Nkerebhuke
JF-Expert Member
- Nov 1, 2021
- 796
- 2,026
Maisha ni safari ndefu sana maana tulipotoka sipo tulipo sasa maana maisha yamebadilika sana. Huko nyuma kipindi kama hichi cha sikikuu watu walicheza disco na kukata ngoma haswaa, wale wa kijijini walicheza mpaka nyasi ziling'oka. Walikuwepo making wa dancing floor yaani akianza kukata wote mtasimama kuangalia vituko na staili alizocheza.
Wale wa mjini tulikata ngoma mpaka jasho linatililika kama maji, miguu kuishiwa nguvu nusu pumzi kukata. Kama ni madem tulibambia kwelikweli kama kupe, staili tulizijua akishuka unashuka nae na akipanda unaishi nae hewani. Maisha yamebadilika vijana wa Leo wana stress hawajui kukata ngoma wala kubambia, wamejaa aibu na woga