Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Pale kwenye kuelezea Monica umesema sura tu inambeba

Ulimaanisha ilimbeba kumfanya aonekane mkubwa huku ni mdogo au ilimfanya aonekane mzuri?

Najiuliza sababu ulisema sura yake ya baba ila kajaaliwa tako tu
Monica sio myenye kalio na sura mbovu. Uyo ni mwingine
 
Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 19.



Kiukweli nilikuwa nimechukia sana namna nilivyodharirishwa pale shuleni mbele ya wanafunzi!,sikutaka kuonekana mkorofi na mkaidi,nilifanya kila nilichoambiwa ili mambo mengine yapite!,niliona angalau Ba'mdogo aniadhibu kuliko taarifa za kulala nje ningemfikia baba yangu hakika angeniua kwa kipigo na shule angeweza kuacha kunisomesha nikawa mchunga ng'ombe!.Japo nilifanya kosa la kulala nje bila taarifa lakini nilidhani ile adhabu ya kudharirishwa haikufaa hata kidogo na ilijaa uonevu mkubwa!.

Basi nilianza kutembea kutoka hapo Senta kuelekea nyumbani huku kile kichwa cha cherehani nikiwa nimejitwisha kichwani,kiukweli nilichukia sana lakini niliamua kujikaza mtoto wa kiumwe,niliamini hayo ni mambo ya kawaida tu na yangepita!.Kile kichwa cha cherehani hakikuwa chepesi kama nilivyodhani na ilipelekea nikawa nafika sehemu najitua kichwani nashikiria kwa mikono miwili lakini bado haikusaidia,kwahiyo nilichokifanya ilikuwa nakiweka begani angalau nikawa naona kuna unafuu!

Nilifika nyumbani nikiwa nimechoka sana na kwakweli kuanzia siku hiyo,mimi na Ema tulikuwa kama Paka na Panya,sikutaka kabisa jamaa aniambie chochote wala kunisogelea kwasababu nilimuona ni mnafiki!,mara kibao tu yeye nilikuwa nikimtunzia siri zake lakini jamaa yeye za kwangu hakutaka kabisa kuziweka moyoni.Kitendo cha kumwambia Ba'mdogo nilikuwa natembea na binti Monica tena mbele ya wanafunzi kilifanya nikamchukia sana jamaa!,na nilichoamua ni kwamba kama mbwai na iwe mbwai!.

Haikupita muda Maza mdogo naye akawa ametoka senta,kama kawaida yeye alikuwa akitoka senta alikuwa anaingia kuoga na kusubiri kula,wa kupika sana sana nilikuwaga mimi maana Ema nae alikuwa anajifanya kusoma kila alipokuwa akitoka shule,sasa nilikuwaga najiongeza tu kuingia jikoni kupika ili kuepuka matusi ya Ba'mdogo.
Siku hiyo nilikuwa nimechoka sana na nilikuwa nanuka jasho kwasababu ya zile kazi kuanzia asubuhi hadi ile usiku lakini sikuweza kuyasogelea maji kwasababu niliambiwa na Monica na akanionya nisiguse maji!.

Siku hiyo nililala kwa uchovu sana,namshukuru Mungu palipo pambazuka niliamka nikajiandaa kuondoka zangu senta,sasa nilichofanya nikupiga mswaki tu na kubadili nguo,sikutaka kabisa hata kunawa uso,nilipomaliza niliingia ndani kuwasalimia Headmaster na mkewe!.

Maza mdogo "Wewe unaenda halafu hicho kichwa cha cherehani nani atakipeleka?"

Nikawa kimya kwa muda huku nikiwa natafakari nini cha kujibu!.

Headmaster "Kwani kichwa cha cherehani sikuhizi unakileta nyumbani?"

Maza mdogo "Juzi sinilikwambia wanasema yule mama Mayala aliwahi kuibiwa kichwa cha cherehani pale kibandani kwake,unadhani chanzo cha Mama Mayala kuacha kushona ni nini?"

Headmaster "Sasa kwanini usiwe unamuomba mama Rebecca unakiacha pale nyumbani kwake kuliko kupata kazi ya kukileta huku!".

