Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Bora hata ya ngedere unaweza ukamfukuza akakuelewa ila panya anazingua sana labda ukitaka uweze inabidi uende sua wakupe mbegu ya nyoka wasiokua na sumu ufuge hapo shambani hapo hutosikia panya hata kidogo hii biological control niliiona kwenye shamba la mzungu la karanga nachingwea
Ya Nachingwea nilisikia nikajua jamaa wanamidanganya
 
Sawa,kwa sasa naona ni risk sana kufanya kilimo kisichokua cha kumwagilia

Vipi utarudi tena shambani?
Nkipata pesa mkuu ntarejea mkuu.Sema mkuu nna uwanja wangu upo Chamazi kama una mtu anahitaji nicheki ni 7mill
 
Mnaolima matunda huwa nawahurumia sana, kijumla mkulima ni mtu wa kulaliwa tu, ndo maana wengi wanaojua wanajikita katika kununua mazao
Naanza kwa kutoa experience yangu.

Niliingia kwenye kilimo baada ya kushawishika na vipindi vya Clouds Media kuhusiana na fursa. Presenters walishawishi sana kuwa vijana hatujitumi na hatutumii brain zetu vizuri.

Nikajitosa kwenye kilimo cha tikiti Migoli Iringa na milioni zangu 2. Nikaingia front mwenyewe sikutaka kilimo cha simu. Nilikutana na changamoto katika kulima nikapambana nazo nilikuwa nalala shamba kwenye vibanda vya nyasi, vibarua wanazingua balaa na changamoto ya madawa. Baadae nikafanikiwa kuvuna na yalikubali sana.

Mziki ukaja kwenye soko sasa. Unatoka mjini na mfanyabiashara kuja shamba kununua mzigo, mjini umeacha bei ya tikiti 1 ni elfu 4. Mfanyabiashara shamba anataka kununua tikiti 1 sh 500, nikaamua kwenda nayo mwenyewe sokoni Dodoma. Kufika pale, dah! washaambizana wafanyabiashara wao hawanunui direct kutoka kwa mkulima; wananunua kupitia madalali, ikanibidi niwakabidhi madalali mzigo. Hapo nilichoka nilirudi nyumbani na laki 4.

Nikaingia kwenye kilimo cha vitunguu Ruaha Mbuyuni. Nikapambana nacho; jani lilikubali balaa kila siku nikawa napiga picha narusha social media. Wakati wa kuvuna kuja kuchimba chini chenga tu nikaishia kuuza reja reja nikatoka na laki 7.

Nikaja kulima mahindi ya kuchoma maarufu kama Gobo. Nilipambana nayo mpaka mwisho kwenye soko tena changamoto. Mfanyabiashara anakuja kuchagua mahindi shamba anataka kununua muhindi mmoja kwa sh 120 ilihali mjini muhindi mmoja sh 500, nikaghairi kuuza nikasubiri yakauke bahati nzuri bei ya mahindi nzuri.

My take: Katika kilimo madalali na wafanyabiashara ndiyo wanaonufaika sana kuliko wakulima.
 
Mnaolima matunda huwa nawahurumia sana, kijumla mkulima ni mtu wa kulaliwa tu, ndo maana wengi wanaojua wanajikita katika kununua mazao
Ni kweli kabisa dalali/mfanyabiashara anapokuja kununua anakulalia anajua huna ujanja wa kuhifadhi zaid ya siku mbili lazima uuze tu
 
Bora hata ya ngedere unaweza ukamfukuza akakuelewa ila panya anazingua sana labda ukitaka uweze inabidi uende sua wakupe mbegu ya nyoka wasiokua na sumu ufuge hapo shambani hapo hutosikia panya hata kidogo hii biological control niliiona kwenye shamba la mzungu la karanga nachingwea
Kuna mchanganyiko tuliwaekea pamoja na saruji.Tuliwapunguza ila hawakuisha.Nyoka hapana mkuu
 
Niliwai lima matikiti 2016 Simiyu(kilimo cha simu)vijana wakayatelekeza yakauka bila kumwagilia.Tukarudia mara ya pili miche ikasombwa na mafuriko.Nikasamehe kila kitu huko shamba sikufatlia tena..

