Tuliopitia maisha ya boarding njooni tukumbushane moments

Tuliopitia maisha ya boarding njooni tukumbushane moments

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Najua wengi humu tumepitia life la shule za boarding,je ni moment zipi hauwezi kuzisahau hususa boarding za gavo au hata private??

Binafsi nimepitia maisha ya boarding za serikali hapa hapa Tanzania miaka hiyo ya nyuma, ila sio maisha ambayo kivile japo ni boarding la serikali ila maisha yalikuwa ya kishua sana wanafunzi usiku mnakula wali nyama mixer ndizi moja moja, ijumaa biliani, siku nyingine wali nazi.

Pia shule ilikuwa na utaratibu wa kugawa maziwa na chai ya maziwa, babaa ss kuna shule fulani ss ya girls ya serikali walikuja kututetembelea siku moja wakaona jinsi tunavyokula vizuri waliporudi kwao wakashinikiza uongozi wa shule nao wanataka kura vizuri kama sisi wakaambiwa haiwezekani.

Kiukweli kwenye kula watu walikuwa wanakula vizuri ila mazingira mengine hovyo sana, kiasi ambacho mtu ukienda chooni unahacha nguo zako nje ili zisinuke nnya yaani na mambo mengi ya hovyo.

Ila kwa ss nasikia serikali imeboresha sana miundo mbinu hususa vyoo na majengo mengine, sijajua kwny kula kama bado wanakuka biliani na wali ulioungwa na nazi mpaka sasa.

😂😂😂😂😂😂
 
Ukienda chooni Nini !?[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Umenikera hapo unaporudia rudia kusema Kura chakula nikajua umekosea lakin umeendelea kukazana Kura Kura Kura..... andika kula siyo kura
 
Mkuu ni biriani na sio biliani![emoji848] so unakumbuka moment ya kula tu? Ulienda shule kula? Tupe na matokeo yako ya darasani!
 
Ule mchanganyiko wa mwisho wa maharage na vimchanga ulinifanya niwe mzingatiaji wa kengele ya chakula kweli kweli....

dah noma sana...
 
Matukio ambayo huwa siyasahau:-

Kupiga simu chooni

Kata Mkia kwa Njuka

Miezi dume ( hapa uji unaungwa chumvi, sukari inasakwa kwa bluetooth)

Kuibiwa blanket na kaka wakubwa

School Baraza hasa segment ya Lover affairs ( wana wanatajwa pale kwa kadamnasi in pairs)

Siku ya kula wali ni jumapili tu, ole wako ukae nje ya line ( Yule ticha wa jikoni alikuwa nuksi ana jicho kunguru anasubiri)

ole wako uonekane kijijini bila ruhusa tena umelewa ulanzi au kiambule huo moto wake hauzimwi na zima moto, fimbo za kutosha!

Disco la yesu.... mnajimix na girls kiasi fulani kwa masaa tu.

Boarding nuksi tupu, hapo ndipo utajua kama maharage ni mboga au zao la biashara, ilinifanya nichukie maharage na kabichi maisha yangu yote.
 
Mkuu ni biriani na sio biliani![emoji848] so unakumbuka moment ya kula tu? Ulienda shule kula? Tupe na matokeo yako ya darasani!
Kuhusu matokeo usiulize baba ,sijawahi pata karai kwenye vyeti vyangu ni B na A tu.🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom