Tulio hamia nyumba zikiwa hazijaisha tupeane uzoefu na changamoto

Tulio hamia nyumba zikiwa hazijaisha tupeane uzoefu na changamoto

Alejandroz

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2017
Posts
329
Reaction score
413
Siku njema wana JF

Kuna wakati unafika unaona kuendelea kulipa kodi kwa mama mjengo sio chaguo sahihi,, hivyo unachagua kuingia kwenye nyumba yako ikiwa bado haijakamilika.

Je, uliingia kwenye nyumba yako ikiwa katika hatua gani, kama ilikua bado haijaisha ni nini kilikusukuma na nichangamoto zipi ulizipitia?

Karibuni [emoji846]
 
Mungu ni mwema nilihamia almost nimemaliza kwa asilimia 90. Nilikuwa nimebakiza tiles vyumba viwili, stoo, varanda mbili ya jikoni na mbele ya nyumba na msingi wote. Vile vile tiles za ukutani za jikoni. Choo cha selfu ya room moja pia nilikuwa sijakamilisha
 
Nilikua najenga ghorofa nimemaliza slab hela ikakata na kazi nikafukuzwa ikabidi nihamie hivo hivo.
Changamoto mvua ilikua ikinyesha maji yanaingia ndani, mwezi wa sita mpaka wa nane nakoma kwa upepo na baridi kali.watoto mafua hayaishi mana linapenya hasa. Mungu si athumani nilikaa kwa jinsi hiyo miaka 2 badae mambo yakanyooka kamjengo kanaendelea
 
Wanasema nyumba aiishagi ,hata Manji/SSB bado wanafanya marekebisho /renovation kila baada ya muda! Nyumba ukishapaua ,ukaweka rough floor ,grill ,nyavu dirishani,choo basi ipo completed mambo mengine ni show-off/mbwembwe tu.
 
Siku njema wana JF

Kuna wakati unafika unaona kuendelea kulipa kodi kwa mama mjengo sio chaguo sahihi,, hivyo unachagua kuingia kwenye nyumba yako ikiwa bado haijakamilika.

Je, uliingia kwenye nyumba yako ikiwa katika hatua gani, kama ilikua bado haijaisha ni nini kilikusukuma na nichangamoto zipi ulizipitia?

Karibuni [emoji846]
Yaani Ina Raha 30% na karaha70%
 
Sisimizi,jongoo,nge, mende, siafu ,mbu, mijusi ya ajaba,wakati mwingine wanyama wanapotea njia wanaingia ndani na kuanza kupiga kelele kutafuta pa kutokea.
Kama juzi kaingia bundi asee alisumbua wee acha ila manati yalinisaidia sana japo nilitoboa bati[emoji30][emoji30]
 
hahah pole mkuu
 
Nilianza ujenzi 26/10. Mvua zinaanza mwezi wa 11 huku kwetu Nyanda za juu kusini. Nikaanza kwa kuchimba shimo la choo na kulijengea hadi juu. Mafundi wakaanza kimbiza kuta na siku 21 wakawa wamemaliza kufunga hadi Renta na course za juu. Toka hapo nikapandisha Kenchi japo jamaa wa kupaua alikuwa ananifanyia figisu.

Mwisho wa mwezi wa kwanza ngoma imeisha kwa kuweka mlango wa mbele na nyuma tu. Kwenye madirisha nikagonga Nylon, milango ya ndani ni mapazia. Tarehe 31 mwezi wa 1 nipo kwangu japo sikuwa nimemaliza kofia kwani fundi alikuwa na kazi nyingi na mafundi wa kupaua nilibadilisha 3. Fundi aliniset kuwa bila kofia hata mvua zikinyesha maji hayaingii ndani. Hahahaaaa, nilipigwa na mvua huku nina watoto wadogo. Usiku ni kuhamisha tu magodoro. Jumatatu nikatafuta fundi mwingine na akanipigia kofia.

Huku kwetu kuna Baridi na upepo. Upepo ukawa unang'oa nylon za madirishani. Mvua kali na upepo ukawa unaingia ndani. Mungu saidia nilifanikiwa maliza sasa mambo safi
 
japo bado sijahamia lakin changamoto ni kwamba mjumbe wa mtaa ni mwanga/sangoma kuna siku nmekatisha kwake nakuta kikundi cha watu wanacheza ngoma huku wamevalia mavazi rangi nyejundu, nyeus na nyeupe..,nilichukia sana
 
mh yakweli haya?[emoji848]
 
Ya kwangu imenigomea kwenye rinta kila nikifosi nachemka, ingekuwa sio watoto wangu wadogo nilionao ningelaza bati mengine ningejua mbele ya safari. Hiki kipindi sijawahi kukutana nacho kwenye maisha yangu
Pole mkuu,,
Hapo bado kwenye kufulia tena kwa kiwango cha sgr,, maana ujenzi unakomba kila shilingi iliyopo mfukoni [emoji846]
 
Back
Top Bottom