Tulioamua kutokuoa tupeane mikakati ya uzeeni!

Tulioamua kutokuoa tupeane mikakati ya uzeeni!

Umeongea point ila pia ukiwa na hela usiishi peke yako kama mchawi,weka house girl hata wawili,chukua mtoto hata kama dio ndugu ishi nae
pote tunaelewana lakin kwenye ukipatwa na hali ya kuhudumiwa maungoni bado sijaona mbadala wa mke kwenye orodha yako!
house girl?!!!!
mtoto wa ndugu?!!!
Hitimisho ni kwamba mke ni kama hakwepeki kwa baadhi ya majukum nyeti!
Nikisema mke namaanisha mke kipenzi na rafiki na si kiumbe wa kike unayeweza kuishi naye ukimwita mke!
Hao ndo wameibua Timu Kataa ndoa.
Hawakawii kukusukumiza kwenye diaba ili wawe wajane warithi!
 
Ni kawaida watu kuwa na mitazamo tofauti namna ya kuishi.
Haijalishi umechukua mwerekeo upi bado kuna changamoto zitakuwepo na hata zinatofautiana uzito.
Kuna msemo between two evils choose lesser evil
Sasa ukweli mchungu ni kuwa .. kutokuoa ni kuchagua shetan hatari zaid!
Utafiti unaonyesha asiyeoa hufa miaka 5 kabla ya aliyeoa!
Na aliyeoa mke mmoja hufa mapema kuliko wa wengi!(sababu siijui na siko tayari kubishana na utafiti bila utafiti)
Sasa inapofikia huwezi kuoa, adui mkubwa ni HOFU ya kutokuwa na msaidizi! (endapo tafsiri, maana na hali ya ndoa itakuwa imebaki ile ile, siyo zile ndoa vita!)
Kwa sasa hoja sio kwanini kuoa au kutokuoa bali ni mashauriano ya endapo hukuoa ni mambo gani ujipange usingoje kuzeeka, wakati ambao ni muafaka kuwa na mwenza wa mnayeanguka na kuinuka pamoja!
Tunajua fika mara nyingi mme ndo huchakaa mapema hadi kuhitaji wa kumbadirisha pampers akipupu kama dogo!
Binafs nina haya kama maandalizi ya msingi.
1. Bima kubwa (km Aghakhan wanaohudumia kuliko 5 star hotel hadi unataman kuumwa tena! sio vifurush vya kutupiwa panadol!)
2. hisa katika kampuni kubwa zisizoyumba ( sio kama za walionunua kampun flan ya simu)
3. real estate investiments kama frames za kukodisha, nyumba/vyumba kupanga. pesa ikufate kwako bila usimamizi wa kila siku.
Pia misitu ya miti.
4. Serikali na wadau wawekeze nchini Bima ya kulea wazee katika nyumba maalum yenye hadhi na huduma kama huko nje (hapa simaanishi vituo vya sasa vya wazee mafukara unatunzwa ili ufe). namaanisha unaishi chini ya uangalizi mkubwa na mzuri kwa pesa zako ulizochangia na unajaliwa.
5. Pia wadau wawaishe AI ya kuunganisha ubongo na huduma mzee atakayo bila kuhitaji binadam.
Hofu yangu ni usipokuwa katika hali ya kifamilia unaweza kukutwa umekauka ndani!
Binadam wanazid kuwa wabinafs na busy, ikiwemo wanao!
.... ukisoma mwanzo hadi mwisho utagundua ,,,heri kuoa!
Kidole kimoja hakivunji chawa..
 
Reasoning ya ajabu sana hii! Unaoa mwanamke ili aje akuoshe ukiwa umeharisha! Basi hakuna haja ya kuoa maana mwanamke aweza kukutoroka ukianza kuharisha
mke ana faida na majukum mengi chanya dhidi ya mmewe kama ilivyo mme kwa mkewe.
lakin mengi yana mbadala au plan b, c ,d...
kwangu ukifikia hatua ya kuangaliwa kiafya naamini mke ahitajiwa zaidi.
inawezekana namna yako ya kutafsiri mambo haitafsiriki!
 
