Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Dejane

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
50,587
Reaction score
71,492
Mim bibi yangu upande wa baba ana vituko huyo,anaongea kuanzia asubuhi mpaka tunaenda kulala
Bibi yangu hua anaamka saa 12 asubuhi ole wako uchelewe kuamka ataanza kusema sijui mtaolewa na kina nani mpo wavivu vivu tu
Akija mtu anauza mboga au chochote bibi atataka apunguziwe na kuanza kusema mbona hata sio kizuri chukua hela wewe unakataa pesa(cha kwake sasa bibi yangu weee umwambie apunguze bei mkali kama nini)
Alilazwa hospital hua ana kisukari hiyo hospital ilikua mpya so kukawa na wagonjwa baadhi ,jumla wakawa wanne akiwemo na bibi yangu,ikifika asubuhi anaanza kuwaamsha kua wafanye usafi wafue nguo zao,mara wakaoge yaan utafikiri ye nurse wa zamu
Akiwa hayupo kwake anaona kila kitu hakiendi anaona kama anaibiwa vitu so muda mwingi yupo nyumbani na anataka kila kitu kikae sehemu yake
Hata itokee safari hataki kuondoka kwake anaona wafanyakazi wataiba

Anapenda watoto wa kiume hakuna mfano wa kike kwake hawana maana kabisa

Akiwa hataki mtu aende kwake na akaenda ukimsalimia tu au kumuuliza chochote anakua mkali na kuanza kulalamika kua huyu kijana hana adabu anaweza niuliza maswali ya hivi mim mzee,,yule mtu akiondoka ,watakuja baba zangu wadogo anaanza kuwapa mashitaka sasa akiona hawamjali,akija mtoto wake mwingine anamuhadithia na kuongeza chumvi ili yule kijana apigwe basi wakiona vile wanajifanya kukasirika na kusema wanaenda kumtafuta yule kijana wamfundishe adabu,basi bibi akisikia hivyo roho kwatuu,

Bibi yangu anaweza sema hivi baadae kikiharibika kitu anawakana wote kua mmesingizia,,

Hapatani na mmewe kila mtu analala chumba chake,,wakianza kurushiana maneno na babu kila mtu ni mbaya,,ataanza kumwambia na ufe tu sijui unasubiri nin mzee mbaya wewe huna maana,,bibi anapenda watoto wake na wajukuu zake kuliko mmewe

Kuna kipindi nilienda kuwasalimia nikawa namtengea babu chakula ,,kabibi kanamuambia babu subiri dinazarde aondoke uone nani atakupa chakula utakula jeuri yako

Bibi yangu watoto wa kiume hata wafanye nin haoni ubaya,nyie wa kike sasa ataongea siku nzima

Akianza kusimulia kua ye alikua mzuri utasema sijui alikuwaje haha

Kila mda anataka mle ye hali ila nyie mle tu chakula ndio furaha yake

Akianza kuchamba siku hiyo tutacheka tu maana siku hizi kabakiza mdomo tu ,maana anakua kakaa kwenye kiti hawezi kutembea haraka kama zamani wala kupiga

Hali kwa watu akiamini sio wasafi kama yeye,akitembelea sehemu atakunywa soda tu chakula hagusi

Bibi yangu ana mdomo huyu ,babu yangu humuambia kwisha habari yako naenda kuoa msichana mdogo,,nae anamuambia nenda umechelewa tukutolee mabegi

Siku moja nilikuta wanagombania kahawa,bibi kamnyima babi kahawa,alitaka kuweka kwenye maziwa
Anamuambia kanunue pesa zako unapeleka wapi

Basi inabidi kesho babu akanunue ile kahawa kubwa

Babu yangu sasa,ana ng'ombe wengi anawapenda kuliko sisi wajukuu ,,ukimuomba hata mmoja anakuambia ng'ombe wangu wagonjwa wamevunjika miguu
Ameanza kusahau pesa hua tunamchenjia buku buku,,akitembea na laki anaweza nunua sweta la 10000 akauziwa 80000,siku hiyi ikabidi wamuambie wee aksema pesa zangu zinawahusu nin nyie,mbona nyie mkinunua kitu siwaulizi,nikinunua mim tu mnatoa macho,,
Bibi yangu sasa utafikiri 80000 zake aliongea na kusema yule kijana afungwe sijui nin,babu anamkatisha nyamaza we mwanamke mzee

Babu yangu siku moja ananipa pesa ile anatoa akadondosha kondom moja nilicheka mpaka nikaanguka chini

