chapachapa
Member
- Jan 14, 2013
- 93
- 21
Naanza kwa kusema MUNGU mkubwa na ashukuriwe.
Naanza kwa kusema majambazi ni watu wabaya Sana tena ni hatari, Binafsi nilikuwa na sehemu yangu ya biashara na nikianzisha biashara ya stationary nikavutiwa na biashara ya kuuza vocha za simu kwa jumla...
Siku ya siku ikafika mchana wa saa 8:30 alikuja mteja mmoja akitaka kununua vocha ya elfu moja tu, pamoja na kumwambia nauza jumla alisisitiza kwamba ana shida ya haraka, nilipompa ghafla akaingia mwingine na mwingine na kuanza kuniambia tumekuja kuchukua pesa unaweka wapi?
Niliona Kama ni ndoto lakini lakini sio ndoto, wote wakichomoa bastola na kukoki kunielekezea nilichofanya ni kupiga yowe la ujasiri na kukata tamaa kwamba liwalo na liwe.
Mmoja akarukia ndani ya eneo ninakohifadhi vocha na pesa na kuanza kukusanya na kujaza mifuko huku nikiwa chini ya ulinzi wao...
Kifupi walifanIkiwa kunipora licha ya makelele niliyopiga msaada wa majirani ulithibitiwa na jambazi mmoja maana walipojaribu kuja risasi moja ilipigwa hewani na kusambaratisha.
Wanausalama walikuja baada ya saa moja na kukuta majambazi wamesepa na kila kitu.
Hata hivyo shukurani kwao maana walifanikiwa kuizingira gari walilitumia baada ya kulitelekeza.
Na jambazi Kiongozi alikamatwa baada ya siku kadhaa.
Kesi ilifuata mlolongo wake na watuhumiwa watatu wakifikishwa mahakamani .... Walifungwa miaka 30... Habari za uhakika wawili walifia jela kwa maradhi mbalimbali
MUNGU ashukuriwe ... Miaka hii ujambazi umepungua