Tulichosema kuhusu Kigamboni kimetimia: Tukimbilie wapi?

Tulichosema kuhusu Kigamboni kimetimia: Tukimbilie wapi?

Santa Matuta,
Unapozungumzia TAIFA kuwa linatakiwa kuweka maslahi ya wananchi wake mbele! - una maana gani!..maanake tusije kuwa tunazungumza lugha mbili tofauti.
Maslahi ya wananchi ni yepi hayo kuwa na kiwanja Kigamboni?... Je, unafikiria uwekezaji ktk sehemu hizo ni maslahi ya wageni - kivipi, ikiwa uwekezaji huo utaongeza pato la taifa, ajira kwa wananchi..Nini hasa maslahi ya wananchi ikiwa Taifa lenyewe halina maslahi!

Hiyo Karikoo kumewekeshwa kitu gani mkuu wangu ebu nifahamishe maanake nijuavyo mimi ni maghorofa yasiyokuwa na elevator (lift), hakuna maji yakutosha, sewerage system mbovu na zaidi ya yote ilitakiwa kuwa residential area badala yake leo hii kila nyumba ina mlango wa Convenience store..Yaani mji unanuka sawa na mwanamke aliyepaka vipodozi mwili mchafu..

Jaribu kuitazama Dar ya kesho kwa jicho tofauti kabisa na Kariakoo ama Sinza!.. tunahitaji zaidi sehemu za uwekeshaji na sio lazima wawe wageni toka nje hata sisi wenyewe Watanzania tunaweza kabisa kujenga Mahotel ya Kitalii kwa kupitia Franchise kama Sandals ambayo inaongoza ktk kuvuta Watalii ktk visiwa vya Carribean...Feza yako tu mkuu ukiweka down payment nzuri watakupa mchoro wa uhakika..lakini binafsi sikubaliani ugawaji wa viwanja kwa kutumia mifano ya Uswazi - Kariakoo ati kuna maghorofa..
Sehemu za uwekeshaji iwe ya uwekeshaji kama Mahotel ama Ofisi na viwanja vitoke kwa madhumuni hayo kutokana na plan ya mji na plan ya ujenzi wa jengo isiwe viwanja kugawiwa ovyo kwa mtu yeyote anayewahi utafikiri sisi ndio wahamiaji..

Mkuu tunahitaji zaidi sehemu za Uzalishaji karibu na mji kuliko residential na sioni sababu kwa nini watu tusitafute viwanja Bunju kuelekea Bagamoyo, Mbagala, na sehemu nyingine nje ya mji ambako bado kunahitaji wakazi zaidi.. zaidi ya hapo ndio bora zaidi kuanzisha makazi mapya ya Uswazi baada ya kuuza Kariakoo..Ninafahamu kwa uhakika wengi wetu tumeuza nyumba za Kariakoo na kuvamia Kigamboni kwa kasi ya mtaji sasa dau linageuka na hatutaki kuuhama mji.. Kigamboni beach haiwezi ama niseme haipendezi kuwa makazi ya watu unless unataka kujenga Condos ktk baadhi ya sehemu zitakazo ruhusiwa...
Kinachoweza kunitisha mimi hapa ni uwezekano wa baadhi vigogo kuchukua viwanja vya watu waliokwisha pewa kwa ajili yao wenyewe! lakini kama kuna mpango wa kuijenga Kigamboni iwe kama Montigo Bay huko Jamaica au kama sehemu za visiwa vya Carribean zilizotengwa ili kuvutia Watalii wakajenga Mahotel kwa kutumia wawekeshaji kama Sandals..
Ikiwa leo hii tunasisitiza Kilimo na viwanda iweje tusiwe na msisitizo ktk Utalii!.. Je, ni kweli tunapojenga misingi hii huwa hatufikirii maslahi ya wananchi ambao wanatafuta sehemu za makazi yao!..Hivi kweli tunaweza kuuza sehemu za mashamba na viwanda kwa ajili ya ujenzi wa makazi (residential)..kisha tunalalamika kuwa nchi haina kazi.

