(a) Hatujali kabisa ethics za kazi; nadhani hili linaeleweka sana.
(b) Hatujitumi kazini katika majukumu ambayo hayana rushwa; hatuogopi utendaji mbovu.
(c) Tunapowewa madaraka, tunaamini kuwa tuko entitled kuwa na madaraka hayo, na tunaweza kujipatia chochote kutokana na madaraka hayo.
(d) Tunathamini sana mali kuliko heshima; tuko tayari kulamba kiatu cha mwekezaji ili atupatie kitu kidogo.
(f) Tunapenda sana njia za mkato kwa kila kitu. Tukiwa na matatizo tunapenda kumtafuta mtu mwingine atutatulie
(g) Hatutaki kuwajibika wala kuwawajibisha tuliowapa majukumu. Kila wakati tunaamini kuwa tuko right, yanapotokea makosa katika mazingira yetu basi tunakuwa wa kwanza kutafuta mtu au kitu cha kulaumu; tukikosa kitu cha kulaumu basi tunamlaumu Mungu.
Mambo haya yameungana kiasi kuwa ni huwezi kuondoa moja ukaacha mengine. Kwa bahati mbaya mambo hayo ndiyo yanasoababisha tunashindwa kuendelea.
Nina maswali mawili ya kujiuliza:
(a) Ni wapi tulipokosea hadi tukajenga element mbovu hizo katika maisha yetu?
Nina imani hali ngumu ya uchumi iliyosababisha mapato halali ya wananchi kupungua vilisaidia kusababisha watu waanza kuachana na ethics za kazi kwa kutafuta rushwa, na kuanza kutumia nafasi za kazi zao kufanya biashara kinyume na masharti ya kazi. Lakini je kweli hiyo ndiyo iliyokuwa sababu pekee? Wizi wa mabilioni ya fedha za umma kweli ni kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi? (b) Je tufanye nini sasa ili kurekebisha makosa hayo?
Mkuu Kichuguu na wanajamvi, ni kweli kuwa kuna mwingiliano mkubwa sana wa hayo aliyoorodhesha kichuguu.
Ninakataa kabisa kuwa kuvunja maadili, rushwa,kutowajikani hulka ya Mtanzania. Maana ya hulka ni kitu kilichopo kati 'genes' za Watanzania au basi kama si genes ni utamaduni.
Ninayo mifano ya hapa nchini ambapo mfanyakazi wa serikali anaacha kazi na kuajiriwa na shirika au taasisi nyingine.
Mtu huyo kwa siku moja anabadilika kabisa katika utendaji, maadili na uzalishaji (delivery).
Wafanyakazi wengi waliokuwa katika benki za taifa walihamia katika mabenki binafsi, huko ndiko wanafanyakazi na mabenki hayo yanapata faida kila siku. Hawajabadilika chochote isipokuwa mazingira tu ni kwanini?
Kinachosababisha hali hiyo ni mnyororo wa uzembe kuanzia juu hadi chini. Hivi ni nani ataamka saa 11 ili awahi kazini saa 2 wakati mkuu wake wa kazi afike saa 5 na kuanza kunywa chai halafu saa 7 anaelekea kwenye kongamano!
Ni nani anaweza kufika kazini saa 3 ikiwa kiongozi wake yupo ofisini saa 1 asubuhi.
Mfanyakazi gani atakuwa na morali ya kazi kuwahudumia wateja wake kwa bidii wakati boss wake anawatu wake wanaokuja kwa wakati wao na kuondoka shida zao zikiwa zimamalizwa ndani ya dakika 10.
Ni nani ana munkari wa kazi kuhudumia jamii kwa kuamka saa 10 usiku awahi dala dala wakati anapoingia getini anakutana na VX zikitoka kwenda kuchukua watoto na wake za maboss kuwapeleka sokoni, mashuleni na kwenye birth day!
Rushwa: Ni mfanyakazi gani anayepokea laki 2 kwa mwezi anaweza kuacha sh 10,000 akisikia kuwa maisha kwa mkuu wake wa kazi ni magumu sana kiasi kwamba amechukua 10% ya mradi wa bilioni 10.
Kwamba mkuu wake wa kazi licha ya mambo yote anayoyapata bado anachukua 10% sasa yeye afanye nini na laki 2 kwa mwezi.
Ni mfanyakazi gani wa sh laki 2 anayejisikia raha akisikia kuwa boss wake wanayefanya naye kazi kila siku ana account ya dollar laki 7. Hivi tumesahau kuwa hawa wafanyakazi ni wanadamu kama walivyo wengine.
Tufikirie, hivi katibu mkuu anapotoa rushwa na kuachiwa astaafu ili atumie rushwa yake vizuri hilo linaingiaje akilini mwa wafanyakazi wenzake.
Hadi hapo nihitimishe kwa kusema, kila tatizo ni zao la tatizo. Watanzania wapo duniani kote na wanafanya kazi kwa ari, maadili na misingi yake. Tunachokiona Tanzania ni tatizo la mfumo wetu wa uongozi. Hatuna uongozi wa kufuata kanuni na maadili. Tuna uongozi uliojikita katika kufikiria matumbo yao na familia zao.
Kuharibika kwa maadili na kuenea kwa rushwa,kutowajibika chimbuko lake ni uongozi mbovu wa nchi. Haiwezekani nchi iongozwe kwa tume kila siku hata pale uzembe ni wa dhahiri. Haiwezekani nchi iendeshwe kishikaji kwa kuangalia marafiki halafu tutegemee matokeo tofauti. Fikiria ni jambo gani lililoleta malalamiko miongoni mwa jamii limefanyiwa kazi kama si usanii wa tume na shtaka lipo mahakani.
Wezi wote na wala rushwa wote wanaishi katika pepo ya Tanzania, ni nani mwenye moyo wa chuma wa kuijali Tanzania zaidi ya wale wenye pepo yao. Ni kwanini nidhani karani anahujumu taifa na si genge la TANESCO linaloua taifa.
Ni kwanini waziri awajibishwe na kelele za bunge badala ya serikali kulitaarifu bunge juu ya kumwajibisha waziri.
Kinachotokea ni kukata tamaa kwasababu katika nchi ya Tanzania karani peke hawezi kuleta mabadiliko kama viongozi wake ni wala rushwa kama wabunge, ni watu wa 10% kama mawaziri na ni wahongaji kama katibu mkuu.
Tufanye nini?
Tumekosa fursa muhimu sana ya kuandaa utaratibu utakaotuongoza kama nchi.
Nafasi ya kuandika sheria na taratibu za nchi yetu tumewakabidhi wale wale wanaongoza kwa tume, rushwa, kutowajibika n.k. Fursa ya kuandika katiba ndiyo ingetupa japo pa kuanzia, kwasasa haipo.
Tumewaamini wajifungie Serena Hotel na kuandika taratibu zitakazowalinda wao kazini na baada ya kustaafu. Kuandika utaratibu wa kulindana katika uhalifu. Wenyewe wanatuaminisha ni tume ya katiba! Hapa ndipo tulipobofoa na naomba muweke maneno haya katika kumbu kumbu ili siku moja munihukumu au munipongeze.