Akiona mkewe kalazwa hayupo siku nyingi nyumbani anasema mleteni mke wangu,akifika siku hiyo tu wanakosana hahaha

Hua nacheka mno mie ,bibi yangu anaweza badili maneno mpaka ukashangaa na kusema juu eti dina mim nilisema hivyo inabidi umfurahishe kua hakusema wakati alisema na sisi tulikuwepo

Babu yangu akiugua mkipeleka ile ile hospital siku nyingine anakataa,,kua hiyo hospital imemchosha nipelekeni Dar nipande ndege,,,inabidi wampeleke tu

Anaweza ondoka bila kuaga akapanda gari akaenda Arusha anaenda kumtafuta mtoto wa ndugu yake ni daktari na kumuambia naumwa sana,akipimwa hakuna kitu
Huku watamtafuta balaa,mpaka simu ipigwe ndio wanamfata

Babu anatupenda wajukuu wa kike kuliko wa kiume,,sie wakike ndii hutupa pesa wa kiume anaawaambia nendeni kwa bibi yenu huko

Hebu elezeeni visanga vua huko kwenu
 
Sisi bibi yetu(RIP) tulikua tukienda kumsalimia kijijini au akija home kitapigwa kigeregere moja matata sana, takrbani karibu dk 40 anapiga shwangwe yaani hadi baadhi ya shughuli za mtaani zinasimama kwa muda. Sijawahi ona kigeregere kama kile tena katika Maisha yangu.
 
Nyani Ngabu mtoto wa kishua atawezana nao hao kweli?

Bibi alikuja O'Bay kutoka MZA,kwa matibabu.

Alikuwa hajazoea kukaa mbali na kwake. Basi akikumbuka kwake, anaanza kuomba tumrudishe.

Mkimzuga atarudi, akistukia mnampa sound, mnamuona huyo anaanza kuondoka, anafungua geti, eti anaanza kutembea anataka kutembea kutoka O'Bay mpaka Mwanza.

R.I.P Bibi.
 
Bibi yangu kwa watoto wa kiume halaf asikie umesoma weee au una pesa anakuona shababi haswa,,Hahaha sijui makwao hua kuna nini hawa watu
Tena kwa wageni mkarimu vibaya simfikii
 
Bibi yangu kwa watoto wa kiume halaf asikie umesoma weee au una pesa anakuona shababi haswa,,Hahaha sijui makwao hua kuna nini hawa watu
Tena kwa wageni mkarimu vibaya simfikii
Huyo kama Bibi yetu mmoja tulikuwa tunasema anapenda watu wenye mafuta.

Bibi alikuwa hageuzi kwangu, mimi namuona mtu poa sana. Lakini wengine wanamuona bonge la mnoko na mlalamishi.

Kila mbuyu na shetani wake, wahenga walisema.
 
Bibi yangu ana fix hatari nikikaa-ga naye haishiwi story. Eti kuna siku alilazwa hosp mimi nilikuwa mdogo sikumbuki ila huwa ananiambia tulikuwa wote namuuguza.

Sasa siku akazidiwa akakata kuja kustuka akajikuta anatembea kwenye kakamba kadogo kembamba anaelekea juu mawinguni. Akawakuta watu watatu huko mbinguni mmoja boss wengine nyokaa wake.

Bibi hakusemeshwa, akasikia wanaambiana vipi moyo wake bado upo? Hahaha mmoja akajibu sijui..boss akamkaripia nenda kaangalie. Jamaa akaenda akarudi akamwambia upo.

Boss akaamuru basi mshushe. Bibi akashushwa bwana. Kwa speculations zake anakuambia eti juu kuna moyo wa kila mtu umetundikwa kama drip so ukipotea kule na huku duniani umepotea.. na ndiyo maana hao jamaa waliangalia wake.

Ukimbishia ukamwambia bibi labda ulikuwa unaota hahaha anakununia week nzima. Bibi nimemisa story zake inakadiriwa anafikisha 115+ sasa.
 
Kupitia bibi nimejifunza mambo mengi hasa dini... Hajui kusoma wala kanisani hajawahi kwenda amestick kwenye dini ya tamaduni yake mmewe alikuwa kiongozi huko.

Sasa story za kwenye hiyo dini na viongozi[mitume] zinafanania na maudhui na hizi za wakristo na muslim. Kuna mmoja ni kama yesu alikuwa anaponya watu hivyo hivyo akatokomea kusiko julikana na hadi leo amebaki maskioni mwa watu labda atarudi tena kuponya watu.

kuna misemo kibao ipo kwenye bible huwa inafanana vilevile na anayoniambia... na huyu bibi kusema alifundishwa bible hakuna.[tusipuuze tamaduni zet].
 
