Tuliifurahia squid game, ila kwenye maisha halisi sio rahisi

Tuliifurahia squid game, ila kwenye maisha halisi sio rahisi

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
Nilisikia hii series ikitamba sana na ikapata umaarufu mkubwa watu walipokuwa wanauawa kwenye game na kujishindia pesa nyingi. Tangu game ya kwanza mauaji yaliyokuwa yanafanyika hayakuwa justified lakini ile movie ilipata umaarufu mkubwa. Waliopenda game ile ni watu wengi ikiwemo watu wa haki za binaadamu na wengineo.

Squid game, au kitu kama hiko kimetokea Tanzania na imekuwa ni hali tofauti. Yes! ukiona zile maiti unagundua tarehe 29 ilikuwa Tanzanian political squid game. Game ambayo kama kawaida inaendelea kupata justification kwa inaowanufaisha huku mataifa na wanaharakati wakilaani.

Tofauti ya Squid game na Tanzania ni kuwa, japo imekuwa maarufu neno sahihi la kiingereza ni "Infamous" suala ambalo linahatarisha uchumi wa nchi. Ikumbukwe Tanzania, ni nchi ambayo inajikongoja kutokana na kutokuwa na strong instutitions, hivi vitisho vya fedha nyingi kuondolewa wakati huu ambao nchi haina capacity ya kukusanya mapato ya ndani inaongeza shida. Yaani, kuna haja ya kujiweka sawa kimataifa ili kuweka sawa hali hii kwa miaka kadhaa ijayo.

Ieleweke kuwa uwezo wa nchi ni jambo la msingi sana kwenye kukabiliana na vikwazo. Sisi sio kama Urusi ambao hata baada ya vikwazo wameendelea kuishi tu. Kwa nchi kama Tanzania, huu wingi wa vikwazo utaleta shida sana na machafuko ambayo yatasababisha majanga zaidi.

Ni muda wa kuwa na busara sana. Na sio kusigishana au kuleta masuala mengine yanayozidisha petrol kwenye moshi unaofuka.

Wito wangu kwa Tanzania ni kuhakikisha kurejesha amani, kuaminiana, umoja na mshikamano kama ulivyokuwa. Turudishe utawala wa sheria.

Nawasilisha.
 
Samuya anajua urusi itampa msaada kumbe ni silahaa.
Samuya anajua waarabu watampa msaada kumbe waje kuchota madini mpaka mbuga.
samuya anajua wachina watampa msaada kumbe wajazane kwetu mpaka wasema nchi ni yao.
 
Back
Top Bottom