A
Anonymous
Guest
Katika mchakato wa kuomba mkopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), tumekutana na changamoto inayohitaji ufafanuzi.
Inaonekana kuwa pale HESLB inapokurejeshea ombi lako ili ufanye marekebisho kwenye baadhi ya nyaraka, ombi hilo huchelewa kufanyiwa kazi tena hata baada ya kuwasilisha marekebisho yaliyohitajika.
Mimi ni mmoja wa waathirika wa hali hii. HESLB ilinirudishia ombi langu kwa ajili ya marekebisho madogo, ambayo niliyafanya na kuwasilisha upya siku hiyohiyo. Hata hivyo, kwa muda mrefu sasa, ombi langu limeendelea kuwa na hali ya "Corrections Submitted" bila kufanyiwa kazi, huku awamu mbalimbali za majina ya wanufaika wa mikopo zikiendelea kutangazwa.
Hali hii inazua maswali mengi kuhusu hatima ya waombaji walio katika mazingira kama yangu. Je, kurejeshewa ombi kwa ajili ya marekebisho na kisha kukaa muda mrefu bila kufanyiwa tathmini upya kunamaanisha kuwa tayari tumepoteza nafasi ya kupata mkopo? Au kuna utaratibu gani unaotumika kushughulikia maombi yaliyofanyiwa marekebisho?
HESLB inapaswa kutoa ufafanuzi kuhusu suala hili ili waombaji wapate kujua hatima ya maombi yao, hasa ikizingatiwa kuwa awamu za utoaji wa mikopo zinaendelea kutangazwa na muda unasonga.