The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 822
- 2,095
Moja kati ya uwekezaji kichaa tuliowahi kufanya ni huu wa ndege. Narudia ili MATAGA wasije kuninukuu vibaya. Sisemi kwamba hatukupaswa kufufua ATCL, ila tulitakiwa kabla ya kufufua tuwe na mkakati wa kujua shirika litajiendeshaje.
Lakini hatukufanya hivyo. Tumefufua ATCL kichwakichwa bila kuwa na mkakati wa kibiashara. Matokeo yake ndio haya tunayoyasikia kwa CAG leo.
Kwa kifupi hakuna ndege ya ATCL inayoruhusiwa kuruka kwenye anga la kimataifa zaidi ya India ambapo tuna kibali. Tukienda hata hapo Sudani kwa maskini wenzetu tunakamatwa. ATCL inadaiwa na mamlaka ya usafiri wa anga kimataifa (ICAO) jumla ya TZS 47.4Bilioni ambapo 45Bil ni deni halisi na 12.4Bil ni riba.
Wakati huohuo ATCL inadaiwa Sh71.48 bilioni na wakala wa ndege za serikali (TGFA) ambayo ni tozo ya kukodisha ndege na fedha ya akiba ya matengenezo. Jumla walikua wanadaiwa 79.62 bilioni, lakini wamelipa 8.14 bilioni, na hivyo kubaki na deni la 71.48 bilioni.
Wakati huohuo mwaka jana ATCL imepata hasara ya 60 Bilioni kwa mujibu wa ripoti ya CAG. Kama haitoshi ndege za ATCL zikiharibika leo haziwezi kutengenezwa kwa sababu ATCL haijalipa 71.48 Bilioni ambazo ni gharama za matengenezo.
Kwahiyo tumenunua ndege ambazo haziruhusiwi kuruka nje (zaidi ya India, Chato na Nyakanazi [emoji1]). Zikiharibika hazitengenezeki, na zinajiendesha kwa hasara ya mabilioni ya pesa kila mwaka. Tukiulizwa tunajitetea eti mashirika yote ya ndege hupata hasara. Uzwazwa.!
Mwendazake alikua na nia njema ya kufufua ATCL lakini hakutaka kushauriwa. Yeyote aliyejaribu kumshauri aliitwa kibaraka wa mabeberu. Nia njema ya mwendazake ilikosa mpango mkakati.
Ni sawa na mtu ana nia ya kuwa daktari lakini hajui asome nini. Kutokana na kukosa exposure anakomaa kusoma Agriculture na Geography. Ukimshauri masomo sahihi ya kusoma anagombana na wewe. Anaamini unataka kumkwamisha asifikie ndoto zake.
Mwishowe unamuacha aende anavyotaka. Akija kushtuka safari ya MUHAS imekufa anajikuta chuo cha ufugaji nyuki Tabora. Hiki ndicho kilichotokea kwa mwendazake. Kila aliyemshauri kwa nia njema aligombana nae. Akajikuta anaenda tu bila dira. Na matokeo yake ni haya yalioelezwa na CAG jana.