Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Nimecheka sana [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119]
 
Dah bibi angu alikua ana duka lake ambapo akikutuma chochote uende pale pale Na si kwngine yaan upite maduka karib matatu Ndo uende duka alitakalo...bas siku moja kanituma soda nikanunua kwny duka la kwanza looh nlijuta kumbe alikua ananichungulia kwa dirishan Bas ile nampa tu chupa ikatupwa chin pwaaaa "nimekwambia kanunue kule we umeenda apo doda zao wanapunja Sukar we mshenz sana "ha ha ha bibi alikua mtata sana ata mchele akigundua tu umenunua sehem asiyotaka utamwagwa ata uwe kilo kumi ha haja

Rest in peace bibi
 
Muda si mrefu naachana na JF imekuwa ya watoto
 
Hahahahah uwiii alikua jeuri,,eti wanapunja sukari
 
anaweka tu chumbani kwake ata kule kijijn ana makopo rum kwake ukiyatupa baada ya cku mbili unakuta tena@dinazarde
Umenikumbusha kuna mama mmoja anapenda makopo huyo sijui akizeeka itakuwaje
 
Hahahahah uwiii alikua jeuri,,eti wanapunja sukari
Ha ha ha alikua ni shida na Ni jeur kwel kina baba walimdekeza sana alikua hawez kutembea bas anajikongoja anakaa nje kibarazan kwake bas kila anaepita ata muuliza kile Mara iki mpaka jion ana Habari zoteeeee Za mji ha aha ha ha
 
Ha ha ha alikua ni shida na Ni jeur kwel kina baba walimdekeza sana alikua hawez kutembea bas anajikongoja anakaa nje kibarazan kwake bas kila anaepita ata muuliza kile Mara iki mpaka jion ana Habari zoteeeee Za mji ha aha ha ha
Hahahaha
Tuna kazi sijui na sie tutakuwa hivyo
 
Umenikumbusha my bibi Dina, ngoja nifanye nikamuone aise after Xmas
 
Mi babu yangu alikua mlevi sana....... Sasa akitoka kupiga pombe bahati mbaya hajakuta mtu........ Anachukua manati yake na mawe yakutosha aliokua anahifadhi ndani kwa ajili ya kuwindia ndege.... ...then anakaa mlangon.
Sasa hapo kila anaekuja kutoka misele anakula Stone zakutosha...kama kukwepa ndo utaisoma namba

Kuna Siku tulilala Kwenye shamba la chai mpka asubuhi mana mawe yalikua hayaishi...... Na anashabaa kinoma
 
Nimeishi na bibi kuanzia la kwanza hadi form 1.
Pamoja na utundu wangu, bibi ananipenda mpk kesho.

Bibi anawajukuu 15, lkn katika wote ole wake asikie kuna mtu ananisema vibaya, hata baba au mama.

Yani Gusa watu wote ila sio, mimi.

Bado yupo, na huwa nampigia sim mara kwa mara. Akisikia sauti yangu anafarijika sana.

Uzuri namjali vipesa vya pombe na nyamaa.

I love you Grandma
 
Hahahahahaha
 
Vizuri
 
Bibi yangu mkubwa yeye alikuwa anapeenda Sana shikamoo ,ukitaka ugomvi nae usimuamkie ,ila sasa yeye alikuwa anapokea hata shikamoo za wiki au mwezi unaweza ukamuamkia shikamoo 21 zote na akikuuliza una mwambie tu nilishakuamkia za wiki tutaonana jumapili
 
Nilkuwa na umri kama wa miaka 12...nilienda kumsalimu bibi mzaa baba Tukuyu siku ya kwanza nilipikiwa wali maharage...siku ya pili alipika samaki Ile jua linaanza kuzama akaniambia nitwange mihogo (majhabhu) kwa aajili ya ugali wangu usiku maana ye atakula ndizi choma (matoki)....bwana weee si nikaenda kucheza nikarudi usiku kama saa 2 hv...ile nafika tu nakuta ameshachoma ndizi ,,akapakua samaki bakuli mbili , yake akaweka ndizi zake alafu yangu akanipa bila chochote , Si nikamuuliza ugali uko wapi akajibu kwa kilugha "kyo ikhi gwhakanagha pakutika itasi""(ndo ule ambao ulikataa kutwanga mda ule)...nilikula samaki peke ake nikaenda Kulala ....nilijifunza kitu....R.I.P mke wangu (bibi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…