Mkuu mimi sina noma kabisaaa na Kigamboni kuwa eneo la kukuza Utalii nchini, najua nini malipo ya Utalii kama huo badala ya kutegemea wanyama na Mlima Kilimanjaro kwa sababu nieona.. Kisiwa kidogo kama Santa domingo kinapata watalii wengi kuliko Tanzania hapo hujagusa kabisa viwsiwa kama Bahamas na hata Jamaica.. Cuba na Ukomunist wao bado wanaheshimu Utalii na ndio kula yao sasa haya maslahi unayozungumzia mkuu ni yepi!
 
Tanzania kinachotumaliza ni ubinafsi na ile tabia ya 'kuchukua chako mapema' kwakweli nchi inapoelekea ni pabaya kuliko tunavyofikiria viongozi wetu kwa kushirikiana na wenye pesa wachache kutwa kucha hawalali wakifikiria ni kwa jinsi gani watazidi kumnyonya na kummaliza kabisa mtanzania wa kawaida. Inatia uchungu kuona watu wanajitahidi kujikwamua kiuchumi ila jitihada zao zinadhulumiwa na wenye uchu wachache.
Hili la ardhi Kigamboni linaweza kuendeshwa vizuri kihalali bila kumwumiza mtu yeyote ila kwa tamaa iliyopo Tz sitashangaa kuona wanaoumia ni maskini ila wakubwa viwanja vyao haviguswi.
Tanzania ninaipenda ila inanikatisha tamaa siku hadi siku.
 
[COLOR="Navy"]Tanzania kinachotumaliza ni ubinafsi na ile tabia ya 'kuchukua chako mapema' kwakweli nchi inapoelekea ni pabaya kuliko tunavyofikiria viongozi wetu kwa kushirikiana na wenye pesa wachache kutwa kucha hawalali wakifikiria ni kwa jinsi gani watazidi kumnyonya na kummaliza kabisa mtanzania wa kawaida. Inatia uchungu kuona watu wanajitahidi kujikwamua kiuchumi ila jitihada zao zinadhulumiwa na wenye uchu wachache.
Hili la ardhi Kigamboni linaweza kuendeshwa vizuri kihalali bila kumwumiza mtu yeyote ila kwa tamaa iliyopo Tz sitashangaa kuona wanaoumia ni maskini ila wakubwa viwanja vyao haviguswi.
Tanzania ninaipenda ila inanikatisha tamaa siku hadi siku.[/COLOR]
[/QUOTE]

Mkulu Tonga,

Heshima mbele,umeeleza yale ambayo labda kwa sababu ya hasira na mwuono wa kudhurumiwa haki nimeshindwa kuyazungumza.Lkn sio neno atleast inatia moyo kuona kuna watu wanaona yale ambayo watu wengine wanafichwa wasiyaone.

Mkulu Mkandara,

Thumb down brother!

Nataka ujue sikataii mifano yako mizuri ya utarii endelevu,pamoja na mji ulio bora kama miji uliyo itolea mifano.
Lakini hivyo vitu vyote na mambo yote mazuri yanawezekana tu kwenye inchi zenye kufata UTAWARA BORA na zenye mipango na dhamila za kweli towards maendeleo ya ukweli kwa JAMII YOTE.
Labda ningekushauri kabla haijawa too late nenda pale ARDHI MAKAO MAKUU nenda kaombe ramani ya kigamboni kutoka MJI MWEMA kwenda KISOTA na MBWA MAJI kupitia KIBUGUMO MPAKA GEZAULOLE,utaona yale ninayo yasema mimi.Yaani tayari ramani ya maeoneo hayo ilishachorwa na katika mpango wa huo MJI MPWA na Ramani za mipango miji zilisha kuwa-signed toka 1998.
Serikali kwa mujibu wa mipango yake ilianza kupima maeneo toka MJI MWEMA kwenda KULIA KIBADA na KISOTA wakaishia maeneo ya kwa GWAZO na kusema kwamba,''Kwakua serikali haikua na fedha za kukamirisha mradi huu,basi wananchi wenye maeneo hayo waendeleze kwa kupima maeneo yao kwa kufata ramani za mji mpya pamoja na mipango miji"
Sasa utaona au kuelewa kwamba mimi,sisi tulio pima tulifata ushauri nwa serikali sasa baada ya kuyaendeleza maeneo yetu linatoka KATAZO na hata wale ambao walikua wanachukua MIKOPO kwa kuweka dhamana nyumab zao zilizoko Kigamaboni hawawezi kufanya hivyo tena kwani katazo hilo limepelekwa mpaka kwenye taasisi za fedha.
Na wakati huu huu katazo hilo halielezi kwa kina ni kwa ajiri ya sababu zipi.
 
