A
Anonymous
Guest
Machi 2026 nilifanya usaili wa TRA na kufaulu, kisha nikawekwa kwenye kanzidata yao. Mwezi Julai 2026, TRA waliniita mimi na wenzangu 64 kuripoti, lakini tulielekezwa kwenda kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Utumishi ili tuweze kupokelewa kazini.
Tulifuata taratibu zote kama wenzetu wa mwaka jana, ambao walipata vibali vyao bila changamoto yoyote.
Hata hivyo, hadi sasa, baada ya kusubiri kwa karibu miezi mitatu, bado hatujapata vibali hivyo. Tunapofuatilia katika ofisi husika, hatupati majibu ya kueleweka kuhusu kuchelewa huko.
Aidha, kuna madai kuwa baadhi ya watu waliotoa fedha kwa vishoka wamepata barua zao, huku nafasi nyingine zikidaiwa kutolewa kwa ndugu wa baadhi ya wenye mamlaka.
Tunaomba mamlaka husika zichunguze madai haya, zitoe ufafanuzi kuhusu kuchelewa kwa vibali vyetu na kuhakikisha mchakato unafanyika kwa haki na uwazi.