Tuliooa kwa mahari ndogo tuje tuseme lolote juu ya jambo letu hili

Kusheherekea jmsiyo jambo ubaya ni nini unasherehekea na je ulazima wa kufanya hilo upo na je kuna natija ya kufanya hivyo ?

Ni ipi maana ya kusherehekea siku ya Wanawake duniani ? Sijaona haja hiyo na sababu ninazo.
Almost celebration zote sio lazima kuzi-celebrate. Na kucelebrate sio jambo la lazima ni jambo la hiari kwa mtu anayependa kufanya hivyo. Ndio maana sio watu wote wanasherekea.

Nikujibu kwa kuuliza swali, kwanini unasherekea Independence Day? Kuna ulazima gani? Kwanini kuna sherehe za muungano? Zina ulazima gani? Kwanini unasherekea Valentine's Day? Kuna ulazima gani?

Edit: sababu zako ni zipi?
 
Nikujibu kwa kuuliza swali, kwanini unasherekea Independence Day? Kuna ulazima gani? Kwanini kuna sherehe za muungano? Zina ulazima gani? Kwanini unasherekea Valentine's Day? Kuna ulazima gani?
Mimi hizo zote ulizo zitaja sisherehekei hata moja. Mimi nina sikukuu tatu tu basi kwa mwaka,nazo ni :

1. Kila siku ya Ijumaa kwangu ni sikukuu
2. Idd al Fitri
3. Idd al Adh'ha (Idd ya kuchinja)

Sasa maswali yako yanatakiwa yatokee katika hizo sikukuu tatu hapo juu.

Tanbihi : Hivi sahihi ni "Sherekea" au "Sherehekea" ?
 
Almost celebration zote sio lazima kuzi-celebrate. Na kucelebrate sio jambo la lazima ni jambo la hiari kwa mtu anayependa kufanya hivyo. Ndio maana sio watu wote wanasherekea.
Hapa kidogo napingana na wewe. Maelezo ya kwanini, yatafata baadae pakionekana kama kuna haja ya kufanya hivyo.
 
Mimi hizo zote ulizo zitaja sisherehekei hata moja. Mimi nina sikukuu tatu tu basi kwa mwaka,nazo ni :

1. Kila siku ya Ijumaa kwangu ni sikukuu
2. Idd al Fitri
3. Idd al Adh'ha (Idd ya kuchinja)

Sasa maswali yako yanatakiwa yatokee katika hizo sikukuu tatu hapo juu.

Tanbihi : Hivi sahihi ni "Sherekea" au "Sherehekea" ?
Wewe hausherehekei lakini zipo na watu wanasheherekea. Na zingine ulikuwa unaambiwa usiende shule usiende kazini na unabaki home.

Sikimbuki kuona umehoji juu ya watu ku-celebrate juu ya hizo siku.
Why Women's Day? Ni muda wa kunipa zile sababu zako.

Asante kwa masahihisho sijui neno sahihi ni lipi ila naamini hilo uliloandika wewe.
 
Hapa kidogo napingana na wewe. Maelezo ya kwanini, yatafata baadae pakionekana kama kuna haja ya kufanya hivyo.
Kwanini unapingana na mimi? Kupingana na mimi ni kinyume ya nilichoandika.
Hiyo ikimaanisha kwamba celebration zote ni lazima kusheherekea na watu wote lazima washerehekee.
 
Wewe hausherehekei lakini zipo na watu wanasheherekea. Na zingine ulikuwa unaambiwa usiende shule usiende kazini na unabaki home.
Sahihi kabisa.
Sikimbuki kuona umehoji juu ya watu ku-celebrate juu ya hizo siku.
Why Women's Day? Ni muda wa kunipa zile sababu zako.
Hizo sijahoji sababu ubatili wake ni maarufu sana.

Nahoji hii sababu, ukimtengeneza Mwanamke ndiyo umetengeneza jamii.
 
Kwanini unapingana na mimi? Kupingana na mimi ni kinyume ya nilichoandika.
Hiyo ikimaanisha kwamba celebration zote ni lazima kusheherekea na watu wote lazima washerehekee.
Hapana hujanielewa. Zipo sherehe ambazo ni lazima kusherehekea, na nyingine hata hazipaswi kuwepo kabisa achilia mbali kusherehekea.
 
