SoC02 Tulinde kizazi cha watoto wetu wa kiume

SoC02 Tulinde kizazi cha watoto wetu wa kiume

Stories of Change - 2022 Competition

jamyoh

New Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
1
Reaction score
0
TUWALINDE NA KUWATUNZA WATOTO WA KIUME

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa ukuu wake katika maisha yangu, lakini pia nimshukuru Mungu kwa kuumba jinsia mbili hapa duniani, yaan jinsia ya kiume na jinsia ya kike, na zaidi ya hapo amegawanya majukumu ya kufanya kwa kila jinsia katika dunia hii, hivyo kila jinisa ina wajibu na kazi ya kufanya hapa duniani.

Nitajikita kuongelea zaidi watoto na vijana wa jinsia ya kiume kwasababu ni jinsia iliyosahauliwa sana katika jamii ikiaminika kuwa ni jinsia inayoweza ikajiendesha yenyewe bila usimamizi wala uangalizi lakini ni makosa makubwa tunayafanya kwani tunatengeneza kizazi kibaya na kiovu kijacho, hivyo ni lazima tuwalinde na kutowasahau watoto wa kiume katika malezi.

Watoto na vijana wa kiume wanakutana na changamoto nyingi za kimaisha na wanashindwa nini cha kufanya au kuamua kwasababu hawana muongozo na hivyo kusababisha kufanya maamuzi mabaya na kuingia katika vitendo viovu vya uvunjifu wa amani na kupoteza dira na maono ya maisha yao.

Na pia kupelekea familia zisizokuwa na misingi bora wa malezi yapasayo katika jamii, hivyo kuna haja kubwa na namna ya kufanya ili kuwasaidia hawa watoto na vijana wa kiume. Nini kifanyike?

Watoto wakiume wapewe elimu jinsi ya kutimiza majukumu yao na jinsi ya kutatua changamoto za kimaisha, watoto na vijana wengi wa kiume hawayajui majukumu yao katika familia na jamii kiujumla hivyo kuwafanya kuonekena kama wanayakimbia au kukwepa majukumu yao, vijana wakiume wapewe elimu ya jinsi ya kuhudumia familia. Siku hizi kuna tatizo kubwa la familia nyingi kulelewa na upande mmoja wa mzazi, haswa upande wa mama (single mothers) ili hali baba wa watoto hao bado wapo hai,vijana wengi wamekimbia majukumu ya kutunza familia na wengi wa vijana hawa ni tegemezi hivyo kuwaachia wamama wengi kuendesha familia wenyewe kwali hali ya tabu ,hivyo lazima vijana wa kiume wapewe elimu ya kujua majukumu yao na kutunza familia kwa matokeo mazuri ya kizazi kijacho.

Kuwafundisha na kuwalea watoto wetu na vijana wa kiume katika maadili na tamaduni za kwetu,watoto na vijana wengi wa kiume wamejingiiza katika tabia mbaya na ovu, kwa kuiga maadili na tamaduni za nchi nyengine, utambulisho wetu wa kitaifa umepotea, watoto na vijana wetu wamepokea mapokeo ya nchi nyengine tunaweza kusingizia utandawazi lakini kama wazazi, walezi na jamii kiujumla tukisimama katika nafasi yetu tunaweza kurudisha maadili na tamaduni zetu, serikali nayo inapaswa kusimamia katika hili kuhakikisha elimu zinazotolewa katika shule zote yaani shule binafsi na za serikali zinafuata maadili na tamaduni zetu ili kulinda utambulisho wetu kama taifa.

Watoto na vijana wa kiume wapewe elimu ya afya ya uzazi, watoto na vijana wengi wa kiume hawana elimu kuhusu afya za uzazi na mabadiliko yanayotokea wakati wa ukuaji wao, wengi hawajui jinsi ya kutunza viungo vyao vya uzazi na kukabiliana na changamoto zinazotokea katika viungo vyao vya uzazi hivyo kuleta shida katika kutunza viungo vyao vya uzazi, lakini pia watoto na vijana wengi wa kiume hawana elimu ihusuyo uzazi wa mpango na elimu hii kwa kiasi kikubwa inatolewa kwa vijana wa kike, lakini kwasababu vijana wa kiume ndio msingi wa familia wanapaswa kupewa hii elimu ili nao waweze kupanga uzazi salama.