Santa Matuta,
Mkuu mbona tunarudia yale yale tuliozungumza zamani..
Nilisema kutokana na Ufisadi uliokuwa ukiemndelea inawezekana kabisa mlifungiwa kanyaboya..
Mimi nimekwisha kwenda wizara ya ardhi na kupimiwa kiwanja ambacho tayari kilikuwa na mtu mwingine na nikapewa File langu kabisa, Kuna kiwanja nilikuwa nacho Mikocheni toka mwaka '84 lakini miezi michache tu tulikuwa wamiliki kama wanne hivi.

Binafsi sikatai kabisa kuwa kuna mchezo lakini kama serikali ina mpango mwingine tofauti na mipango iliyopitishwa toka enzi za Mkapa...wakaona umuhimu wa kutumia Kigamboni kuwa sehemu maalum ya kivutio cha Watalii, sioni noma kabisa... Hata huku Ulaya kuna sehemu hubomolewa na kujengwa upya sehemu za Uzalishaji, iwe hata kiwanja cha mpira tu..

Nakumbuka kuna waziri mmoja aliyasema haya kuhusiana na kujengwa kwa daraja la Kigamboni na kwamba litajengwa kama nilivyopendekeza hapa kijiweni kurahisishwa traffic toka mjini..
halafu mkuu kumbuka tu kuwa mimi huwa naandika hapa kama sehemu ya kutoa mchango wangu na sio kabisa kuwa niko hapa kubishana tu na kuwa mtazamo wangu ndio bora..Laa hasa ni ktk kutazama hiyo shilingi upande wa pili ambayo sio lazima utekelezaji wake utakuwa mzuri.

Maswala ya viongozi wabaya ambao wanataka kupotosha Umma ama kutumia sheria kwa manufaa yao binafsi nadhani sasa hivi watakuwa na wakati mgumu zaidi, na hofu yetu sote, mimi na wewe ni pale tunapofahamu kwamba hatuna viongozi wazuri isipokuwa wenye tamaa za Utajiri.
 
Heshima Mbele,

Nina Habari hapa,ila nashindwa kuthibitisha.Naoma tusaidiane ku connect to the dot..

1.Kwanini huo mradi mipango yote imeanzia marekani?

2.Kwanini iwe haraka hivyo na lazima mradi uanze 2011

3.Kwanini kuna baadhi ya watu ,wafanyabiashara maarufu ndiyo wameuziwa badhi ya viwanja huko?

4.Hivi ni kwanini George alikaa muda mrefu hapa Tanzania?

Kuna habari nimepewa muda huu,bado nazifanyia utafiti ila am speechless
 
Mkuu Gembe
Labda ndo mambo ya Mkulu kutimiza ajira milioni moja. Ila mimi bado naumia kichwa hapo nilipomwagia wino. Kuna matajiri kweli kweli eneo moja...sijajua kama ni kuwahamisha watalipwa kiasi gani au ndio mpango wa kuwatajirisha wachache kwa umaskini wa wengine?
 
jamani, hivi uo mpango ni kigamboni yote mpaka kibada na kule ngamiani kwenye zoo? naomba kueleweshwa
 
Mkandala,

Hii hii story ya kusema wanajenga ili kuvutia utalii unainunua? Kama hawa jamaa wangekuwa na nia nzuri basi tungeiona kwenye madini. Badala ya kuata 3 % tungpata atleat 40+. Sasa leo tuwaaminije kuwa wana nia nzuri na nchi zaidi ya kututosa????
 
Wakulu natafuta wadau ili kuaandamana mpaka wizarani tupate TAMKO lasmi
 
jamani, hivi uo mpango ni kigamboni yote mpaka kibada na kule ngamiani kwenye zoo? naomba kueleweshwa

Huo ni mpango wa kujenga mji wa kisasa ambao unachukua kata 4 ambazo ni Kibada Kigambaoni Mjimwema na Vijibweni kule kwenye Ngamia haufiki maana hiyo ni kata ya Kisarawe 11 wizara bado inauaanda nitakupeni taarifa kadri unavyoendelea
 
shukrani ndugu Ipole, maana moyo ulikuwa mdundo mdundo, sasa huko Vijibweni kama mtu una kajumba ambacho hakana hati sijui itakuwaje.
 
Wakulu natafuta wadau ili kuaandamana mpaka wizarani tupate TAMKO lasmi

Wewe ndio umeamua ndugu yangu, hii sirikali yetu inataka kutupeleka peleka inavyotaka yenyewe,

MIMI NAKUUNGA MKONO KUHUSU MAANDAMANO MPK TUPATE MUAFAKA NI NINI HATMA YA WAKAZI WA KISIWA CHA KIGAMBONI.
 
Jamani mwenye Dta zaidi atuoe ili tuweze kufunguka Macho maana Kila mahali nasiki hili nikigeuka huku nasikia hili.

Naombeni mwenye Full Data azimuvuzishe huku kwenye JF
 
Santa Matuta,
Unapozungumzia TAIFA kuwa linatakiwa kuweka maslahi ya wananchi wake mbele! - una maana gani!..maanake tusije kuwa tunazungumza lugha mbili tofauti.
Maslahi ya wananchi ni yepi hayo kuwa na kiwanja Kigamboni?... Je, unafikiria uwekezaji ktk sehemu hizo ni maslahi ya wageni - kivipi, ikiwa uwekezaji huo utaongeza pato la taifa, ajira kwa wananchi..Nini hasa maslahi ya wananchi ikiwa Taifa lenyewe halina maslahi!

Hiyo Karikoo kumewekeshwa kitu gani mkuu wangu ebu nifahamishe maanake nijuavyo mimi ni maghorofa yasiyokuwa na elevator (lift), hakuna maji yakutosha, sewerage system mbovu na zaidi ya yote ilitakiwa kuwa residential area badala yake leo hii kila nyumba ina mlango wa Convenience store..Yaani mji unanuka sawa na mwanamke aliyepaka vipodozi mwili mchafu..

Jaribu kuitazama Dar ya kesho kwa jicho tofauti kabisa na Kariakoo ama Sinza!.. tunahitaji zaidi sehemu za uwekeshaji na sio lazima wawe wageni toka nje hata sisi wenyewe Watanzania tunaweza kabisa kujenga Mahotel ya Kitalii kwa kupitia Franchise kama Sandals ambayo inaongoza ktk kuvuta Watalii ktk visiwa vya Carribean...Feza yako tu mkuu ukiweka down payment nzuri watakupa mchoro wa uhakika..lakini binafsi sikubaliani ugawaji wa viwanja kwa kutumia mifano ya Uswazi - Kariakoo ati kuna maghorofa..
Sehemu za uwekeshaji iwe ya uwekeshaji kama Mahotel ama Ofisi na viwanja vitoke kwa madhumuni hayo kutokana na plan ya mji na plan ya ujenzi wa jengo isiwe viwanja kugawiwa ovyo kwa mtu yeyote anayewahi utafikiri sisi ndio wahamiaji..

