Tuliooa kwa mahari ndogo tuje tuseme lolote juu ya jambo letu hili

Tuliooa kwa mahari ndogo tuje tuseme lolote juu ya jambo letu hili

Naona mada imetoka kwenye mahari Hadi..kusherekea women's day..

Sijaona hao wanazuoni wakitoa dalili za kutosherekea Sherehe...zaidi ya kusema zimeanzishwa na wasio waasilamu

Na watakao iga Mila za wasio waisilamu ...hawapo nasi..

Kweli kuna mambo yakuiga SI mazuri...lakini sherehe kama birthday...zinakatazwa kusheherekea,.. women's day ....zinakatazwa.. kusherekea....mwaka Mpya Hali kadhalika..

Mimi...naishi kwa kufuata maamrisho na makatazo ya Allah...na kufuata sunna za Mtume...

Mengine natumia Common Sense
 
Leo niko huku kwa mtindo huu, ila nasikia leo ni siku ya kina mama (Wanawake) duniani maana yake siku zilizobaki ni zetu sisi kina baba, yaani kwa thamani na nafasi ya mwanamke ambaye natakiwa kumpa mara tatu zaidi ya baba, kwa mwaka anaadhimishwa mara moja. Huu ni udogashaji na udhalilishaji wa hali ya juu, ila maskini wenyewe vipofu wanaona sawa, utawaona wamevaa vitenge na kutembea uchi. Salamu zangu ndiyo hizo nawaambia waache habari za siku ya mwanamke duniani, hii ni aina ya udhalilishaji kwake.

Baada ya salamu hizo, narudi kwenye mada kwa mapito haya, asikwambie Mtu,ndoa yenye baraka ni ile ambayo kufungwa kwake mahari yake ilikuwa ndogo sana. Haya si maneno yangu, bali ni maneno yaliyotoka katika kinywa twahara.

Ni nini ndoa na kwanini tunaumizana katika kutoa mahari kubwa bila sababu za msingi hali ya kuwa sote ni wanufaika na wahitaji. Ndoa ni mkataba wa maridhiano baina ya pande mbili,mwanamke akiwa muolewaji kwa mahari waliyokubaliana na mwanamume akiwa muoaji, kwa kukubaliana waishi kwa wema, na kama ikitokea wameachana basi waachane kwa wema.

Tuliokadiriwa kutoa mahari ndogo, tuje tuwaambie vijana na watajaji mahari ya kuwa ndoa ni jambo le kheri,kwahiyo tusiumizane.

Mimi mahari niliyotoa kwa mke mkubwa ilikuwa chini ya Tsh 150,000/- pesa taslimu.

Vijana tuoeni mapema na tuoe sana, wake wawili au watatu au wanne ikibidi ila ukiwa na mmoja kuwa nae lakini uwe na simanzi kubwa ya kwanini uwe na mmoja.
Hongereni mimi mahari ilikuwa 3m.
 
My dear.. Wacha watu waishi watakavyoo..kusherekea women's day Kuna muuzi Mungu?... Kufanya Sherehe sijui ya birthday Napo.. masheikh wanapinga.... Je nikisherekea kufauli mtihani... nikisherekea mavuno ....

Kuna tatizo Fatawa zimekuwa nyingi... Usisherekee lizika na iddi mbili TU... kusherekea Kuna tatizo gani.....?
Sawa.
 
Jurjani...kuwa was Kati na Kati katika Dini...

Mtu akiamua kusherekea achana nae.
.Mimi nafurahi Mwenyezi Mungu kunifikisha mwaka Mpya... Napika pilau langu na soda nakunywa...NALALA.

Hapa kosa langu lipowapi?
Wewe ukifanya mambo huwa unatarajia nini hasa kifurahisha nafsi yako kupata thawabu au unafanya kuwafurahisha watu na ruwaza yako ni nani ?

Hapo kosa lako lipo, tena kosa kubwa, nitakwambia hapo baadae.

Ukati na kati ndiyo sifa ya Umma huu, na dini ukiifanya ngumu lazima itakushinda na mimi nipo katika ukati na kati ndiyo maana naangalia maslahi zaidi kuliko kupoteza hela na muda.
 
Ila Uislamu ni raha asikudanganye mtu, nilifunga ndoa pamoja na mahari kwa shillingi 70,000 ukijumulisha pamoja na usafiri.......sasa ni mwaka wa 9 watoto watatu, nyumba tumejenga gari tunazo mahaba tunayo pia
Hiyo raha umeipima kwenye unafuu wa mahari au?
 
Hiyo raha umeipima kwenye unafuu wa mahari au?
Mkuu Mambo mengi sana uislamu una unafuu sanaa, ila mada iliokuepo ni mahari, ndo maana nimetoa mfano huo tu.....

Tena likija suala la kufiwa achana na waislamu watakuzikia ndg yako hata ukiwa huna shilling 100, waislamu hawana mbwembwe katika masuala ya msingi, kwenye Dini.
 
Naona mada imetoka kwenye mahari Hadi..kusherekea women's day..
Hizi zilikuwa salamu tu kuja kwenu. Mada ya msingi ni Mahari.

Wewe mahari yako utataja kiasi gani au itakuwa nini ?
Sijaona hao wanazuoni wakitoa dalili za kutosherekea Sherehe...zaidi
Hapa inaonyesha wazi hujasoma hizo dalili, ila zipo nyingi sana.