Huyo kama Bibi yetu mmoja tulikuwa tunasema anapenda watu wenye mafuta.

Bibi alikuwa hageuzi kwangu, mimi namuona mtu poa sana. Lakini wengine wanamuona bonge la mnoko na mlalamishi.

Kila mbuyu na shetani wake, wahenga walisema.
Mim bibi nampenda lakin anaongea mno,,hata akiumwa ye anaongea tu
 
Ahahaha hata bibi yangu anachokuambia umsikilize usimbishie
 
Bibi yangu yeye namkumbuka kwa mengi especially hadithi zake zamani huko mambo ya Mwaka wa njaa,, ati mama ake(mama ake bibi) alikuwa anabandika jiwe kwenye chungu na maji mpaka juu anawaambia wachochee wasifunue kabisa bhasiii wanachochea mpaka yao anakuja wanachochea Wee mpaka wanasinzia wanamuacha anachochea, kustuka Kumekucha!! Walikuja jua hii kitu wamekuwa wakubwa lol
Pili bibi yangu anapenda ela uyoo (asili yake inachangia nadhani) Yaani Kama wewe ni mjukuu wazazi wako njema jua utapendwa hatarii na watoto wake pia kuna anao wapenda kuliko wengine
Anapenda wajukuu wenye majina yake pia,, also alinichapa mpaka nikaacha kukojoa kitandani Jamani aliniambia ataniletea Kobe nimkalie mbona niliacha kukojoa mweeh
Nakumiss bibi see you kwenye holiday
 
Alikua na maana gani kuchemsha jiwe kwenye chungu?
 
hahahaha Dina bibi yako amenichekesha sana vituko vyake....aiseee hakuna bibi asiye na vituko ngoja leo nisome kwanza nami nitashare siku nyingine....
Asante nimecheka sana tena sana ila mabibi wote wana mapenzi sana na watoto hasa wajulkuu...
 
Dinazarde nimecheka had machozi jaman !dah eti ukiomba ng'ombe anasema miguu imevunjika !jamani nimecheka !i can imagine kwa bibi yako !Mungu ampe maisha marefu jaman muendelee kuenjoy !
mie sijaishi karibu na bibi zangu walikua hawajui kiswahili na mie sijui kisukuma bas nikawa napishana nao tu round about !rip bibi zangu
 
Yaan acha we ukiishi na bibi yangu wiki utajichekea mno
 
Babu yangu ana vituko nadhani hakuna,, haha

Alisema anakuja dar,, mjomba wangu akaenda kumfuata ubungo akamleta kwetu( yani kwa mamangu) ili akae siku tatu then atamfuata aende na kwake( mjomba angu ana mke ila hana watoto so kule hamna wajukuu),, basi akaja nyumbani siku ya tatu mjomba akaja kumfuata kuwa twende na kwangu baba,,,akamjibu,WAKATI NATOKA KIJIJINI NILIKUA NA LIST YA MAJINA KWENYE KARATASI YA WALE NITAKAO WATEMBELEA ,NA KILA NINAYEMUONA NAMTIKI,,SASA WEWE NISHAKUTIKI NILIVOKUONA TU UBUNGO SO SIJI.
Afu mkavuu na kamaliza .

Siku moja tukamwambie twende mjini tukuoneshe maeneo ,,akasema mi sijaja kuona maeneo nimekuja kuona watu,,yani anakatisha tamaa vibaya,, ila ukikaa naye ni kucheka muda wote
 
Bibi yangu mzaa baba alikuwa hataki tukacheze kwa majirani kila cku anashtaki kwa mama watoto wako wanazurura mno kila cku kesi hiyohiyo cku moja mama akaamua kutupiga haswa sasa alikuwa hataki kaka yetu apigwe maana anamwita mume na mama akawa anamtembezea fimbo zaidi kaka maana yeye ndo kiongoz wa kuzurura bibi kaamulia weee alivoshindwa akakusanya nguo ucku anarudi kwake. Ikabid mama aanze kumbembeleza. Kingine akipewa kitu chochote cha kula anaficha ili baadaye awagawie mkiwa mnakula mama inabidi atuangalie maana bibi maziwa aliyowekewa atawaongezea mpaka yaishe. RIP bibi
 
Hhhaaaaaa
 
Nimependa hapo pa kukalia kobe ili usikojoe kitandani[emoji2] [emoji2]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…