Tuliona Tulioyoyaona: Ukuu wa Kihistoria na Laana ya Kiti cha Enzi

Tuliona Tulioyoyaona: Ukuu wa Kihistoria na Laana ya Kiti cha Enzi

Yako Atta

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2016
Posts
288
Reaction score
468
Tuliona tuliyoyaona Zimbabwe ya Mugabe wa ZANU PF na Morgan Tsvangirai wa MDC, tuliyajua pia ya Venuzuela ya Hugo Chavez kabla ya Nicolas Maduro na baada ya Nicolas Maduro-Venezuela: Populism, Petro-State na Mporomoko wa kiuchumi. Huenda tuliona ndivyo sivyo na pengine zilikuwa ni taswira zaidi ya moja tafauti, lakini matokeo ya madhila yenye kufanana, Utu wa Mtu ulitwezwa na kuhiniwa. Hata Somalia ya baada ya Siad Barre tulipata na tumebahatika kuiona hata sasa .Kuanguka kwa serikali ya Siad Barre mwaka 1991 kulisababisha taifa kukosa mfumo wa katiba, uthabiti na mamlaka ya kati rejea Menkhaus, K. (2007). “The Crisis in Somalia: Tragedy in Five Acts.” African Affairs. Ni mfano wa nchi ambako kutoweka kwa taasisi rasmi na zisizo rasmi kunazaa vurugu za kudumu.

Sina hakika kama kuna ambaye hakuiona Rwanda ya baada ya April 1994, rejea Straus, S. (2006). The Order of Genocide: Race, Power, and War in Rwanda. Dunia ni kama tulivuliwa nguo, tulikuwa tukifanya nini zaid ya watu milion 1 wakiuwawa na kutupwa mto Kagera?

Hakuna yeyote mwenye yakini ya kile tulichokiona kote huko na tunachokiona hata sasa, lakini hatukustahili kushuhudia ila tulilazimika kuwa mashuhuda na hakuna ambacho tuliweza kufanya. Muhimu ni kwamba hayakuwa matukio mapya, yalishashuhudiwa toka Rumi ya kale, Uingereza, Ufaransa hata Marekani ya kipindi cha uhuru na uasi dhidi ya Ufalme wa Uingereza.

Swali ni moja fikirishi, walikosea wapi na walikosea nini? Ni sera zao kinzani dhidi ya mifumo ya utawala wa kidunia au ukosefu wa ustahimilivu wa kitaifa?

Wasomi wa siasa wanaeleza kwamba migogoro hutokea pale ambapo matarajio ya kisiasa yanakua haraka kuliko uwezo wa taasisi kuyadhibiti rejea Huntington, S. P. (1968). “Political Order in Changing Societies”.

Ninapojaribu kuwaza sana, nafikia hitimisho la kuwa najichosha, huenda isiwe kushindwa kwa sera wala isiwe kukosekana kwa ustahimilivu na huenda pia vikawa vyote kwa pamoja ama visiwe vyote kwa pamoja.

Kushindwa kwa mifumo ya utawala ni mchakato unaochukua muda. Hakuna litokealo ghafla. Kuna sehemu ni lazima ilikiukwa na mchakato wa mparaganyiko ulianzia hapo. Wakati fulani Dunia ni kama Treni, ina njia yake na kamwe haiwezi kutembea nje ya njia hiyo. Lakini hakuna urahisi wa utabiri juu ya kufika kwake au kuparaganyika kwake njiani. Kila Taifa lina nguzo na mifumo yake ya kiutawala na inayofanya Taifa hilo liendelee kuwa moja. Ni kama maagano ambayo wakati mwingine si rasmi lakini yenye kutambulika na kuheshimiwa.

Siasa yetu ya baada ya Ben Mkapa, 2005-2015, kunajisika kwa Ikulu, kupotea kwa ushawishi wa Chama Tawala na hitaji la haraka la kunusuru Chama na The class of Elites(The Establishment) kulimleta aliyekuja baada ya hapo (The Populist) itakuwa ni vigumu sana kumhukumu Marehemu bila kuangalia madudu ya Kabla yake. Hitaji lilimfanya kufanya aliyoyafanya lakini kama Taifa bado tulikuwa katika ustahimilivu wetu kama nguzo yetu kitaifa. Hakika alifanya aliyoyafanya na si haba tulistafidi ingawa pia kama binadamu alikosea sana.