Pili, naomba unitajie Wanazuoni wako japo watatu tu ambao unawarejea na kuwaamini.
Na watakao iga Mila za wasio waisilamu ...hawapo nasi..
Maana ya kutokuwa nasi unajua ni nini ? Hili jambo zito sana.
Kweli kuna mambo yakuiga SI mazuri...lakini sherehe kama birthday...zinakatazwa kusheherekea,.. women's day ....zinakatazwa.. kusherekea....mwaka Mpya Hali kadhalika..
Kwetu sisi tunaamini ya kuwa hakuna jambo jema kwalo kinatukurubisha zaidi kwa Allah ambalo Mtume hakutuambia wala hakuna jambo baya kwalo linatuweka mbali na Allah, ambalo Mtume hajatutahadharisha kwalo.

Ikiwa wewe na mimi ruwaza wetu ni Mtume, nitakuuliza Mtume alikuwa anafanya inapofika siku yake ya kuzaliwa ? Swali, je weww unaafanya kama alivyokuwa anafanya Mtume au unaiga ? Hapa naacha ujihukumu mwenyewe, sababu mambi haya yako wazi sana.
Mimi...naishi kwa kufuata maamrisho na makatazo ya Allah...na kufuata sunna za Mtume...
Sasa hapa kwenye Sunnah, jaribu kujikita zaidi, utapambaukiwa na mengi.
Mengine natumia Common Sense
Yapi hayo ? Naomba unitajie matatu tu.
 
Mimi nilitoa ela ya mboga tu nyingine nikaambiwa nisijali watalipa ata wajukuu zangu

Mahari kubwa haimkomoi mtoaji Bali kwa wapokeaji uwezi niambia nimlipie bint yenu mahari kubwa alafu siku mkipata shida mtegee lolote kutoka kwangu ata hyo nliemlipia mahari sintamruhusu anyanyue mguu aje kwenu siku mkipata shida.
 
Mimi mahari niliyotoa kwa mke mkubwa ilikuwa chini ya Tsh 150,000/- pesa taslimu.

Kauli hiyo yako kwa mujibu wa mada uliyoianzisha bado haijathibitisha kwamba ulioa kwa mahari ndogo, Unaposema Mahari ilikuwa chini ya Tsh 150,000 mtu anaweza kubashiri labda ulioa kwa Tsh 10,000/= au Tsh 2000/= nk, isitoshe utuambie ulioa mwaka gani kwani thamani ya ela inaendana na muda.

Tuambie ulioa kwa mahari ya Tsh ngapi na mwaka gani??--- hapo ndipo tutapima kama kweli ulioa kwa mahari ya ubwete na mada yako itakuwa na mashiko.🤣
 
Kupewa mke bila mahari au mahari Kiduchu ni Mtego mkubwa
Wakati naoa niliomba wazee waende ukweni kwa mzee Macha ili waeleze nia ya kijana wao na kupewa taratibu za mahari.

Kichwani kwangu nilikuwa nawaza hiyo list ya mahari maana mzee alikuwa jeuri na binti amemsomesha. Wazee wakaambiwa njooni mwezi ujao na huyo kijana niwatajie mahari, tulipofika mzee akaita binti yake, Mankaaaaa njoo hapa! Mzee akamuuliza Unamjua huyu kijana? Umempenda mwenyewe? Manka akajibu ndio baba. Mzee akaniambia kijana kama mmependana nawapa baraka mkaishi vizuri hayo Ndio mahari.

Sasa ni Mtego Kwasababu ukweni wakikohoa tu Nimeshafika kwa jinsi ninavyowaheshimu na kuwapenda, yaani niko frontline utadhani mimi mtoto wao wa kiume.
aise nimewapenda Sana hao ,wakwe zako mkuu.kwa maisha na tamaduni za kiafrica ni ngumu Sana ukakuta familia zenye mitizamo Kama ya hao kuhusu mahali.Nina brother angu alioa kwa tsh.700 tu,sema enzi zile wakati sent,sumuni, zilikuwa bado in use.
 
Paula Paul
sherehekea sikukuu yako/yenu vile uwezavyo, hata kama itagharimu fedha ila kikubwa ni kuifurahisha nafsi yako.

nmependa ukimya wako wa kuacha kuendeleza mjadala.
 
Mkuu, Mbwembwe za chochote zinasababishwa na wahusika wa jambo lenyewe
Mkuu Mambo mengi sana uislamu una unafuu sanaa, ila mada iliokuepo ni mahari, ndo maana nimetoa mfano huo tu.....

Tena likija suala la kufiwa achana na waislamu watakuzikia ndg yako hata ukiwa huna shilling 100, waislamu hawana mbwembwe katika masuala ya msingi, kwenye Dini.

Paula Paul
sherehekea sikukuu yako/yenu vile uwezavyo, hata kama itagharimu fedha ila kikubwa ni kuifurahisha nafsi yako.

nmependa ukimya wako wa kuacha kuendeleza mjadala.
Huyu Dada Paula inaonyesha ni msomi aliyeelimika (siyo wale wasome vyeti wa kuongea kiswanglish) maana akikuona huelekea kuwa muelewa anakuacha kama ulivyo (hatakagi ujinga kabisa) kama na nje ya jukwaa yupo hivi basi mumewe amepata mke mwema.
 
Mkuu, Mbwembwe za chochote zinasababishwa na wahusika wa jambo lenyewe

Huyu Dada Paula inaonyesha ni msomi aliyeelimika (siyo wale wasome vyeti wa kuongea kiswanglish) maana akikuona huelekea kuwa muelewa anakuacha kama ulivyo (hatakagi ujinga kabisa) kama na nje ya jukwaa yupo hivi basi mumewe amepata mke mwema.
Umeligundua hilo. Sipendi kuendelea ku-argue na mtu huku nikijua siwezi kubadili mtazamo wake.
Thank you.
 
Back
Top Bottom