Tulioomba kuhamishwa Wodi hali hii ilipotukuta tulipolazwa Mahospitalini tutambuane tafadhali

Tulioomba kuhamishwa Wodi hali hii ilipotukuta tulipolazwa Mahospitalini tutambuane tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mwaka 1994 nililazwa katika Hospitali Moja hivi Jijini Dar es Salaam baada ya Kuteguka Mguu kutokana na Kucheza Ndiki / Mpira / Fabo Shuleni.

Kwa wale Wakongwe Wenzangu mtakumbuka kuwa hiyo miaka ya nyuma Hospitali zetu zilikuwa zinawarundika Wagonjwa wa kila aina kama vile Figo, TB, Bandama, UKIMWI, Kolomero, Kichocho, Kipindupindu, Kisukari ( Fei Toto ) na Njaa Wadi / Wodi moja ila tu kwa Jinsia zenu.

GENTAMYCINE nililazwa katika Wodi yenye Wagonjwa Mseto ( wa kila tatizo ) na nakumbuka nilishuhudia Vifo vya Wagonjwa Wenzangu mfululizo kwa Kufuatana na Vitanda vyetu vilivyopangwa.

Hivyo basi niliingiwa na Uwoga mkubwa na kuhisi / kudhani kuwa akimalizika Kufa Mgonjwa Jirani yangu basi nami nafuatia kwa kutoa Ushirikiano kwa Israeli na Kufa.

Kwa Uwoga mkubwa niliokuwa nao ilinilazimu nitunge Bonge la Uwongo wa Wazazi kuwa Mgonjwa aliyekuwa Jirani yangu ( ambaye nae alikuwa tia maji tia maji ) na kwamba muda Wowote angekata Kamba ( Angekufa ) kuwa alikuwa Amechanganyikiwa na Usiku huwa ananitishia Kuniua na Silali hivyo waniombee ruhusa kwa Madaktari nikajiuguzie Nyumbani.

Kweli Mbinu yangu hii ya Kudanganya ili nitolewe Wodini kwa Kuogopa vile Vifo mfululizo Wodini ilifanya Kazi na hatimaye Kuruhusiwa Kuondoka pale Hospitalini na kurejea Nyumbani Kujiuguza.

Usiombee hali hii ikukute kwani kiukweli huwa inatisha na sijui Madaktari wa Siku hizi huwa wanafanya nini Kuwatia Moyo Wagonjwa walioko Mawodini Mahospitalini ambao Kutwa tu wanashuhudia Wagonjwa Wenzao Wakidondoka / Wakifa ili na Wao wasiwe Waoga / Wanyali kama ilivyokuwa Kwangu GENTAMYCINE mwaka huo wa 1994 ambao najua 60% ya Members hapa bado mlikuwa mnatafakariwa katika Zipu za Baba zenu kama mletwe duniani au mgongeshewe tu Besela ( msizaliwe )

Tuliokumbwa tu na hili tutambuane.
 
Pole sana, waliyobaki nyuma wao hawakutishiwa na mgonjwa...
 
Iliwahi kutokea kwangu pia kwenye hospital kubwa ya umma kinondoni mwaka huohuo wa 1994 nililazwa kwenye ward yenye wagonjwa kibao na kila siku wagonjwa vitanda vya jirani wanakufa, mama yangu alichofanya ni kuniinua kama ananipeleka toilet tukatembea taratibu hadi geti la hospital kufika pale tukakutana na ndugu wamekuja kuniona wakamuuliza mama unampeleka wapi mtoto akawambia watu wanakufa sana nimeamua nimrudishe nyumbani, ndugu walijaribu sana kumshawishi ili nibaki wakaita hadi madokta ila bi mkubwa akakaza akasema mtoto hawezi kurudi ile ward, nikapelekwa home nikaendelea na matibabu nikiwa nyumbani kuna nesi mmoja alikua akiishi mtaani akawa anakuja kunichoma sindano na siku ingine yule dokta akawa anakuja kunicheki hadi nikapona.
 
Back
Top Bottom