Maza mdogo "Ngoja nitajaribu kuongea nae!".

Headmaster "Wewe nenda uwahi kwenye shughuli zako bhana!"

Maza mdogo "Sasa nani atanisaidia kukipeleka senta"

Headmaster "Utakamata hapo mwananfunzi akusaidie"

Sasa mimi sikutaka kabisa kuonekana uenda nilichukia kukibeba kile kichwa,niliamua kujikaza na kumwambia ningekifata baada ya kupeleka miwa senta.

Mimi "Haina shida mama ngoja nikachukue miwa nipeleke senta halafu narudi kukichukua".

Maza mdogo "Sawa,uwahi sasa"

Sasa nilidhani uenda Headmaster alivyokuwa amemshauri ya kwamba angekamata pale shuleni mwanafunzi amsaidie kubeba kile kichwa na kukipeleka Senta angekubaliana nae lakini haikuwa hivyo,kitendo cha kuniambia niwahi kurudi kukibeba ilionyesha kabisa alifurahishwa na mimi kwenda senta na kurudi kukibeba!.Basi sikuwa na hiyana mtoto wa kiume nikaondoka zangu kuelekea kwenye mashamba ya mzee Masumbuko kwa ajili kufata miwa kama kawaida,ingawaje miwa iliyokuwepo haikuisha ila niliona ni heri nikakusanya ikawa mingi ili inipunguzie safari ya kila siku kuamka asubuhi na mapema kisa kuwahi miwa!.

Nilipofikisha ile miwa pale senta niliibwaga chini nikaondoka zangu kurejea nyumbani kwa kukimbia ili kuwahi kurudi!,sasa kuna sehemu nilifika nikamuona dogo mmoja akiwa kwa mbele kabeba kile kichwa cha cherehani huku Maza mdogo akiwa nyuma yake,nilipowafikia nilimwambia dogo anipe kile kichwa nimsaidie na yeye arudi shule!.

Nilijifanya kuchangamka na kutabasamu kiunafiki lakini kiuweli nilikuwa nimechukia sana,nikawa najiuliza kama alikuwa anajua angempatia mwanafunzi amsaidie kubeba kwanini alitaka nirudi tena?,kama kawaida yangu sikutaka maneno na mtu nikaamua kufunga bakuli langu ili mwanaharamu apite.Wakati huo kiukweli nilikuwa nimeanza kupoteza nuru ya muonekano wangu kwasababu ya kushinda kule senta wakati mwingine sili kabisa mchana na chakula nilikuwa nakutana nacho usiku tu!,mara nyingi nikiwa pale senta nilikuwa nashindia sana miwa!.

Tulifanikiwa kufika senta na nikakipeleka kile kichwa kwenye kibanda alichokuwa akishonea na mimi kwenda mpaka kwa yule mama ambaye nilikuwa nikilaza ile miwa,niliichukua nikaenda kuinganisha na ile niliyokuwa nimekuja nayo na kuanza kuuza!.Namshukuru Mungu siku hiyo niliuza sana ile miwa,japo haikuisha lakini mpaka kufika mida ya saa 10 alasiri ikawa imepungua kwa kiasi kikubwa!
Sasa nikiwa naendelea kuuza miwa yangu pale,kwa mbali nikamuona yule binti Mwise akiwa na binti mmoja wakiwa wamevaa sketi za shule na tisheti za kawaida wakiwa wanakuja hapo senta, sikufahamu kilichokuwa kimewaleta uenda walifata mahitaji kama watu wengine!.

Yule binti kiukweli ndiye alikuwa binti wa kwanza kwa hapo kijijini kuumiza na kuutesa moyo wangu,nilikuwa nampenda na kumtamani sana kutokana na shepu yake nzuri!,ila baada ya kuanza kutembea na Monica kiukweli upendo na matamanio yangu kwake yakaanza kupungua kwa kasi ya ajabu!.Walipofika karibu waliingia kwenye duka moja wakanunua kilichowaleta kisha wakatoka wakawa wanaelekea kwenye vibanda na maduka ya mbele ambako huko pia ndiko mama mdogo anakofanyia shughuli zake,sasa baada ya kugeuka na kutazama uelekeo niliokuwepo mimi,nikampiga mkono kwa ishara ya kwamba aje!.