Mungu aliposema atampa adamu msaidizi hakukoseaa...for sure fainali uzeeni na nyakati za magonjwaa..Na mkiumwaga mlivyoo walegevuu..
 
Mikakati Yangu:
  1. Kwa sababu maisha yangu ya uzeeni bado napenda niendelee kula bata, kwa sasa kila mwezi nahakikisha nahifadhi kiasi kisichopungua laki 6 -8 kwenye masoko ya fedha.
  2. Nikifanikiwa kufikisha miaka 40 nanunua mbuzi kati ya 20 - 30 na ng'ombe 4 - 6, kisha nawaandalia mazingira kwenye eneo langu (Shamba) huko arusha kisha natafuta kijana wa kimasai namjengea room 1 na kumkabidhi mifugo aichunge.
  3. Nikifanikiwa kufikisha miaka 50, Naenda kwenye shamba langu najenga nyumba ya kawaida tu yenye vyumba vikubwa vitatu, na sehemu ya jiko kubwa (napenda kupika). Hii ni maandalizi ya kujiandaa kustaafu.
  4. Nikifanikiwa kufikisha 55 - 60 narudi rasmi kwenye nyumba yangu na kuanza kujishughulisha na ufugaji tu wa kuku wa kienyeji kama 100 hivi, hawa sitowafuga kwaajili ya biashara, ni kwaajili ya kula tu na ku ni keep busy.
  5. Kwakuwa napenda party life, kila mwezi naweza nikawa na host house party kwenye nyumba yangu, ni kula na kufurahia tu na wazee wenzangu.
mungu aendelee kunijalia afya njema, mafanikio na umri mrefu ili niendelee kuishi maisha haya.
 
Je vile vichanga vinavyo kufa kabla au baada ya kuzaliwa sababu ni huwa hiyohiyo??
 
Mjadala huu unaonyesha jinsi wanaume waliojichanganya kuoa wanavyoishi kwa stress na mawazo yao ni kuugua tu watakapokua wazee, kwanini mnawaza kwamba mtaugua na mtahitaji kuhudumiwa???nani kasema ukiugua wa kukuhudumia lazima awe mwanamke/mke??acheni mawazo ya kiwaki hayo
Jambo la msingi ni kutafuta hela na kujiwekeza sana ingali bado una nguvu PESA HAINUNUI UHAI TU ILA INAWEZA KUFANYA VINGINE VYOTE
Ndoa ni utapeli
KATAA NDOA
TUNZA FURAHA YAKO.
 
Sikubaliani na timu kataa ndoa kwani mimi nina mke. Lakini hoja ya kusema unaoa ili ukipata na maradhi hasa ya uzeeni mkeo akusitiri sikubaliani nayo kwa asilimia 100.

Vifo vingi vya wazee wetu vinatokana na msongo wa mawazo baada ya kutengwa na mke na watoto. Kumbuka kadri umri unavyozidi kusonga ndivyo ambavyo mke anazidi kuwaweka watoto karibu na yeye na kuwaeleza bad sides tu kuhusu wewe.

Hivyo basi, kama mwanaume ni vyema kujiandaa na maisha ya uzeeni ukiwa bado una nguvu bila kujali una mke au lah! Hii ni pamoja na kujiandaa kusaikolojia endapo familia itakutenga, kujiandaa kuwa na uwezo wa kuingiza kipato cha kila siku hata kama utakuwa umelala kitandani.

Maandalizi mengine ni pamoja na kuishi vizuri na watu wakiwamo majirani pamoja na kuwajali ndugu. Katika watu 100 uliowafanyia wema, huwezi kukosa walau mmoja atakayerudisha fadhila.
 
Kataa ndoa iv inatofautiana vipi na rainbow 🙄
 
Back
Top Bottom