Mazee, tunaongelea lugha rahisi tu ya kawaida inayoweza kueleweka kwa wengi wetu, nomino na misamiati ya kutosha ipo inayoweza kutosheleza hilo kwenye swala kama hili bila ya kuingia kwenye asili na vyanzo vya maneno tuyatumiayo.
Umesema sawa kabisa katika swala hili, kwamba kutumia Kiswahili ingeweza kuwa rahisi zaidi.
Mimi naongelea swala kubwa zaidi katika makosa ya lugha ya kila siku, mara nyingi watu wanapokosea Kiingereza tunakuwa rahisi kulaumu kwamba Kiingereza ni lugha ya kigeni, lakini tukianza kuangalia hata tunavyoandika Kiswahili, hata hapa JF, hatuwezi kusema kwamba hata hicho Kiswahili ambacho ni lugha yetu tunakijua vizuri.
Kwa hiyo tatizo letu ni lugha na mawasiliano, pamoja na umakini. Utasikia mtu kakosea, unamsahihisha kwa mfano, halafu anakwambia "si umenielewa?" yaani hamna umakini, hamna kutaka kufanya mambo sawa, kila mtu anataka kulipua lipua tu aende zake.
Yaani kwenye hiyo hundi tatizo si Kiingereza tu, maana nina hakika kama mtu mmoja Kiingereza chake si kizuri, lakini kama kuna utamaduni wa kupitia vitu kwa macho ya pili, ku hakiki na kadhalika, watu wangeona makosa hapo.
Lakini naona Kiingereza ni tatizo, lakini zaidi ya hilo umakini ni tatizo kubwa zaidi.Tatizo linalotufanya hata Kiswahili chetu wenyewe tusikiweze.