Mwise "Narudi!"

Kwakuwa aliniambia anarudi nikasema ngoja nisubiri.Safari hii sikutaka kabisa kuwa na kimuhe muhe kwasababu sikuweza kujificha na ile biashara yangu na yeye alifahamu kabisa nilikuwa muuza miwa!,niliamini kama ni kumpata basi ningempata tu na kama ni kumkosa basi ningemkosa vilevile!.

Haukupita muda wakawa wanarudi na huyo mwenzie,sasa alipofika pale kwenye eneo langu la biashara akaanza kama kuonyesha nyodo na dharau.

Mwise "Nionjeshe muwa rafiki yangu!"

Mimi "Kwahiyo mimi leo nimekuwa rafiki yako?"

Mwise "Jamani!,kwani kuna ubaya wewe kuwa rafiki yangu?"

Basi nikamkatia pingili mbili za muwa yeye pamoja na mwenzie!,basi wakawa wanazungumza na huyo rafiki yake maneno ya kisukuma huku wakicheka kwa kicheko cha kichini chini!,kiukweli walikuwa wanikiteta kwa kisukuma na ishu kubwa walikuwa wakizungumzia zile stiki nilizokuwa nimelambwa na Headmaster mbele ya wanafunzi!,wao walidhani siwaelewi lakini hata kama sikuelewa kisukuma vizuri mtu alikuwa akiteta inafahamika kabisa!.

Walipomaliza kukwangua kwangua miwa kwa kisu akawa ameniambia wanaondoka kuwahi kurudi nyumbani,nikawa nimemuomba anivumilie angalau kwa dakika mbili nizungumze nae!,sasa yule mwenzake akawa amemwambia atamkuta mbele!.

Mwise "Sasa na wewe unaniacha nyanoko"

Mwenzie "Utanikuta mbele bhana"

Mwise "Mmh!,niambie mi nina haraka"

Mwise "Kwahiyo Mwise Ombi langu vipi lakini?"

Mwise "Ombi gani tena jamani"

Mimi "Kwani mara ya mwisho mimi na wewe tuliongea nini?".

Mwise "Siulianimbia unanipenda,nashukuru kwa kunipenda"

Mimi "Usinifanyie hivyo Mwise"

Mwise "Wewe si unaye mwanamke wako"

Mimi "Mwanamke gani tena jamani!?"

Mwise "Wewe ema kaniambia habari zako nyingi tu!,kumbe ulikuwa tu unataka unilale uniache"

Mimi "Daaah!,hebu achana na mambo ya Ema Mwise,Ema anashida kubwa na wewe yule unamfahamu akili yake".

Mwise "Mimi nachelewa bhana,kesho!"

Basi yule binti alianza kukimbia kumfuata mwenzie aliyekuwa akimsubiria.Niliamini kabisa kwa kilichotekea pale shule ukichanganya na uongo wa Ema,haikuwa rahisi mimi kumpata tena yule binti.Niliamua kujipa moyo ya kwamba mademu mabaya siku zote ndiyo yanayoringa lakini kuna muda bado nilikuwa nikifikiria kiuno cha yule binti na kuwaza kinavyo chakatwa na wanaume wengine,kiukweli nilikuwa naumia sana!.

Sikuwa na namna ilibidi niwe tu mpole ili maisha yasonge!.

Baada ya kukamilisha siku ya uuzaji wa miwa niliamua kurudi nyumbani na namshukuru Mungu safari hii sikurudi na kichwa cha cherehani kwasababu maza mdogo alipata pa kukiweka hapo senta.

Sasa nilifika nyumbani mida ya saa 1 usiku,nilielekea lamboni ile usiku kuchota maji ili nije nioge kwasababu nilikuwa sijaoga tangu jana yake!,sasa nilipotoka bafuni kuoga,nikawa nimeingia ndani kwa ajili ya kupaka mafuta!,sasa wakati napaka mafuta nikasikia kuna mtu ananipiga piga mgongoni kwa mkono akiashiria nigeuke!,sasa ile nimegeuka nikawa nimekutana na Monica uso kwa uso!.

