Kutokana na miundombinu mibovu kama barabara kujaa maji automatically magari yana slowdown na mengine yanazimika njiani. Slowdown ya, say, one hour rush hours athari zake sio mchezo. Kwa mfano, kwenye kipande ambacho kwa dk. 30 yalitakiwa yawe yamekatiza magari 1000 under normal circumstances badala yake under slowdown yatakatiza, say, 400 hivyo utaona ndani ya muda huo huo wa slowdown magari 600 yatalazimika kuwa "on waiting" ambayo ndio foleni yenyewe!
Huo ni mfano wa dk. 30 tu; kadiri muda unavyoenda ndivyo speed inazidi kupungua na rate ya foleni kuongezeka hadi itafikia situation hakuna gari linalosogea! Na hali huwa mbaya zaidi blockage inapotokea kwenye junction; hakuna gari inayokatiza kuelekea upande wowote yanakuwa yameji-lock kwenye loop ambayo hakuna kwenda wala kurudi - stand still mode. Simple mathematics!
Hata katika mazingira ambayo sio ya mvua au hali mbaya ya hewa, ukikukatana na dereva mmoja mpuuzi naendesha kijinga rush hours "mtukane" maana madhara anayosababisha huko nyuma sio ya kawaida. In fact, kuna haja ya kuangalia upya sheria 50km/hrs; ifike mahali kuwe na minimum speed baadhi ya maeneo kuondoa kero ya foleni.