Uchaguzi 2020 Tulinganishe sera za Magufuli, Lissu na Membe

Uchaguzi 2020 Tulinganishe sera za Magufuli, Lissu na Membe

puza46b

Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
91
Reaction score
261
TULINGANISHE SERA ZA MAGUFULI, LISU NA MEMBE:

Tukielekea kwenye uchaguzi tumeanza kuona washabiki wakibezana na kuhoji sera za washindani wao. Wapo waliomwambia Lisu kuwa yeye ni kutukana tuu hana hoja. Kuna waliosema Magufuli anatumia vitisho na kulazimisha watanzania wampende. Na mwisho kuna wanaodai Membe katumwa na kitengo kufanya kazi yakuchafua upinzani na Zitto kabwe alikuwa project yake ya kuiharibu chadema.

Wahenga wanasema wahukumu watu kwa matendo yao kuliko maneno yao. Lakini pia kuna wale wanaosema muongeaji sana ni vigumu kuficha anachowaza.

Sasa basi, ningependa kutumia hii mada kuorodhesha hoja mbalimbali za hawa wagombea wetu wakuu watatu. Disclaimer: sijasoma ilani za vyama vyao nasinampango wa kuzisoma kwa sababu naamini kinachotoka midomoni mwao kinaonyesha nini wanawaza:

KATIBA
Lisu:
Atabidili katiba na ni swala atakalolishughulikia siku 100 za kwanza.​
Atapunguza madaraka ya Raisi kuondoa dhana ya Raisi mfalme​
Atawezesha miji, wilaya na kata ziwawajibishe watendaje wake kwa kufuta kuteuliwa.​
Atafanya bunge liweze kumuwajibisha raisi - raisi anatumikie watu na siyo vinginevyo​
Magufuli:
Hakurudisha muswada wa katiba bungeni​
Watendaji wote wanamtumikiwa raisi.​
Membe:
Atabadili katiba kama Lisu alivyosema. Sijaona uchambuzi wake zaidi​

WAKULIMA:
Lisu:
Atawapunguzia makato na vizuizi vya kuuza mazao​
Atawaruhusu wauze mazao popote wanakopata bei nzuri (bila kuangalia national food security)​
Atawapa uhuru wa kufanya biashara yao bila kuingiliwa​
Magufuli:
Analinda chakula kuwafae watanzania kwanza (national security)​
Yuko tayari kuingilia soko la mazao kama anaamini ni faida kwa taifa​
Membe:
Atawapunguzia makato kama lisu​
Atawapa uhuru wa kuuza mazao wapate faida​
Atatoa nyezoza kuwasaidia kwenye kilimo (hii zitto huiongelea sana)​
Ataanzisha bima ya kuwalinda wakulima (sera ya zitto pia)​

WAFANYAKAZI
Lisu:
Atawapandisha Madaraja​
Atawalipa hela zote ambazo hawakuongezewa miaka mitano iliyopita​
Magufuli:
Mishahara itapanda baada ya kumaliza kujenga miundo mbinu​
Membe:
Atawapandisha Madaraja​

VIWANDA
Lisu:
Ataweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kupunguza manyanyaso ya kodi​
Magufuli:
Inchi inahitaji viwanda kukua kiuchumi na kuondoa umaskini​
Tanzania ya viwanda inawezekana na atahakikisha mpaka 2025 uchumi wa viwanda umeimarika​
Membe:
Ataweka mazingira mazuri ya uwekezaji​

WAFANYABIASHARA
Lisu:
Ataondoa ubugudhaji wa wafanyabiashara​
Atabadili TRA ili isiwe chombo cha kunyanyasa wafanyabiashara​
Atapunguza kodi kwa wafanyabiashara​
Magufuli:
Kila mtu anawajibu wa kulipa kodi​
Membe:
Sera zake zinafanana na Lisu​

MAHUSIANO YA KIMATAIFA
Lisu:
Tanzania siyo kisiwa inahitaji mahusiano mazuri​
Atafufua mahusiano na nchi nyingine​
Magufuli:
Tanzania ni tajiri haiko tayari kudhalilishwa na nchi nyingine​
Yuko tayari kuvunja mahusiano kama hayana tija kwa taifa.​
Membe:
Atatumia ujuzi wake wa kidiplomasia kurudisha mahusiano ya kimataifa​

MIUNDO MBINU
Lisu:
Hata wakoloni walijenga miundo mbinu hivyo isitumike kuwanyanyasa watanzania​
Kila serikali inawajibu wakujenga miundo mbinu na yeye ataiendeleza​
Magufuli:
Anajenga miundo mbinu ili iwe chachu ya kukua viwanda.​
Miundo mbinu itawapunguzia gharama wafanyabiashara (reli na umeme)​
Membe:
Atahakikisha mradi wa bandari ya bagamoyo unakamilika​

ZANZIBAR
Lisu:
Zanzibar watakuwa na haki sawa katika muungano​
Zanzibar watapata fare share katika pato la taifa (hapa sikumwelewa kama alimaanisha nusunusu)​
Hataingilia kazi kubwa iliyofanya na Maalimu katika kutetea haki ya wazanzibari.​
Magufuli:
Haliongelei hili​
Membe:
Zanzibar watakuwa na haki sawa katika muungano​

MALIASILI
Lisu:
Atawaruhusu wawekezaji wa nje kushiriki kwenye kuvuna maliasili​
Hatuna technolojia au hela ya kuvuna hizo maliasili sisi wenyewe na hata sasa wavunaji wakuu ni wageni.​
Magufuli:
Tanzania lazima ipate pato kubwa kwenye madini​
Sisi ni donor country hatuhitaji mabeberu.​
Membe:
Atawarudisha wawekezanji​
Atahakikisha miradi mkubwa ya LNG unakamilishwa​

Mwisho ningependa kusisitiza kuwa haya ni yale niliyoyasikia kama kuna mengine nikiyasikia mbeleni nitaendelea kuyaandika hapa.
Pia Moderators kama mnataka kuratibu hii mada kwa kuendelea kuweka orodha ya mambo wanasiasa wanatu ahidi mnakaribishwa. Kelele zitakuwanyingi kwenye siasa mwaka huu tunahitaji mahali ambapo tunaweza kuelewa nini wanajaribu kusema.

Heshima za dhati kwa wagombea wengine ambao sijawaorodhesha hapa. Hoja zenu sijazisikia na sina uhakika kama mna nia ya kweli ya kuliongoza taifa au mmefuata rudhuku.
 
Back
Top Bottom