Kiukweli nilishituka sana ila akanifanyia ishara ya kidole mdomoni akinitaka nisipige kelele wala kuongea!.

Mimi "Monica kuna nini mbona huko humu"

Monica "Vaa nguo tuondoke"

Mimi "Tuondoke twende wapi tena!?"

Monica "wewe vaa twende"

Mimi "Tunarudi lakini?,maana mwenzio jana jana nimepigwa kwasababu yako"

Monica "Hatuendi mbali tutakuwa nje hapo"

Basi baada ya kuvaa nguo,Monica akawa amenishika mkono na ghafla tukawa nje ya nyumba kwa pembeni kidogo.

Monica "Tusogee pale kwenye lile jiwe!"

Baada ya kufika pale kwenye lile jiwe akanitaka tukae pale na kuna watu tuwasubiri walikuwa wanakuja!.

-SEHEMU YA 20
Monica ushampata sasa mwise wa nini tena?
 
Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 9.




Basi mizagamuano ilipamba moto kiukweli hadi nikasahau kurejea nyumbani nikajikuta nimepitiwa na usingizi.Nimekuja kushituka ni saa 1 asubuhi sikumuona yule binti kwenye godoro.Nikakurupuka kuamka nikavaa zangu nguo na kutoka nje.

Sasa ile nimetoka nje na endelea kushangaa shangaa kumuangalia yule binti, nikamuona akiwa anakuja amejitwisha ndoo ya maji kichwani.Alipofika nikamsaidia kumtua.

Binti "Mbona mapema?"

Mimi "mapema tena!,mimi naondoka!"

Binti "Subiri basi nimebandika michembe ule ndiyo uende"

Basi kwakuwa nilikuwa nina njaa sikula tangia nilipokula kule nyumbani mchana wa ile siku tuliyokula kuku,sikuwa na namna ikabidi nisubiri michembe iive nipakuliwe nile,kiukweli nilikuwa nina njaa sana!.Aliingia ndani akawa amenitolea kiti nimekaa zangu pale nje huku nikiendelea kuyaangalia mazingira ya pale kwao.

Kiukweli pale kwao miji ya majarani ilikuwa mbali sana na kilichokuwa kimezunguka nyumba ni mashamba ya mahindi na mihogo.

Mimi "Mama yuko wapi?"

Binti "Ameenda shambani"

Basi baada ya kuniambia mama yake amekwenda shambani nilikaa kwa kujiachia nikapata amani sasa.Sikuona mtu mwingine pale kwao tofauti na yule binti pamoja na mama yake,sasa sikuweza kufahamu kwa haraka haraka wanaishi wao wawili tu au kuna watu wengine,sikutaka kabisa kupeleleza peleleza.
Ile michembe ilipoiva alinipakulia pamoja na uji uliokuwa umejazwa maziwa ya kutosha,ingawa uji haukuwa na sukari lakini ulikuwa mtamu.

Alitandika jamvi chini akaweka chakula kile tukaanza kula.Sasa wakati tunakula kiukweli nilikuwa nikimtazama yule binti na mambo aliyonipa usiku vilikuwa haviendani, binti alikuwa wa umri mdogo tu kama miaka 17 lakini alikuwa na mambo yaliyowazidi wakubwa wengi tu!.,Japo hakuwa mnene lakini alikuwa na umbo la wastani,kiukweli sura ilimbeba sana.

Mimi kwa wakati huo nilichojua ni kupunguza tu ugwadu,hizo habari nyingine za sijui matako makubwa mimi kwa wakati huo sikutaka kuzisikia,cha msingi nilikuwa nimepunguza ugwadu basi mambo mengine yangefahamika mbele kwa mbele.Sasa wakati tunakula akawa ananiambia.

Binti "Usije kabisa ukamwambia Ema"

Mimi "Hapana siwezi kusema chochote,mimi siyo mjinga"

Binti "Unajua Ema aliniambia atanioa"

Mimi "Kweli eeeh".

Binti "Kweli kabisa"

Mimi "Kama ndivyo atakuoa wala usijali".

Sasa kwa akili ya yule ndugu yangu hayo maneno ya kumuoa binti wa watu nilijua kabisa ni uongo na asingeweza kumuoa zaidi ya kumpotezea muda tu!.

Binti "Unajua yule Deborah ningemfanya kitu kibaya sana,sema tu mama yake anafahamiana na mama na ni marafiki tangu zamani,lakini isingekuwa hivyo angenitambua!"

Sasa nilikuwa naangalia binti aliyekuwa anasema angemfanya Deborah kitu kibaya nabaki namshangaa tu kwasababu ukiwapima yeye na Deborah hata hawaendani kimuonekano na kimabavu,Deborah alikuwa na nguvu kumshinda!.

Basi baada ya kula nikashiba ikabidi nimwambie anionyeshe njia ya kuelekea senta ili mimi niende zangu nyumbani.

Alinisindikiza huku akiendelea kunisisitiza nisije kumwambia mpenzi wake jambo tulilokuwa tumefanya.Mimi nikamhakikishia sitoweza kumwambia.

Nilitembea zangu kuitafuta senta ili niwahi nyumbani.Nilifika nyumbani mida ya saa 4 asubuhi moja kwa moja nikaingia ndani kupitia mlango wa uani!.Sikutaka kupoteza muda nikaingia jikoni nikachukua dumu la maji ili nielekee lamboni kuchota maji nije kuoga.
Sasa nadhani wakati nafungua mlango maza mdogo akawa amesikia hivyo akatoka kuja kuangalia ni nani aliyekuwa akifungua mlango.

Mimi "Oooh mama,shikamoo!"

Maza "Marhaba,vipi?"

Mimi "poa,za mjini?"

Maza "Nzuri"

Maza "Sijakuona,ulikuwa umelala nini?"

Mimi "Hapana kuna mahali nilienda mara moja ndo narudi"

Maza "Aaah sawa,kuna uji humo kwenye chupa utakunywa"

Mimi "Sawa mama".

Baada ya salamu na mazungumzo alirudi ndani.Sasa wakati nashuka zangu lamboni nikawa najiuliza jana ilikuwaje?,Je yeye na headmaster walielewa jambo hivyo kaamua kuuchuna au hakuna walichoelewa?,sikutaka mambo yawe mengi,niliamini jamaa angekuwa shule na angetoka ningemuuliza ishu za jana zilienda vipi.

Basi baada ya kuoga nikachukua ule uji nikapiga vikombe viwili,japo nilikuwa nimeshiba lakini nikanywa tu kwa kujilazimisha!.Niliingia kulala na nilishitushwa na jamaa akinishika miguu akiniamsha kwa kunitingisha!.

Nilipoamka baada ya jamaa kuniona tukajikuta tunaanza kucheka!.

Ema "Mwanangu jana ulipotelea wapi?"

Mimi "Wewe acha tu!,sinilikimbia nikajikuta hata njia ya kurudi home nimeisahau!".

Ema "Sasa ulilala wapi?

Mimi " Kuna mahali nilifika nikakuta jamaa wamekoka moto ikabidi nijumuike nao"

Sasa nilimdanganya ili maswali yasiwe mengi,ingawaje na yeye alishindwa kuelewa ya kwamba ule niliyomwambia ulikuaa uongo kabisa kwasababu kwa miezi ile ilikuwa miezi ya palizi na mvua zilikuwa zikinyesha.Jamaa yeye alikuwa akicheka tu bila mpango.

Mimi "Wewe ulilala home?"

Ema "mwanangu mimi nilikimbia na lile hotpot japo nilifika nyumbani nimeloana na michuzi lakini sikujali"

Mimi "Ulikuta dingi ameshafika?"

Ema "Alikuwa bado hajaja,mimi nilikwambia huyu namfahamu vizuri,tena akiwa na mke wake ndiyo kabisaa!"

Ema "Walikuja wakagonga nikaamka kuwafungulia,hata chakula chenyewe hawakula".

Baada ya jamaa kunieleza vile angalau sasa moyo wangu ukatulia.

Ema "Lakini ile sauti nilisikia ilikuwa kama ya Monica!"