Mkuu tunahitaji zaidi sehemu za Uzalishaji karibu na mji kuliko residential na sioni sababu kwa nini watu tusitafute viwanja Bunju kuelekea Bagamoyo, Mbagala, na sehemu nyingine nje ya mji ambako bado kunahitaji wakazi zaidi.. zaidi ya hapo ndio bora zaidi kuanzisha makazi mapya ya Uswazi baada ya kuuza Kariakoo..Ninafahamu kwa uhakika wengi wetu tumeuza nyumba za Kariakoo na kuvamia Kigamboni kwa kasi ya mtaji sasa dau linageuka na hatutaki kuuhama mji.. Kigamboni beach haiwezi ama niseme haipendezi kuwa makazi ya watu unless unataka kujenga Condos ktk baadhi ya sehemu zitakazo ruhusiwa...
Kinachoweza kunitisha mimi hapa ni uwezekano wa baadhi vigogo kuchukua viwanja vya watu waliokwisha pewa kwa ajili yao wenyewe! lakini kama kuna mpango wa kuijenga Kigamboni iwe kama Montigo Bay huko Jamaica au kama sehemu za visiwa vya Carribean zilizotengwa ili kuvutia Watalii wakajenga Mahotel kwa kutumia wawekeshaji kama Sandals..
Ikiwa leo hii tunasisitiza Kilimo na viwanda iweje tusiwe na msisitizo ktk Utalii!.. Je, ni kweli tunapojenga misingi hii huwa hatufikirii maslahi ya wananchi ambao wanatafuta sehemu za makazi yao!..Hivi kweli tunaweza kuuza sehemu za mashamba na viwanda kwa ajili ya ujenzi wa makazi (residential)..kisha tunalalamika kuwa nchi haina kazi.

Mkuu mimi sina noma kabisaaa na Kigamboni kuwa eneo la kukuza Utalii nchini, najua nini malipo ya Utalii kama huo badala ya kutegemea wanyama na Mlima Kilimanjaro kwa sababu nieona.. Kisiwa kidogo kama Santa domingo kinapata watalii wengi kuliko Tanzania hapo hujagusa kabisa viwsiwa kama Bahamas na hata Jamaica.. Cuba na Ukomunist wao bado wanaheshimu Utalii na ndio kula yao sasa haya maslahi unayozungumzia mkuu ni yepi!

Mimi naona ndugu yangu wewe huna uchungu cos huna eneo ambalo umelighalamia na serikali inataka kukunyang'anya.

Sehemu za kuwapa hao wawekezaji zipo nyingi tu mfano wangewapeleka hao wawekezaji nje kabisa ya mji kama KIMBIJI na maeneo mengine kama hayo. Tangu lini sehemu za uzalishaji zikawa karibu na mjini kama sio uchafuzi wa mazingira???????

Mfano mdogo tu tembelea pale mwenge maeneo ya viwanda na uone uchafuzi wa mazingira ulivyo, wanaoathirika ni wakazi wa karibu na eneo lile. Mimi nionavyo udhalishaji unatakiwa ufanyike nje ya mji na sio karibu na mjini.
 
Huo ni mpango wa kujenga mji wa kisasa ambao unachukua kata 4 ambazo ni Kibada Kigambaoni Mjimwema na Vijibweni kule kwenye Ngamia haufiki maana hiyo ni kata ya Kisarawe 11 wizara bado inauaanda nitakupeni taarifa kadri unavyoendelea

Sawa mkulu,
Lakini vp wale tayari wanamaeneo wanayo yamiliki kiharali kwa maan ya Offer na Hati je wataathirika?
Katazo halieleweki linasema,"Usiendeleze ama kupima" je kwa wale wanao malizia ujenzi?

Kama uko karibu na waheshimiwa tafadhali tufahamiske nini malengo
 
Sawa mkulu,
Lakini vp wale tayari wanamaeneo wanayo yamiliki kiharali kwa maan ya Offer na Hati je wataathirika?
Katazo halieleweki linasema,"Usiendeleze ama kupima" je kwa wale wanao malizia ujenzi?

