno ya kejeri, na kudai wao wanafuatilia jambo la muhimu, na wakiwa na majonzi, halafu yeye anataka kuwasumbua! Akamuita muhudumu mmoja, na kumuamrisha aizime hiyo TV.
Kabla hajafanya chochote, sauti za kumuonya zilivuma hapo, na kunywea. Akaanza kutishwa hata tajiri mwenyewe, na kuamua kuondoka.
Hao watazamaji, siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho kuja hapo, kwani, haikutolewa tena nje ile TV.
Kwa hiyo mkuu UMUGHAKA ,waaalaaa usijali na hayo maudhi. Si hapa JF tu kuna ambao hatuna shukrani, bali ndiyo tabia za binadamu zilivyo! Endelea kupoteza muda wako, kwa ajili ya kutuburudisha nduguzo!