Tuliokoswakoswa kuuawa na majambazi tukutane huku

Tuliokoswakoswa kuuawa na majambazi tukutane huku

Ila majambazi acheni banah wasikie tu wasikukute na wanataka kitu ulichonacho, majambazi ni magaidi yani ni magaidi, mimi walikua wakate shingo na panga, hiyo siku sema gambe likaniokoa, nilikua na vitu kichwani full kujihami yani gambe noma sana, walikua ntu tatu na sisi tupo wawili na jamaa yangu tukavamiwa pah jamaa yangu ni mrefu halafu alikua ni mtu wa makareti ila siku hile alitulia yani ninatembea nae nasema nipo na mwana ni ulinzi tosha, dah sasa tumevamiwa mimi nikaparangana nao na nina gambe kichwani so najiona baunsa sana pigana nao sanaa yani sio mchezo ilikua mida ya usiku kidogo saa sita hivi nimetoka kwenye harusi naelekea club aisehh wale jamaa walinishambulia na mapanga dah jamaa yangu katulia tuli, nikapanga nao mkono sijui hata mkono wa kurusha ngumi nilitoa wapi, niliona suluhu ni kuwa face walinipa mapanga nilivuja damu sana, wakachukua simu na pesa kidogo wakakimbia mfuko wa shati ndiyo kulikua na hela ila hawakusachi zaidi ya mifuko ya suruali, siji sahau hilo nilicheza nilishonwa nyuzi nyingiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka ilikua miaka kadhaa imepita nilivomaliza lasaba nikalazimisha kusafiri na bro alikua dereva wa lori pamoja na kukataliwa ila nilingangania na nikaruhusiwa kwenda io siku bro alikua amepakia viazi vya kwenda dar bhana bhana bhana safari ikaanza ile kufika msata tukakamata bagamoyo rod kwenda kidogo tukaona malori kama mia yamepaki yanawasha dabo hazad bwana we bro akanambia kumekucha lala chini na uloku mlango nikafanya kama nilivoelekezwa na broo .......ile kwenda kidogo kukaribia zile gar tukakuta magogo barabaran na miamba wakatokea maporini wakitutaka tusimame yule alokua anakuja na upande wa kushoto kashika panga bro akampelekea gar kama anataka kumgonga jamaa akalaza ile kukwepa gari broo akaona kumbe kupitia kushoto kwa yale magar kuna njia na inaezapitika bro kwa ufundi wa hali ya juuu alilenga ile njia kama kapimia na rula kwa nyuma tunaskia risasi zimarindima wakapasua tair moja ya nyuma uzuri ile gari ilikua ni tandam tukapona cku io ikawa ndo mwisho wangu wa kungangania safari
 
Back
Top Bottom