Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mi nadhani pamoja na sababu nyingine, pengine lugha inayochechemea pia ni sababu inafanya watu washindwe kusema kile wanachotaka kukisema katika maandishi.
Walishindwa nini kuandika hundi hiyo kwa lugha ya Kiswahili??!!
Walishindwa nini kuandika hundi hiyo kwa lugha ya Kiswahili??!!
Au waliandika haraka haraka kuwahi picha
Hapo sasa ndio nami najiuliza. Kulikuwa na ugumu gani kuandika 'shilingi milioni nne na laki nane tu'....
Sisi tunashangaza sana wakati mwingine. Tunalazimisha vitu pasipo na ulazima wowote. Ulazima wa kuandika kwa lugha ya Kiingereza kwenye hiyo hundi ulikuwa ni upi?
Au watasema Kiswahili hakina misamiati na maneno ya kutosha kama wasingiziavyo kwenye sheria zetu zilizoandikwa kwa Kiingereza? Yaani ni uzumbukuku mtupu hadi unatia kichefuchefu.
Mara nyingine tatizo wala si lugha, hata Kiswahili tunachotumia mara nyingi tu kina matatizo.Ni rahisi kusingizia Kiingereza kwa sababu ni lugha ya kigeni, lakini ushajiuliza nani anajua kuisema Roman Alphabet yote kwa Kiswahili ?
Mazee, tunaongelea lugha rahisi tu ya kawaida inayoweza kueleweka kwa wengi wetu, nomino na misamiati ya kutosha ipo inayoweza kutosheleza hilo kwenye swala kama hili bila ya kuingia kwenye asili na vyanzo vya maneno tuyatumiayo.
Mwe...kweli kazi tunayo! Umakini ni zero kabisa.
Sio swala la umakini wala lugha! Kwenye mahojiano na vijana wetu (kwa ajili ya kazi na darasani) usilogwe ukamuulize swali linalohusu tarakimu hata mara moja! Mwanzoni nilikuwa nawacheka lakini niligundua kumbe ni tatizo. Enzi zetu za kusoma tulikuwa tunakariri orodha ya 1 hadi 14 kama mnanipata. Halafu kukariri jinsi ya kuzitamka hizo tarakimu. Siku hizi hawafanyi hivyo, ukikutana na muuza duka kijana, ukataka soda 6 na kila moja ni shs 500/= kijana atafuta calculator. Tunawafundisha kuwa watumiaji wa mashine bila kujua kinachoendelea, tatizo ni hapo linaanzia.

Sasa na wewe badala ya kufagilia "kujua" vitu unafagilia "kukariri" vitu......SMH
Ndiyo maana hata wasomi wetu ni watu wa kukariri tu, hatuna wavumbuzi.Utavumbua nini wakati unasubiri kukariri bila kuelewa undani wa mambo ?