Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

2018 ni mwaka stausahau!nilima mpunga mpanda heka3 na ulistawi poa tu ila....narudia tena ila kuna haya matakataka TEMBO yaliutafuna na kuukanyagia matopeni!tangu siku hio tembo ndio kiumbe nambari moja nayemchukia shenji gete amashino genayo ehaha nalechola ngongh'o nabhasange nyane bhenabha!ila kilimo kinatoa wakuu#obheja
 
Hahahaaaaaaaa mkuuu nimecheka kama mazuriii mkuu, poole sana mkuu. "Mashenji sana amashinho genayo"[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hahahaaaaaaaa mkuuu nimecheka kama mazuriii mkuu, poole sana mkuu. "Mashenji sana amashinho genayo"[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Hahah!lekaga do ongw'a bhabha,yaan kama muda wako hujafika hata ufanye nin znakuwa harakat za pimbi...ila eligembe nsabho#obheja
 
Kuongea ni rahis sana ingia field uone utamu wake. Unakodi eneo unaweka matikit then unakod gari unaanza kusambaza una mzigo fuso limejaa ukifika kwa wanunuzi mtaani anakwambia nachukua matikit 15, anaenda kwa mwingine anachukua 6, mwingine anataka mkopo. Kadri siku zinavyoenda yapoteza ubora wakati huko na we gharama zinazidi za kukaa Dodoma pamoja na za kusambaza mzigo.
Na ndiyo maana wafanyabiashara wanachukua mzigo kwa dalali,
manake malipo huwa ni baada ya kazi
 
Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu.

Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
Ulijichanganya mwenyewe,kua na pesa na kwenda shambani hai ku qualify kua MKULIMA,ekari 40 kwa 10m ni wastani wa 250,000tsh kwa ekari moja,hapa gharama zako binafsi sijazitoa...,hebu nipe mchanganuo wa hiyo 250,000 ilifanya nini na nini na ilitosha vipi kwenye ekari moja na ulichokua unategemea kuvuna?,

(maana hichi kiasi ni wavunaji na mlizi peke yake),kwa kifupi 10m ili uvune vizuri hapa nna assume kila kitu kipo okey(shamba,rutuba,maji) italima kwa mafanikio ekari 10-15 tuu ndo itoe gunia kubwa 20-30 kwa ekari moja,nje ya hapo mnadanganywa na hao washauri wenu na wasimamizi.

Vinginevyo uwe na mashine za upandaji na kuvunia kama zile za masanja na shamba ziwe sio za kukodi na rutuba iwe ya kutosha ndo 10m ikulimie 20-30 ecres
 
Na mimi ndio nataka nianze ila mnanivunja moyo.
Moyo haujengwi hapa jukwaani wala kwenye simu mkuu,chagua utachokitafiti vizuri kabisa alafu ingia field,changamoto utazokutana nazo ndo zitakujenga na baada ya muda utakuja kutufundisha hapa
 
Kama umeangukia pua mshukuru Mungu wengine tumeangukia mgongo kabisa yaani hata mbegu ya kupandia tena msimu ujao unaikosa shambani
Wakuu kilimo ni habari nyingine asikwambie mtu
 
Mwaka jana nililima tikiti hekari mbili maeneo ya ruvu yalistawi vizuri sana ila yakiwa yamebakiza wiki moja niyavune lahaula naamka asubuhi nakuta mto ruvu umefurika shamba lote lipo ndani ya maji.

Miguu iliisha nguvu nikajikuta nimekaa chini hata sijui nilikaaje, kuna mzee pale kijijini akaniambia nisikate tamaa msimu wa mvua utakua umewahi, akanipa shamba lake lenye ukubwa wa hekari tatu na nusu ambalo lipo mbali kidogo na mto akaniambia lima bamia.

Ikabidi nivunje kibubu ili nipate hela ya kulimia, mbegu na mbolea hiyo ilikua mwezi wa 11 mwaka jana, hadi kufikia mwezi wa tatu mwaka huu mavuno ya bamia yakawa yamenirudishia mtaji na kafaida kidogo.

Hapa nilipo nimelima shamba lilelile lililonizamishia matikiti mwanzoni tena nimeliongeza limekua hekari nne.

Baada ya kufanya tathmini niligundua kua pamoja na msimu wa mvua kuwahi kama alivyoniambia mzee lakini pia nilichelewa sana kupanda maana nakumbuka nilipanda mwezi wa nane nikiwa na matarajio mvua itaanza mwezi wa 11 mwishoni ambapo nitakua nimeshavuna.

Changamoto za shamba zipo ila uwezekano wa kuzikabili upo mkubwa tu, changamoto ambazo sizijui niza sokoni kwa upande wa tikiti japokua nafanya utafiti wa hapa na pale.

Nitakuja kuleta mrejesho mwezi wa 9.
 
Umeielewa au na ww umeipaste tu hapa??
Mkuu I'm living that philosophy right now kwaiyo huyo philanthropist ni kama alinilenga mm. Nimeielewa nafanya mradi nawekeza sana at the moment expecting the results later.
 
Mimi nililima hekari 40 za mpunga Ifakara (signal). Nilitumia milioni kumi lakini nilikuja kuvuna gunia 14 tu. Na hizo gunia 14 ndiyo pesa ya vibarua; mfano kukata, kukusanya, kupiga kupepeta, kununua viroba. Kwa ufupi ziliishia humo tu.

Niliambulia kupata gunia moja la mpunga nikakoboa nikapata mchele kilo 70. Kesho yake nikapanda basi kurudi Dar Nikawaletea chakula tu kilichopatikana. Nipo Ilala nawaza bora ningefungua duka la spea, ILA YA MUNGU MENGI.
Kilimo cha mvua ni aina nyingine ya tatu mzuka, au biko
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Sitakuja kusahau kifo cha rafiki yangu graduate wa UDOM kamaliza chuo kaona akafanye kilimo kusini huko, basi wafugaji wakawa wanapeleka mifugo shambani kwake akawa anagombana nao mara kwa mara, saa ingine akawa anaenda kuwaambia waache kulisha mifugo Yao shambani kwake, jamaa wakamvizia kalala wakamtia sime kafia hospitali. Na wafugaji wana hela hamna aliyechukuliwa hatua.Mungu amlaze mahala pema peponi.
 
Dah pole Sana mkuu
 
THE HORTICULTURISTS

Jiunge kwenye kundi letu la whatsap tujadili mada mbali mbali kuhusu kilimo.
Kutana na wataalamu upatiwe majibu ya maswali yako kuhusu kilimo.
 
Back
Top Bottom