Tuliooa kwa mahari ndogo tuje tuseme lolote juu ya jambo letu hili

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
28,481
Reaction score
28,749
Leo niko huku kwa mtindo huu, ila nasikia leo ni siku ya kina mama (Wanawake) duniani maana yake siku zilizobaki ni zetu sisi kina baba, yaani kwa thamani na nafasi ya mwanamke ambaye natakiwa kumpa mara tatu zaidi ya baba, kwa mwaka anaadhimishwa mara moja. Huu ni udogashaji na udhalilishaji wa hali ya juu, ila maskini wenyewe vipofu wanaona sawa, utawaona wamevaa vitenge na kutembea uchi. Salamu zangu ndiyo hizo nawaambia waache habari za siku ya mwanamke duniani, hii ni aina ya udhalilishaji kwake.

Baada ya salamu hizo, narudi kwenye mada kwa mapito haya, asikwambie Mtu,ndoa yenye baraka ni ile ambayo kufungwa kwake mahari yake ilikuwa ndogo sana. Haya si maneno yangu, bali ni maneno yaliyotoka katika kinywa twahara.

Ni nini ndoa na kwanini tunaumizana katika kutoa mahari kubwa bila sababu za msingi hali ya kuwa sote ni wanufaika na wahitaji. Ndoa ni mkataba wa maridhiano baina ya pande mbili,mwanamke akiwa muolewaji kwa mahari waliyokubaliana na mwanamume akiwa muoaji, kwa kukubaliana waishi kwa wema, na kama ikitokea wameachana basi waachane kwa wema.

Tuliokadiriwa kutoa mahari ndogo, tuje tuwaambie vijana na watajaji mahari ya kuwa ndoa ni jambo le kheri,kwahiyo tusiumizane.

Mimi mahari niliyotoa kwa mke mkubwa ilikuwa chini ya Tsh 150,000/- pesa taslimu.

Vijana tuoeni mapema na tuoe sana, wake wawili au watatu au wanne ikibidi ila ukiwa na mmoja kuwa nae lakini uwe na simanzi kubwa ya kwanini uwe na mmoja.
 
Wapi huko shekhe wangu na Sisi tuende!
Tafuta wapo kibao, ila kaa ukijua ya kuwa ndege wafananao huruka pamoja.

Mimi kuna swahiba wangu mmoja, alioa kwa mahari ya Juzuu, nenda kaulizie bei ya juzuu madukani utaambiwa, nahisi juzu halizi Tsh 500/-.

Haya mambo sijui kwanini watu wanayatia uzito namna hii.
 
Ni kweli Kaka, kama ulivyosema ndoa yenye baraka ni Ile yenye mahari ndogo! Au kama qaala Mustafa alayhi swalatu waswalaam!
 
Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha. Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari, tulipofika mzee akaita binti yake, Mankaaaaa njoo hapa! Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana? Umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba. Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vizuri hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda, yaani niko frontline utadhani mimi mtoto wao wa kiume.
 
Ila Uislamu ni raha asikudanganye mtu, nilifunga ndoa pamoja na mahari kwa shillingi 70,000 ukijumulisha pamoja na usafiri.......sasa ni mwaka wa 9 watoto watatu, nyumba tumejenga gari tunazo mahaba tunayo pia
 
Leo niko huku kwa mtindo huu, ila nasikia leo ni siku ya kina mama (Wanawake) duniani maana yake siku zilizo baki ni zetu sisi kina baba, yaani kwa thamani na nafasi ya mwanamke ambaye natakiwa kumpa mara tatu zaidi ya baba, kwa mwaka anaadhimishwa mara moja.
Nisamehe post hainihusu ila nimepita kukuambia Men's International Day ni tarehe 19 November. Kwahiyo siku zilizobaki sio zenu.
Anyway, Happy belated International Men's day Jurjani.
 
Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha.Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari,tulipofika mzee akaita binti yake,Mankaaaaa njoo hapa!
Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana?umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba.
Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vzr hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda,yani niko frontline utadhani mm mtoto wao wa kiume

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Leo niko huku kwa mtindo huu, ila nasikia leo ni siku ya kina mama (Wanawake) duniani maana yake siku zilizo baki ni zetu sisi kina baba, yaani kwa thamani na nafasi ya mwanamke ambaye natakiwa kumpa mara tatu zaidi ya baba, kwa mwaka anaadhimishwa mara moja. Huu ni udogashaji na udhalilishaji wa hali ya juu, ila maskini wenyewe vipofu wanaona sawa, utawaona wamevaa vitenge na kutembea uchi. Salamu zangu ndiyo hizo nawaambia waache habari za siku ya mwanamke duniani, hii ni aina ya udhalilishaji kwake.

Baada ya salamu hizo, narudi kwenye mada kwa mapito haya, asikwambie Mtu,ndoa yenye baraka ni ile ambayo kufungwa kwake mahari yake ilikuwa ndogo sana. Haya si maneno yangu, bali ni maneno yaliyotoka katika kinywa twahara.

Ni nini ndoa na kwanini tunaumizana katika kutoa mahari kubwa bila sababu za msingi hali ya kuwa sote ni wanufaika na wahitaji. Ndoa ni mkataba wa maridhiano baina ya pande mbili,mwanamke akiwa muolewaji kwa mahari waliyokubaliana na mwanamume akiwa muoaji, kwa kukubaliana waishi kwa wema, na kama ikitokea wameachana basi waachane kwa wema.

Tuliokadiriwa kutoa mahari ndogo, tuje tuwaambie vijana na watajaji mahari ya kuwa ndoa ni jambo le kheri,kwahiyo tusiumizane.

Mimi mahari niliyotoa kwa mke mkubwa ilikuwa chini ya Tsh 150,000/- pesa taslimu.

Vijana tuoeni mapema na tuoe sana, wake wawili au watatu au wanne ikibidi ila ukiwa na mmoja kuwa nae lakini uwe na simanzi kubwa ya kwanini uwe na mmoja.
Kwenye uislamu kuna KUOANA hakuna KUOA wala KUOLEWA.
 
Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha.Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari,tulipofika mzee akaita binti yake,Mankaaaaa njoo hapa!
Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana?umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba.
Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vzr hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda,yani niko frontline utadhani mm mtoto wao wa kiume
Hilo ni tatizo lenu binafsi.
 
Leo niko huku kwa mtindo huu, ila nasikia leo ni siku ya kina mama (Wanawake) duniani maana yake siku zilizo baki ni zetu sisi kina baba, yaani kwa thamani na nafasi ya mwanamke ambaye natakiwa kumpa mara tatu zaidi ya baba, kwa mwaka anaadhimishwa mara moja. Huu ni udogashaji na udhalilishaji wa hali ya juu, ila maskini wenyewe vipofu wanaona sawa, utawaona wamevaa vitenge na kutembea uchi. Salamu zangu ndiyo hizo nawaambia waache habari za siku ya mwanamke duniani, hii ni aina ya udhalilishaji kwake.

Baada ya salamu hizo, narudi kwenye mada kwa mapito haya, asikwambie Mtu,ndoa yenye baraka ni ile ambayo kufungwa kwake mahari yake ilikuwa ndogo sana. Haya si maneno yangu, bali ni maneno yaliyotoka katika kinywa twahara.

Ni nini ndoa na kwanini tunaumizana katika kutoa mahari kubwa bila sababu za msingi hali ya kuwa sote ni wanufaika na wahitaji. Ndoa ni mkataba wa maridhiano baina ya pande mbili,mwanamke akiwa muolewaji kwa mahari waliyokubaliana na mwanamume akiwa muoaji, kwa kukubaliana waishi kwa wema, na kama ikitokea wameachana basi waachane kwa wema.

Tuliokadiriwa kutoa mahari ndogo, tuje tuwaambie vijana na watajaji mahari ya kuwa ndoa ni jambo le kheri,kwahiyo tusiumizane.

Mimi mahari niliyotoa kwa mke mkubwa ilikuwa chini ya Tsh 150,000/- pesa taslimu.

Vijana tuoeni mapema na tuoe sana, wake wawili au watatu au wanne ikibidi ila ukiwa na mmoja kuwa nae lakini uwe na simanzi kubwa ya kwanini uwe na mmoja.
Mke wa pili mahari ulitoa sh.ngapi?
 
Back
Top Bottom