Vijana wa kiume wapewe elimu ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi(ujasiliamali) , vijana wengi hawana elimu ya namna ya kujikwamua kiuchumi, wengi wanafanya biashara pasipo elimu maalumu ihusuyo usimamizi mzuri wa biashara na husababisha wengi kupata hasara na kutoendelea na biashara hizo, saccos nyingi na vikoba vinawahusu wanawake huku vijana wakiume wakiachwa wakiaminika kuwa wanaweza kujisimamia wenyewe lakini kiuhalisia vijana wengi hawana elimu hiyo na wengi wako katika kuhangaika na maisha bila mafaniko lakini wakipatiwa elimu itawasaidia sana katika maisha yao na kujikwamua kiuchumi.

Kuwepo na semina, makongamano na warsha mbalimbali zitakazo wasaidia watoto na vijana wakiume kuwa wazi na kuelezea changamoto wanazokutana nazo katika maisha na kuwasaidia katika kutatua changamoto hizo, Kiuhalisia watoto na vijana wengi wa kiume wanapitia changamoto nyingi lakini hawana sehemu ya kuelezea wanayoyapitia kwa uhuru zaidi hivyo huwafanya muda mwengine kuchukua maamuzi ambayo siyo sahihi, semina na warsha hizi zitasaidia kubadilishana mawazo na mbinu za kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Wazazi na walezi tusiwasahau watoto wa kiume katika malezi, wazazi na walezi tupate mda mzuri wa kuongea na watoto wa kiume, watoto wengi wanajiingiza katika tabia ovu za ushoga, uvataji bangi, wizi na madawa ya kulevya kwa kukosa usimamizi mzuri wa maisha yao, watoto wa kiume wanapitia changamoto nyingi ambazo zinahitaji utatuzi kutoka kwa wazazi na walezi, jamii nayo inapaswa kuwalinda watoto wa kiume kwani katika kundi linalopotea zaidi kimaadili ni kundi la vijana wa kiume.

Serikali nayo inapaswa kuingilia kati swala hili la kuwalinda watoto na vijana wa kiume, serikali ihakikishe wazazi wote wawili wanashiriki katika malezi ya watoto, itunge sheria itayao amuru wazazi wote wawili kushiriki katika malezi na kutowaachia wamama peke yao katika ulezi lakini pia itoe fursa za ajira nyingi kwa vijana, hii itasaidia vijana kuwekeza nguvu zao katika kazi na kuacha tabia mbovu, katika hili serikali lazima itafute namna nyengine ya kuupanua uchumi kuzipa nguvu sekta nyengine zinazoweza kuongeza uchumi nchini kama viwanda, michezo na teknolojia, sehemu kama hizi ndizo zimeweza kuwaajiri vijana wengi katika nchi zilizoendelea na kuongeza pato la taifa, kwa kufanya hivi vijana wengi haswa wakiume tutawalinda kutoka katika tabia ovu na mbaya katika jamii.

Tuwalinde watoto na vijana wa kiume kwani ndio wababa wa kesho wa familia, ndio jeshi na nguvu kazi ya taifa la sasa na lijalo, tusiache vijana wakaangamia katika ouvu na kukosa muelekeo, tuhakikishe kama jamii kwanzia ngazi ya familia kuwa tunatimiza ndoto za vijana hawa, ndoto nyingi za vijana zimekwama kwasababu walikosa muelekeo na dira ya wanakoelekea, hata vitabu vya dini vinasema pasipo maono taifa huangamia, lakini pia pasipo maarifa jamii na taifa na jamii pia inaangamia hivyo tunapaswa kuhakikisha kuwa tunatunza maono yao nakusimamia hayo maono ili yafanikiwe.

Tukilisahau kundi hili tutatengeneza taifa na jamii ovu baadae jamii isiyokuwa na maadili na heshima, hili ni swala la kila mtu kuhakikisha tunawakumbuka watoto na vijana wa kiume katika malezi.

JAMES YOHANA KIFWETE
0754818642/0714901233
 
Upvote 0
Back
Top Bottom