Nikalima heka tatu za mahindi ya kuchoma.Nikapata vizuri (Msowelo)Akatokea mnunuzi anataka shamba zima kwa kila heka laki 8.Nikaona kama anataka kunilaghai nikagoma mana maindi yalikua mazuri sana na makubwa japo kulikua na changamoto ya panya na ngedere.Ukaidi wangu panya na ngedere wakashambulia na sikupata mnunuzi yakakaukia shamban mengine.Nikavuna nikapiga dawa nikisubiri bei ipande na haikupanda mpaka dawa ikaisha makali yakaanza kubunguliwa.mwisho nikaambulia 350k

Nikaamua kuhamia kwa vitunguu.Nikalima heka tatu.Nilipata vitunguu vya kutosha na vyenye afya.Likatokea jamaa linataka kunipa 15M kwa heka zote tatu.Katokea mshauri (shetani)na kilimo cha mahesabu ya pdf.Nikaona naweza piga zaidi ya 100M.Tamaa zikaniponza sikupata kitu.Baada ya kuvuna nimevihifadhi kwenye chanja kila siku tunavigeuza nikisubiria bei ipande. vingine vinaoza.Vingine vijana shamba wanaiba wanauza,vingine nabeba nyumbani.Kwa makadirio ya chanja gunia zilikua zaidi ya 150.Nikapata mtu wa 70k kila gunia nikagoma aongeze 10k akagoma akakimbia.
Bahati mbaya ikapiga mvua mbaya sana.Sasa vijana kumbe hawakulala shamba.Hata sijui walienda kunywa pombe ama walilala kwa wanawake.Kuna vilivyokuwa vimeanikwa chini vililoa chapa chapa,Chanja alikufunikwa pembeni na maturubai.mvua ilikua kubwa na ya upepo ukavunja na chanja vitunguu vyote vikaloa.Nilifika shamba nikachanganyikiwa.Toka niliondoka hapo sikuwai kurudi na sirudi tena shamba.

Nataka nijaribu ufugaji wa mbuzi ama kuku wa kienyeji nikipata mda.
Na mimi nataka kufuga mbuzi
 
Mimi niliwekeza mkuranga kama 28 mil nikachimba Visima nk, Nikaweka Wafanyakazi wawili, Siku ya kwanza tukapanda Embe ekari nane, asubuhi miche yote imeibiwa ! Niliagiza miche SUA kila mche elfu 3... Roho iliuma hatari..

Nilisikitika mno, nikaanza mboga mboga, mpunga, basi bwana si nikaanza kilimo cha simu, sikuambulia hata shilingi moja ! Nikastop...

Nikahamia kwa broilers, île nataka kuwatoa soko likaharibika hata tuliyekubaliana awe anachukua akashindwa maana naye alikua anapeleka mahala, nikafanya batch nne nikaona sasa huu Msala... Nikastop...

Ila sasa Nimerudi tena kivingine, Nimepata mikataba ya broilers tumesaini ndo nimeanza, nitakua natoa broilers elfu moja kila Wiki, nilichojifunza Ni kutokukata tamaa na kufanyia kazi zile changamoto zilizokukuta, usiache.. Jitafakari anza tena !
Hao broiler unawatengenezea au unawanunulia chakula
 
Mimi nililima mpunga heka kumi ukakubali kweli kweli shamba lilikua langu bwana bwana kukaa hivi napigiwa simu wasukuma wameingiza ng'ombe usiku wamekula shamba lote aisee nilidata. Alafu washenzi wale wamehonga polisi ukienda kushtaki unapigwa danadana tu nilitamani nikapige risasi ng'ombe wote. Morogoro iyo
Washenz sana wafugaji mwaka jana waliingiza ng'ombe wakala dengu zangu zote tukaenda na Mr kutia mikwaraaaaa na kutoa report police,wakiingiza tena ng'ombe zao tutaziuuaa!So far nimeanza kuvuna mpunga hawajaingiza tenaaa wale washenzi ukiwachekea wanakupa umaskini
 
Nimesahau kuongezea nililima Tikikiti nilipata mkuu.wakaja madalali wa moro town wakataka tikikiti kubwa kwa 3000 na dogo kabisa kwa 1500.wakataka zote heka 3.Tamaa dalali wa dar kanipigia simu tikikiti dogo buku3 kubwa mpaka buku7.Kihehere nikaona bora nikauze dar.nikadaka fuso brother.Kuruka bongo daresalam.Nakuta tikiti zimemwagika kama mvua ya mawe.Dalali kaishiwa pozi akaniambia hali ndio hio.Nikauza hadi jero jero nikalipa fuso.Nikarudi zangu moro mpoole kama nimemwagiwa maji...Kama ningekua sina hajira ungekuta nimeshachanganyikiwa.


SHAMBA SIRUDI KAMWE.Nyie nendeni tu.Nawatakia mafanikio mema
Una nyota ya fisi=tamaa... Hapo tu, unaacha mia iliyoko mkonon kwa 300 yakusadikika
 
Risk na tamaa kwako vinaenda sambamba
Sikujui unijui kwanini nikunyweshe chai ya matango?
Tamaa huenda huo ndio udhaifu wangu.Kilimo kina kazi na changamoto nyingi sana.Unapovuna unategemea kupata faida.Kama una ona kuna fursa ya kupata pesa nyingi kwanini usijitose.Maisha ni risk.
 
Back
Top Bottom