Kama uko karibu na waheshimiwa tafadhali tufahamiske nini malengo[/QUOTE)

Nadhani utakadiliwa ulipwe kiasi gani na utapewa eneo nnje ya mji.

Tusubiri hiyo January tutajua nini hatma yetu, inauma kwa kweli.
 
Sawa mkulu,

Nadhani utakadiliwa ulipwe kiasi gani na utapewa eneo nnje ya mji.

Tusubiri hiyo January tutajua nini hatma yetu, inauma kwa kweli.

Hapo ndipo "mtu mweusi" anaponichosha!!!!!!!!!!!!!!!! Lini tutaamka?
Yaani mtu mweupe akija na kampango uchwara unabeba tu!
Yaani kiongozi unaona ni halali kwa watu wako "kunyang'anywa ardhi na kupewa mtu mweupe eti mwekezaji? anawekeza nini ? Kama wapi walipowahi kuwekeza tukaona matokeo mazuri????.

Leo hii maskini mtu amejikusanyia vijisenti vyake hadi akanunua kiwanja amejenga vyumba viwili amepumzika kulipa kodi. Ghafla unamwambia una "mpango wa kuundeleza jiji" mpango gani???????? Hapo Posta mvua yenyewe ikinyesha dak 5 tunatafutana...maji yamejaa kila mahali.
Inabidi wananchi tuamke.. tuachane na hizi bla bla...sasa hata kama ni Bush anataka eneo kwa akili zako timamu unaenda kumpa kata 4 "zilizoendelea kupita zote". Mtu tayari ni Maskini unapelekwa kwenye umaskini zaidi! Eneo gani watakalowagaia hawa watu waridhike???

Isitoshe huu ni ufanyaji kazi usio na tija..unatoa tamko una timeframe wala maelezo yanayofuata!Yeye mwenyewe aliyetoa tamko ukimwita sasa hivi hana jibu la hakika. Tayari mwananchi alikuwa na mpango wake wa kueleweka ..mwingine anamalizia nyumba ...mwingine anataka mkopo...

Unaambiwa "uvute subira" yaani wewe ukae tu mpaka yeye atakaposema tena!

Ni lazima mtu mweusi afike mahali ajue kuwa hii ardhi na vyote vilivyopo alipewa na Mungu kama mtu mwingine yeyote na he deserves the best!
 
Domo Kaya,
Hapana mkuu, sio kweli na kama ungekuwa ukifuatilia hoja zangu humu JF ungeelewa nimesha poteza...
Halafu sidhani kama ni lugha nzuri kutumia neno umepoteza kwani gharama ya fedha ambayo inaweza kufidiwa, haiwezi kulinganishwa na sisi tuliopoteza ardhi na mashamba...
Huu ndio Ubepari, na maendeleo ya Ubepari ni lazima kuna waathirika kwa maslahi ya Taifa..Uwekeshaji kwanza kabla ya maslahi ya Taifa na ndio maana unaona katika Ubepari GDP inapazwa mbele ya Human development..wakiamini kuwa uwekezaji zaidi unapandisha GDP, ambayo lengo lake ni kuboresha pia maisha ya wananchi wake.
 
nataka ujue ninaheshimu mchango na mawazo yako kwenye hili.
Lakini maelezo hayo hapo juu ni kama Lugha ya kiarabu ama kichina kwa mtu asiye fahamu lugha hizo.
Hizo techinicalies hazi apply kwenye inchi yenye uongozi mbovu na mipango hewa kama hii ya kwetu .
Maelezo ya MAMA LAO hapo juu ni tosha,ila tunahitaji kuonyesha kwamab hatujapendezwa na uendeshaji mbovu wa mpango huu na LAZIMA TUANDAMANE,shime jamani tujipange kuandamana
 
Back
Top Bottom