Mimi "Monica!,Monica yupi tena?"

Ema "Si kile kidemu changu cha kule Masairo!"

Mimi "oooh sawa"

Mimi "Sasa kama ilikuaa sauti ya demu wako mbona tulikimbia?"

Ema "Mi nilishituka tu nikajikuta nakimbia"

Mimi "Lakini una uhakika alikuwa Monica?"

Ema "Kaka ile sauti niya kwake kabisa,na siunakumbuka aliniita Mpenzi?"

Mimi "Sasa alikuwa anatoka wapi muda ule?"

Ema "Yawezekana alikuwa akitufuatilia,unajua kale nako ni kajanja kajanja sana"

Basi nilianza kuvuta picha na kuunganisha,sasa nikawa najiuliza yule binti ni binti wa namna gani?,Kama mpaka muda ule wa saa 3 usiku hakuwa kwao nilibaki nashangaa,ukiacha hivyo ule muda niliyokutana nae kule kwenye uwanja wa mnadani ilikuwa usiku mnene lakini hata hawazi,niliendelea sana kupata mashaka kuhusu binti Monica.

Basi kuna siku headmaster akawa ametuambia isije ikatokea kufika saa 12 jioni mtu akakosa hapo nyumbani,alisema yaani ikifika saa 12 na ukawa hujarudi nyumbani basi utafute pa kwenda!.Kwa upande wangu nilijisikia vibaya kwasababu sasa zile mechi za Arsenal zilizokuwa zikichezwa usiku ningekuwa nazikosa!,kiukweli niliumia sana.

Sasa siku moja nakumbuka Maza mdogo akawa amenituma mafuta ya kupaka kule senta ambayo ni losheni,sasa akawa ameniandikia jina la ile losheni akanipatia na hela nikaondoka zangu!.,Sasa nilipofika nikakuta yale mafuta yapo ya aina 2,muuzaji akawa ameniuliza ni yapi kati ya hayo ninahitaji?,ikabidi nimuulize ambayo kina mama wanapendelea sana kati ya hayo mawili ni yapi?,yule mama akasema kina mama wengi wanapendelea yaliyokuwa na harufu ya cocoa,basi nikamwambia anipatie hayo hayo yenye harufu ya cocoa!.
Niliporudi nyumbani Maza akawaka sana,kwamba ni mafuta gani yale nimemletea,nikajaribu kumwambia kwamba niliyakuta yapo ya aina mbili na yeye hakuniambia nichukue yapi niache yapi.

Maza "Chukua ya kopo la maziwa bhana"

Maza "Ushakuwa mtu mzima hebu uwe unajiongeza"

Kiukweli nilikasirika sana na kwakuwa alikuwa Maza mdogo ikabidi niuchune,kiukweli sema alijikuta tu amekuwa Maza mdogo basi heshima ilibidi ichukue mkondo wake lakini kwa upande wa umri hakuwa mkubwa wala nini!.

Maza "Hebu rudi ukanichukulie yale mengine".

Basi ikabidi niwe mpole nirudishe tena midenge yangu kule senta,yeye alikuwa afahamu kwamba senta palikuwa mbali,kwenda na kurudi si chini ya kilometa 6,sasa nilipoenda mara mbili maana yake nikajikuta natembea zaidi ya kilometa 12.Nilichukia sana lakini sasa ningefanyaje?,ilibdi nienda nikayafuate tu!.

Sasa wakati narudi ilikuwa mida ya 10 jioni.Nikamgongea mlango nikampa mafuta yake lakini nikiwa nimechukia sana!.

Maza "Siku nyingine nikiwa nakuagiza uwe unaniletea haya siyo yale uliyorudisha"

Mimi "Sawa mama haina shida"

Basi yeye kwa akili yake alidhani mpaka hayo mafuta yaishe mimi ningeendelea kuwa hapo,kwa maisha aliyoanza kuyaonyesha kwa siku chache hizo tu,yalionyesha tungekuja kukwazana sana.

Sasa nikaingia zangu kupumzika kitandani kwasababu nilikuwa nimechoka halafu jua lilikuwa kali.Nikiwa nimejiegesha kuutafuta usingizi kwa mbali,mara ghafla nikasikia sauti ya Maza mdogo akipika kelele!.

