A
Anonymous
Guest
Naomba kufikisha kilio chetu kuhusu haki ya mafao yetu ya NSSF. Sisi ni wafanyakazi tuliokuwa katika Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call Center) cha TANESCO, tulioajiriwa kupitia Kampuni ya Erolink, kwa kipindi chote tulichofanya kazi, mwajiri wetu hakuwasilisha michango yetu ya NSSF, na licha ya mkataba wake na TANESCO kumalizika, bado hajatekeleza wajibu huo.
Tumefuatilia mara kadhaa bila kupata ushirikiano wa kuridhisha. Wengi wetu kwa sasa hatuna ajira, tuna familia zinazotutegemea, na maisha yamekuwa magumu. Haya ni mafao yetu ya halali ambayo tunastahili kuyapata.
Pia soma:
~ Kampuni ya EROLINK ni wababaishaji, wanawanyonya vijana waliowaajiri
~ Erolink: Kampuni inayowanyanyasa Watanzania. Ichukuliwe hatua za kisheria
~ Kampuni ya Erolink Limited imetukata fedha za NSSF lakini fedha hazifiki na NSSF hawasemi chochote
~ Ero Link Recruitment Agency - Scandal
Kwa heshima, tunaomba uingilie kati ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuhakikisha tunapata haki yetu. Tunaamini msaada wako unaweza kuwa mwanzo wa suluhisho kwa vijana, akina mama na akina baba wengi wanaoathirika na tatizo hili.
Tunashukuru kwa muda wako na tunatumaini utalisikia ombi letu.
Walichojibu TANESCO ~ Ufafanuzi wa TANESCO kuhusu mafao ya Wafanyakazi wa Call Center