Tulioamua kutokuoa tupeane mikakati ya uzeeni!

Umeongea point ila pia ukiwa na hela usiishi peke yako kama mchawi,weka house girl hata wawili,chukua mtoto hata kama dio ndugu ishi nae
pote tunaelewana lakin kwenye ukipatwa na hali ya kuhudumiwa maungoni bado sijaona mbadala wa mke kwenye orodha yako!
house girl?!!!!
mtoto wa ndugu?!!!
Hitimisho ni kwamba mke ni kama hakwepeki kwa baadhi ya majukum nyeti!
Nikisema mke namaanisha mke kipenzi na rafiki na si kiumbe wa kike unayeweza kuishi naye ukimwita mke!
Hao ndo wameibua Timu Kataa ndoa.
Hawakawii kukusukumiza kwenye diaba ili wawe wajane warithi!
 
Kidole kimoja hakivunji chawa..
 
Reasoning ya ajabu sana hii! Unaoa mwanamke ili aje akuoshe ukiwa umeharisha! Basi hakuna haja ya kuoa maana mwanamke aweza kukutoroka ukianza kuharisha
mke ana faida na majukum mengi chanya dhidi ya mmewe kama ilivyo mme kwa mkewe.
lakin mengi yana mbadala au plan b, c ,d...
kwangu ukifikia hatua ya kuangaliwa kiafya naamini mke ahitajiwa zaidi.
inawezekana namna yako ya kutafsiri mambo haitafsiriki!
 
Mungu aliposema atampa adamu msaidizi hakukoseaa...for sure fainali uzeeni na nyakati za magonjwaa..Na mkiumwaga mlivyoo walegevuu..
 
Mikakati Yangu:
  1. Kwa sababu maisha yangu ya uzeeni bado napenda niendelee kula bata, kwa sasa kila mwezi nahakikisha nahifadhi kiasi kisichopungua laki 6 -8 kwenye masoko ya fedha.
  2. Nikifanikiwa kufikisha miaka 40 nanunua mbuzi kati ya 20 - 30 na ng'ombe 4 - 6, kisha nawaandalia mazingira kwenye eneo langu (Shamba) huko arusha kisha natafuta kijana wa kimasai namjengea room 1 na kumkabidhi mifugo aichunge.
  3. Nikifanikiwa kufikisha miaka 50, Naenda kwenye shamba langu najenga nyumba ya kawaida tu yenye vyumba vikubwa vitatu, na sehemu ya jiko kubwa (napenda kupika). Hii ni maandalizi ya kujiandaa kustaafu.
  4. Nikifanikiwa kufikisha 55 - 60 narudi rasmi kwenye nyumba yangu na kuanza kujishughulisha na ufugaji tu wa kuku wa kienyeji kama 100 hivi, hawa sitowafuga kwaajili ya biashara, ni kwaajili ya kula tu na ku ni keep busy.
  5. Kwakuwa napenda party life, kila mwezi naweza nikawa na host house party kwenye nyumba yangu, ni kula na kufurahia tu na wazee wenzangu.
mungu aendelee kunijalia afya njema, mafanikio na umri mrefu ili niendelee kuishi maisha haya.
 
Je vile vichanga vinavyo kufa kabla au baada ya kuzaliwa sababu ni huwa hiyohiyo??
 
Mjadala huu unaonyesha jinsi wanaume waliojichanganya kuoa wanavyoishi kwa stress na mawazo yao ni kuugua tu watakapokua wazee, kwanini mnawaza kwamba mtaugua na mtahitaji kuhudumiwa???nani kasema ukiugua wa kukuhudumia lazima awe mwanamke/mke??acheni mawazo ya kiwaki hayo
Jambo la msingi ni kutafuta hela na kujiwekeza sana ingali bado una nguvu PESA HAINUNUI UHAI TU ILA INAWEZA KUFANYA VINGINE VYOTE
Ndoa ni utapeli
KATAA NDOA
TUNZA FURAHA YAKO.
 
Sikubaliani na timu kataa ndoa kwani mimi nina mke. Lakini hoja ya kusema unaoa ili ukipata na maradhi hasa ya uzeeni mkeo akusitiri sikubaliani nayo kwa asilimia 100.

Vifo vingi vya wazee wetu vinatokana na msongo wa mawazo baada ya kutengwa na mke na watoto. Kumbuka kadri umri unavyozidi kusonga ndivyo ambavyo mke anazidi kuwaweka watoto karibu na yeye na kuwaeleza bad sides tu kuhusu wewe.

Hivyo basi, kama mwanaume ni vyema kujiandaa na maisha ya uzeeni ukiwa bado una nguvu bila kujali una mke au lah! Hii ni pamoja na kujiandaa kusaikolojia endapo familia itakutenga, kujiandaa kuwa na uwezo wa kuingiza kipato cha kila siku hata kama utakuwa umelala kitandani.

Maandalizi mengine ni pamoja na kuishi vizuri na watu wakiwamo majirani pamoja na kuwajali ndugu. Katika watu 100 uliowafanyia wema, huwezi kukosa walau mmoja atakayerudisha fadhila.
 
Kataa ndoa iv inatofautiana vipi na rainbow 🙄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…