Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nilishawai kuwa wa 37 kati ya 43 form two 1996 ,kipindi hicho mama yangu alikuwa anakaanga mihogo ilitusome watoto wanne sekondari plus baba katutelekeza.AISEE mama yangu alivyoona matokeo alilia sana na mimi niliumia sana ndio ikawa mwanzo wakufanya vizuri mpaka leo
Mimi ningekuwa moderator ningekupiga bani ya kufa mtu kwa kusema uongo, hapo kwenye red utasemaje kuwa ukiandika kitu cha maana kinafutwa? Ni mara ngapi umeandika kitu cha maana wakati kwenye JF huna hata miezi mitatu
Kuna huu unafiki wa wazazi kuwadanganya watoto wao eti wakati wanasoma wao walikuwa wanakuwa wa kwanza darasani, mimi wacha niwe mkweli, nilikuwa nashika nafasi za mkiani darasani nilipokuwa primary, kuna wakati enzi hizo siku ya kufunga shule, wakisomwa wanafunzi hata 40 katika darasa la wanafunzi 50 nilikuwaga sisomwi, huu ulikuwa shule za vijijini, kuna wakati nikasoma shule za mjini, hizo unapewa matokeo kwenye barua, nilikuwaga nashika nafasi ya 30 kati ya wanafunzi 33, hizo ni nafasi za mkiani, namshukuru Mungu sikuwahi kuwa wa mwisho kabisa.
Pamoja na kushika nafasi za mkiani darasani sikukata tamaa, niliendelea kujikongoja, ikafikia wakati nikaanza na mimi kusogea madhabahuni, nafasi za mbele, hadi nikaanza kushika namba moja nilipofika kidato cha 2 hadi namaliza kidato cha 6, nimeingia chuo sikujali tena masomo, nikakalia tu wanawake, kusoma hakuna tena, ila nikamaliza salama, leo hii ni mtu naheshimika katika jamii ingawa katika jukwaa hili nimekuwa naandika mambo ya kuniondolea heshima, ni kwa kuwa ndo tulivyoamua jukwaa hili liende, ukiandika cha maana kinafutwa.
Washika mkia darasani hebu na nyie toeni ushuhuda wenu, je wewe ulibakia kuwa mshika mkia hadi lini? hii ni fursa kuonesha hata washika mkia wanaweza kufanikiwa kutoka mkiani hadi kujijengea heshima katika jamii, tusione soo hata kama tulikuwa washika mkia hadi kunakucha.
mkoroshokigali sijakupata mheshimiwa, nataka nijue jinsi ulivyoichukua post yangu ukaileta kwenye post yako na kuijibu, kala maana yake ni nini?
mkuu kuandika vitu vya maana kuna uhusiano wowote na muda mtu aliojisajili hapa?
iam really disappointed with you!
dont judge others by just looking at your front ear only!
Jeki nisamehe tu bure naona wakati nakujibu sikufanya analysis vizuri
nilishawai kuwa wa 37 kati ya 43 form two 1996 ,kipindi hicho mama yangu alikuwa anakaanga mihogo ilitusome watoto wanne sekondari plus baba katutelekeza.AISEE mama yangu alivyoona matokeo alilia sana na mimi niliumia sana ndio ikawa mwanzo wakufanya vizuri mpaka leo
Hahahaha pole sana mkuu