Tuliokuwa tunavutiwa na Rebeca Gyumi tuwe wapole, kuna jamaa ameshafanya kweli

Jaribu ku-google utapata habari zake. Mwakembye na A.G hawana hamu naye maana amewagaragaza kwenye matope Mahakama kuu alipoishitaki serikali kupinga sheria mbovu inayoruhusu ndoa za watoto. Kapewa tuzo huko UN kwa ujasiri wake.
binafsi sikuwahi mfahamu.
ila naomba nionge jambo moja,
mtu yeyote akianzisha movement ya kupigania haki za watoto,wanawake,
au walemavu,mwisho wa siku lazima atashinda tu.

kisheria ni masuala mepesi sana kushinda.so I see nothing special from her.

angejitosa kupigania masuala ya bungelive au sakata la lema,hakika ningemuona mwanamke wa shoka haswa.
 
nilichelewa kwa modesta, nimechelewa kwa huyu, sasa hata sioni kichwa kingine kilichobaki...😀
 
Mkuu naheshimu mawazo yako lakini ujue hiyo sheria aliyoipinga ilikuwepo tangu siku nyingi tu lakini hakuna mtu mwingine aliyefikiria au kuonyesha uthubutu wa kuipinga. Kubadilisha sheria mbovu kwa hapa kwetu sio kazi rahisi ndio maana hata zile sheria kandamizi zilizoanishwa na kina Nyalali na Kisanga na mpaka leo hazijafutwa. Mbona mimi naona masuala ya Bungelive, ukiukwaji wa katiba na sakata la kina Lema ni ya kawaida tu. Japo hiyo Tuzo ya kimataifa aliyopewa haikuwa kenye malengo yake lakini sidhani kama ingeipata kwa kujishughulisha na hayo masuala uliyoyaanisha.
 
Haitokei kila mwezi kijana wa kitanzaia kupewa Tuzo ya kimataifa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na kuhojiwa na kina Christine Amanpour wa CNN. Ikitokea ujue jambo lililofanyika sio la kawaida.
 
basi sawa.
 


Bongo bila kukaa uchi, kutawaliwa na scandals, au kujihusisha na siasa zetu, hatufuatilii kabisa. Humu wengi ni wadau wa ubuyu, so insta ndiyo makazi, ila kwa aliye Twitter karibu na TOT angemjua huyu bibie na harakati zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…