Tuliocheza disco dhamani mpaka miguu inatetemeka tukutane hapa

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
796
Reaction score
2,026
Maisha ni safari ndefu sana maana tulipotoka sipo tulipo sasa maana maisha yamebadilika sana. Huko nyuma kipindi kama hichi cha sikikuu watu walicheza disco na kukata ngoma haswaa, wale wa kijijini walicheza mpaka nyasi ziling'oka. Walikuwepo making wa dancing floor yaani akianza kukata wote mtasimama kuangalia vituko na staili alizocheza.

Wale wa mjini tulikata ngoma mpaka jasho linatililika kama maji, miguu kuishiwa nguvu nusu pumzi kukata. Kama ni madem tulibambia kwelikweli kama kupe, staili tulizijua akishuka unashuka nae na akipanda unaishi nae hewani. Maisha yamebadilika vijana wa Leo wana stress hawajui kukata ngoma wala kubambia, wamejaa aibu na woga
 
We super ngedere.
 
Kwahiyo wewe mcheza disco umeshindwa kutofautisha dhamani na zamani.
 
Dhamani ndiyo kitu gani? Hivi we binafsi unajionaje kuandika huu upupu?
 
sio dhamani ni zamani
 
Siku hizi disiko watu wanaenda kulewa pombe na si kusikiliza mziki na kucheza.

Zama zimebadirika wajameni
 
Wuueh unazungumzia majoka? Huku town kipindi hicho kuna madensa kama kina dudu na wengine walikuwa wanacheza majoka utafikiri mwili hauna mifupa. Ngoma kama holiday likiimbwa kwenye dance floor ilikuwa hatari tupu.
Nakumbuka back to the 90s kuna muwasibu mkubwa tu wa serikali enzi hizo alikua ndio Don wa mtaa. Alikua anatoa mredio wake nje na maspika ya mataataa afu ndio wanakuja hao wana ilikuwa sio kitaa.
Sema jamaa akaacha mbwembwe zake baada ya majambazi kumvamia na jiwe fatuma, walilipua baruti wakafunga mtaa
Dah the old was gold kwakweli.
 
Niliwahi shudia dingi yangu akikata ngoma mpaka leo nikikumbaka nacheka machozi yananitoka😂😂😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…