Leo niko huku kwa mtindo huu, ila nasikia leo ni siku ya kina mama (Wanawake) duniani maana yake siku zilizobaki ni zetu sisi kina baba, yaani kwa thamani na nafasi ya mwanamke ambaye natakiwa kumpa mara tatu zaidi ya baba, kwa mwaka anaadhimishwa mara moja. Huu ni udogashaji na udhalilishaji wa hali ya juu, ila maskini wenyewe vipofu wanaona sawa, utawaona wamevaa vitenge na kutembea uchi. Salamu zangu ndiyo hizo nawaambia waache habari za siku ya mwanamke duniani, hii ni aina ya udhalilishaji kwake.

Baada ya salamu hizo, narudi kwenye mada kwa mapito haya, asikwambie Mtu,ndoa yenye baraka ni ile ambayo kufungwa kwake mahari yake ilikuwa ndogo sana. Haya si maneno yangu, bali ni maneno yaliyotoka katika kinywa twahara.

Ni nini ndoa na kwanini tunaumizana katika kutoa mahari kubwa bila sababu za msingi hali ya kuwa sote ni wanufaika na wahitaji. Ndoa ni mkataba wa maridhiano baina ya pande mbili,mwanamke akiwa muolewaji kwa mahari waliyokubaliana na mwanamume akiwa muoaji, kwa kukubaliana waishi kwa wema, na kama ikitokea wameachana basi waachane kwa wema.

Tuliokadiriwa kutoa mahari ndogo, tuje tuwaambie vijana na watajaji mahari ya kuwa ndoa ni jambo le kheri,kwahiyo tusiumizane.

Mimi mahari niliyotoa kwa mke mkubwa ilikuwa chini ya Tsh 150,000/- pesa taslimu.

Vijana tuoeni mapema na tuoe sana, wake wawili au watatu au wanne ikibidi ila ukiwa na mmoja kuwa nae lakini uwe na simanzi kubwa ya kwanini uwe na mmoja.
Ilikuwa enzi za Mwalimu au hizi hizi za JPM?
 
Tofauti yangu mimi na wewe ni kuwa, wewe unazungumzia matokeo mimi naongelea asili, siku zote asili haipitwi na wakati.
 
Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha. Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari, tulipofika mzee akaita binti yake, Mankaaaaa njoo hapa! Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana? Umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba. Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vizuri hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda, yaani niko frontline utadhani mimi mtoto wao wa kiume.
Eti uko font fedi🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Leo niko huku kwa mtindo huu, ila nasikia leo ni siku ya kina mama (Wanawake) duniani maana yake siku zilizobaki ni zetu sisi kina baba, yaani kwa thamani na nafasi ya mwanamke ambaye natakiwa kumpa mara tatu zaidi ya baba, kwa mwaka anaadhimishwa mara moja. Huu ni udogashaji na udhalilishaji wa hali ya juu, ila maskini wenyewe vipofu wanaona sawa, utawaona wamevaa vitenge na kutembea uchi. Salamu zangu ndiyo hizo nawaambia waache habari za siku ya mwanamke duniani, hii ni aina ya udhalilishaji kwake.

Baada ya salamu hizo, narudi kwenye mada kwa mapito haya, asikwambie Mtu,ndoa yenye baraka ni ile ambayo kufungwa kwake mahari yake ilikuwa ndogo sana. Haya si maneno yangu, bali ni maneno yaliyotoka katika kinywa twahara.

Ni nini ndoa na kwanini tunaumizana katika kutoa mahari kubwa bila sababu za msingi hali ya kuwa sote ni wanufaika na wahitaji. Ndoa ni mkataba wa maridhiano baina ya pande mbili,mwanamke akiwa muolewaji kwa mahari waliyokubaliana na mwanamume akiwa muoaji, kwa kukubaliana waishi kwa wema, na kama ikitokea wameachana basi waachane kwa wema.

Tuliokadiriwa kutoa mahari ndogo, tuje tuwaambie vijana na watajaji mahari ya kuwa ndoa ni jambo le kheri,kwahiyo tusiumizane.

Mimi mahari niliyotoa kwa mke mkubwa ilikuwa chini ya Tsh 150,000/- pesa taslimu.

Vijana tuoeni mapema na tuoe sana, wake wawili au watatu au wanne ikibidi ila ukiwa na mmoja kuwa nae lakini uwe na simanzi kubwa ya kwanini uwe na mmoja.
Mahari Laki saba ilikuwa Mwaka gani?
 
Women's day kwanini haipaswi kuwepo?
Inampoteza Mwanamke.

Kwanini unataka iendelee kuwepo au unaionaje wewe ? Kwa hadhi ya Mwanamke je siku hii inaweza kukidhi haja ?
 
Back
Top Bottom