Huenda tulikosea hesabu zetu kisiasa 2015. Ni vipi tungepatia ilhali tuliharibu miaka yote kumi ya kula kucheka na kuimarisha mkataba wetu wa Mwitongo?

Makosa makubwa yalifanyika 2021 pale the elites walipokosa ustahimilivu na kumfikia marehemu rejea chapisho la Malcolm Lumumba Jamii Forum "Mfalme akiuwawa huwa inachukua muda mrefu Taifa Kupona"

Ikiwa kweli Mamlaka hutoka kwa mungu, basi kuihini mamlaka ya kiungu ni laana kubwa, Dhulma aliyofanyiwa Marehemu itachukua muda kuliponya Taifa hili. Na kuvunjwa kwa nguzo ya kitaifa ya Ustahimilivu ni LAANA na mzimu wa marehemu utaendelea kukiandama kiti chake. Kumbukeni Vilio vikubwa vya uchungu vya wafuasi Maamuma wa marehemu, kumbukeni shangwe na vifijo vya wale waliokuwa wakikwazwa na aliyoyafanya marehemu na vipi hali ya sasa?

Kiti hakijatulia, kiti hakitatulia hivi punde, kuna gharama ya kulipa na tutapaswa kuilipa. Huenda yaliyotokea Oktoba 29, 2025 ni advance payment au first Installment ya gharama halisi tunayipaswa kuilipa ambayo bado hatuijui. Hakuna dhulma iliyowahi kufanywa na isilipwe. Alidhulumiwa Qadafi 2011, Libya imeandamwa na Laana mpaka leo, alidhulumiwa Cyprian Ntryamira na Habyarimana tulishuhudia laana kubwa zaidi barani Afrika, Sometimes in April. Mzimu wa Lumumba umeipa laana DRC. Kamwe kiti cha enzi cha DRC hakijawahi kutulia na hakitatulia hivi karibuni.

Kiti hakitatulia hivi karibuni, hata akitoka huyu aliyopo hakuna matumaini ya kutulia kwa kiti. Hakuna katika kariba yao wa kuweza kutuliza hali iliyopo kwa sasa. Hakuna mwenye hekima na Busara. Ni kama hatuna wazee. Tuna kizazi cha watumishi wastaafu wasiotaka kuzeeka, waliogoma kuzeeka, walioshindwa kuishi na kujifunza ili waje kuwa na busara uzeeni. Wamezeeka mwili ni kama hawajabaleghe kiakili. Hawaioni hatari, ni kama sote tupo gizani.

Matokeo ya kushindwa kwa sera, matokeo ya kuishi kwa nadharia, matokeo ya kuishi kwa hadaa, huzaa ufedhuli, ufisadi na kutojali. Wenye dhamana ya kuilinda na kuitunza Demokrasia wamejiweka pembeni, wameungana kimaslahi na watesi-huenda ni kundi moja.

Madaraka ya nchi ni taasisi takatifu.
Hayapaswi kuguswa kwa pupa au maslahi ya muda mfupi. Historia inaonyesha kuwa kuvunjika kwa mfumo wa kitaifa hubeba gharama na hakuna taifa linaloepuka kulipa hizo gharama.

Kama ilivyo Rwanda, Libya, Somalia na DRC, dhana ya “mamlaka ni agano” inabaki kuwa msingi wa utulivu.
Kukiuka agano hilo kunazaa mzunguko wa laana za kisiasa na kiti cha enzi hakiwezi kutulia hadi makosa ya kihistoria yatakapokiriwa na kurekebishwa.
 
Kumbukumbu nzuri.
Nakuongezea laana ya kuuwawa mfalme wa Kushi Haile Selassie,
Laana ya kuuwawa Thomas Sankara, .......
Samuel Doe wa Liberia na kilichofuata bloodshed ya akina General Mosquito.
 
Back
Top Bottom