Sasa ile nafungua mlango nakuta anakomaa kufungua mlango wa bafuni yeye akiwa kwa ndani,ndipo nikasogea kwenda kumsaidia,sasa ile nimefika mlangoni nataka kuusukuma maana alikuwa akiomba msaada na mimi nikadhani uenda aliingiliwa na nyoka bafuni lakini kumbe yeye alikuwa naya kwake.

Maza "Yaani umughaka kabisa umekuja kunishika matako mimi!"

Maza akaendelea "Wewe niwa kunishika matako mimi nakuuliza?"

Nilibaki nimepigwa na butwa nikawa hata kuongea siwezi nabaki kujing'ata ng'ata tu kwa mshangao.

Mimi "Mimi mbona nilikuwa nimelala!"

Maza "Wewe ngoja baba yako arudi"

Mimi "Mama mimi nimekuja kukusaidia baada ya kusikia kelele"

Maza "Peleka huko utahira wako mbwa wewe"

Maza "Yaani wewe ni wakuja kunishika mimi matako?"

Basi baada ya kusema maneno yale kwa ukali akawa ameingia ndani.Sasa nikabaki najiuliza maswali yasiyokuwa na majibu,Je ni kweli ameshikwa matako?,na kama ameshikwa matako ni nani kamshika?,ina maana hakuona kama mlango alikuwa amelock kwa ndani na mimi ningengiaje bafuni?,Au uenda ni style tu za kunifukuza pale ki-aina?.

Uenda aliona kama tunammalizia mumewe chakula au yale maziwa aliyokuwa akiletewa kila siku!.Kiukweli moyo wangu uliuma sana.

Kumbuka mpaka mida hiyo nipo tu mimi na yeye hapo nyumbani,Ema na Headmaster wako shuleni,swali nililokuwa nalo kichwani ni nani ataniamin?

Muendelezo Soma: Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe
no 10 tafadhali,
 
Wakuu nipo kijiweni,kuna muda naamua kuangalia tu comments za wadau,marafiki na ndugu zangu wa JF nabaki kufurahi tu[emoji23][emoji23].

Yaani kama unahasira za kijinga JF haikufai maana unaweza mrushia mtu ngumi ingawaje niya upepo[emoji23][emoji23][emoji23].

Humu kuna watu wanakera

Humu kuna watu wanaudhi

Humu kuna watu wanachukiza

Humu kuna watu wanafurahisha

Humu kuna watu wanajua kila kitu.


Yaani ukitaka kupata raha na karaha wewe tembelea JF [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

All in All nawependa sana ndugu zangu na tuonane muda si mrefu!
Umughaka...Mzee wa mizagazuguano...hongera sana kwa stori zako
 
Miaka hiyo ya 2004 hata nauli ya wanafunzi ilikuwa 50 tu na kitambulisho chako cha shule. hivyo ,100 ya enzi ya Mkapa ilikuwa na thamani kubwa sana. Waliozaliwa juzi JK anatawala hawawezi kujua hilo.
Wajuaji wengi mkuu
Endelea achana nao hao na kingine waambie huo mwaka nauli ya daladala ilikua 150 wakati nauli ya kutoka Dar mpaka Moro uliwa ndani ya Abood Andare Class nauli 2500
Wakati sasa daladala 500 nauli ya Abood Yutong Dar mpaka Moro 10000.
Ungewaongezea na tusi lingine mkuu.
 
Wadau huu uzi una page 103,anayeweza kunipa link ya page ya 50 wadau,natumia kiswaswadu nashindwa kuipata unless niende next kuanzia page 1 mpaka 50
 
Shukran sana mkuu
 
Tayari nina off days siku 3, nimeanza kuandika

Safi sana mkuu
 
Mods, tunaomba mtusaidie kupanga zile sehemu zinazofuata ili ziwe chini ya kila episode au hata ziwe zote mwisho wa episode ya 1 ili iwe mtu unabonyeza tu kusoma sehemu inayofuata.
YinYang Maxence Melo
 
Back
Top Bottom