Kuna huu unafiki wa wazazi kuwadanganya watoto wao eti wakati wanasoma wao walikuwa wanakuwa wa kwanza darasani, mimi wacha niwe mkweli, nilikuwa nashika nafasi za mkiani darasani nilipokuwa primary, kuna wakati enzi hizo siku ya kufunga shule, wakisomwa wanafunzi hata 40 katika darasa la wanafunzi 50 nilikuwaga sisomwi, huu ulikuwa shule za vijijini, kuna wakati nikasoma shule za mjini, hizo unapewa matokeo kwenye barua, nilikuwaga nashika nafasi ya 30 kati ya wanafunzi 33, hizo ni nafasi za mkiani, namshukuru Mungu sikuwahi kuwa wa mwisho kabisa.
Pamoja na kushika nafasi za mkiani darasani sikukata tamaa, niliendelea kujikongoja, ikafikia wakati nikaanza na mimi kusogea madhabahuni, nafasi za mbele, hadi nikaanza kushika namba moja nilipofika kidato cha 2 hadi namaliza kidato cha 6, nimeingia chuo sikujali tena masomo, nikakalia tu wanawake, kusoma hakuna tena, ila nikamaliza salama, leo hii ni mtu naheshimika katika jamii ingawa katika jukwaa hili nimekuwa naandika mambo ya kuniondolea heshima, ni kwa kuwa ndo tulivyoamua jukwaa hili liende, ukiandika cha maana kinafutwa.
Washika mkia darasani hebu na nyie toeni ushuhuda wenu, je wewe ulibakia kuwa mshika mkia hadi lini? hii ni fursa kuonesha hata washika mkia wanaweza kufanikiwa kutoka mkiani hadi kujijengea heshima katika jamii, tusione soo hata kama tulikuwa washika mkia hadi kunakucha.