KERO Tulilipa Ada Veta Mbeya, hatukusoma kwa vitendo, hatujapewa Leseni, tukiuliza wanatuzungusha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni dereva wa malory nimesoma VETA Mbeya tangu mwezi Juni 2026 lakini mpaka leo hatujapata vyeti, leseni zimeisha tunashindwa kuhuisha leseni zetu tulio wengi kazi tumeachishwa kwa kutokuwa na leseni, familia zetu ninahali mbaya😭

Wanasema japo si taarifa rasmi ya chuo ni kwamba kilifungiwa kutoa mafunzo ya Daraja C na E kwa kuwa hawana magari ya kujifunzia madaraja husika, tukauliza why walitupatia Control Number na ada tukalipa wakati wanajua changamoto waliyonayo, wanasema tusubiri tutaitwa kufanya mtihani wa Polisi.

Pia soma ~ Tunaojifunza magari VETA Mbeya, magari mengi ni mabovu

Control Number ni za Serikali kabisa na siyo za utapeli, hata darasani tulisoma theory tu bila kufanya practical, kwa maana hatukufanya vitendo, tulipohoji wakasema tutafanya mitihani ya Polisi.
 
Veta wana hilo tatizo siku nyingi sana kwenye kutoa vyeti sijui huwa wanachangamoto gani hata fani zingine
 
Mimi ni dereva wa malory nimesoma VETA Mbeya tangu mwezi Juni 2026 lakini mpaka leo hatujapata vyeti, leseni zimeisha tunashindwa kuhuisha leseni zetu tulio wengi kazi tumeachishwa kwa kutokuwa na leseni, familia zetu ninahali mbaya😭

Wanasema japo si taarifa rasmi ya chuo ni kwamba kilifungiwa kutoa mafunzo ya Daraja C na E kwa kuwa hawana magari ya kujifunzia madaraja husika, tukauliza why walitupatia Control Number na ada tukalipa wakati wanajua changamoto waliyonayo, wanasema tusubiri tutaitwa kufanya mtihani wa Polisi.

Pia soma ~ Tunaojifunza magari VETA Mbeya, magari mengi ni mabovu

Control Number ni za Serikali kabisa na siyo za utapeli, hata darasani tulisoma theory tu bila kufanya practical, kwa maana hatukufanya vitendo, tulipohoji wakasema tutafanya mitihani ya Polisi.
Ni VETA zote Tanganyika, wanachukua hela halafu wanasema hakuna magari na hata hayo mafunzo kwa maneno hayafanyiki.
Nilipeleka mtoto wangu VETA Tanga na tukalipa halafu magari hakuna.
Wakaishia kuwatoza rushwa eti wanazipeleka Polisi ili wasifanye test wafaulishwe.
 
Back
Top Bottom