Tuliopitia maisha ya shida baada ya kufiwa mama zetu tukutane hapa

Village fooler

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2020
Posts
722
Reaction score
1,463
Habari za weekend ndugu zangu poleni na mihangaiko pamoja na hii changamoto ya covid- 19 kama title inavosema
Mimi Ni mhanga wa kufiwa na Mama yangu mzazi nikiwa katika umri wa miaka 11 tu nikiwa darasa la tano.

Kwakweli kati ya vitu vinavyoumiza na bado vinazidi kuniumiza mpaka Leo Ni kitendo cha kufiwa mama yangu nikiwa na umri ule naumia mpaka Leo

Baba yangu alikua na wanawake watano japo hakua na uwezo kifedha lakini alijitahd kila mwanamke akawa amempatia nyenzo ambayo itamsaidia yeye na watoto wake coz kwa watoto alikua nao aliona kabisa hataweza kuwahudumia so ikabidi afanye hvo, katika nyumba yetu tulizaliwa wanne mm nikiwa wa mwisho na tulizaliwa kwa interval nzur tu coz mpaka mama anafariki nikiwa darasa la 5 Dada yangu ninaemfuata alikua tayar ameolewa kiufupi kila mmoja alikua na maisha yake kwahiyo Mimi ndo nlikua naishi na mama.

Siku zikaenda huku msaada Mkubwa ukiwa unatoka kwa mama mzee alikuepo tu kutimiza wajibu lakn mchango wake ulikua mdogo sana katika kuendesha maisha yetu,

Nikiwa darasa la tano ndipo mama alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu taa ya maisha yangu ikawa imezima matumaini yakakata kabisa maisha yakaanza kuyumba nikakomaa na shule mpaka nikafika kidato cha sita bahati mbaya mzee nae akawa amefariki nikiwa kidato cha 5 nikazidi kuchanganyikiwa baada ya kuhitimu form 6 nikakosa mkopo akiba ambayo mama alikua ameacha ikawa haiwezi kutosha mpaka nimalize chuo nikaamua kupiga chini maisha ya shule nikaanza maisha rasmi ya mtaani Leo Ni miaka 7 toka nimeanza maisha Namshukuru Mungu amenisaidia siwezi kukufuru aliponitoa Ni mbali sana yeye Ni muweza wa vyote.

R.I.P mama Leo nimekukumbuka ty ghafla japo Ni miaka Mingi tangu umetangulia mbele za haki Mungu akuangazie raha ya milele natamani ungepewa tena japo dakika moja uamke uone matunda kidogo ambayo mwanao ameyapata kutokana na malezi yako mzuri ila unajua haiwezekani ila najua siku ya ufufua nitakuona tena.
 
Pole Sana mkuu..
Kazi ya Mungu haina makosa,
Yeye aliwachukua wazazi kwa mapenzi yake mwenyewe na Yeye mwenyewe Anajua namna ya kukutunza wewe,usiwe na shaka..
Amini Mungu ni Baba yako, Yeye anasema ni baba wa yatima.
Amini una mzazi ambaye ni Mungu..
Furahi katika Bwana.

Mungu azidi kubariki kazi za mikono yako zikazae matunda moja kwa mia.

Kwa wote mliopoteza mama zetu ,mama yangu ni mama yetu wote.[emoji3590]

Mungu akutunze[emoji120]
 
  • Thanks
Reactions: THT

Ubarikiwe sana mkuu kwa maneno ya faraja uhakika Mungu Ni muweza ameniheshimisha sana na bado anazidi kunipigania
 
Habari za weekend ndugu zangu poleni na mihangaiko pamoja na hii changamoto ya covid- 19 kama title inavosema
Mimi Ni mhanga wa kufiwa na Mama yangu mzazi nikiwa katika umri wa miaka 11 tu nikiwa darasa la tano.
Kwakweli kati ya vitu vinavyoumiza na bado vinazidi kuniumiza mpaka Leo Ni kitendo cha kufiwa mama yangu nikiwa na umri ule naumia mpaka Leo
Baba yangu alikua na wanawake watano japo hakua na uwezo kifedha lakini alijitahd kila mwanamke akawa amempatia nyenzo ambayo itamsaidia yeye na watoto wake coz kwa watoto alikua nao aliona kabisa hataweza kuwahudumia so ikabidi afanye hvo, katika nyumba yetu tulizaliwa wanne mm nikiwa wa mwisho na tulizaliwa kwa interval nzur tu coz mpaka mama anafariki nikiwa darasa la 5 Dada yangu ninaemfuata alikua tayar ameolewa kiufupi kila mmoja alikua na maisha yake kwahiyo Mimi ndo nlikua naishi na mama.
Siku zikaenda huku msaada Mkubwa ukiwa unatoka kwa mama mzee alikuepo tu kutimiza wajibu lakn mchango wake ulikua mdogo sana katika kuendesha maisha yetu,
Nikiwa darasa la tano ndipo mama alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu taa ya maisha yangu ikawa imezima matumaini yakakata kabisa maisha yakaanza kuyumba nikakomaa na shule mpaka nikafika kidato cha sita bahati mbaya mzee nae akawa amefariki nikiwa kidato cha 5 nikazidi kuchanganyikiwa baada ya kuhitimu form 6 nikakosa mkopo akiba ambayo mama alikua ameacha ikawa haiwezi kutosha mpaka nimalize chuo nikaamua kupiga chini maisha ya shule nikaanza maisha rasmi ya mtaani Leo Ni miaka 7 toka nimeanza maisha Namshukuru Mungu amenisaidia siwezi kukufuru aliponitoa Ni mbali sana yeye Ni muweza wa vyote.
R.I.P mama Leo nimekukumbuka ty ghafla japo Ni miaka Mingi tangu umetangulia mbele za haki Mungu akuangazie raha ya milele natamani ungepewa tena japo dakika moja uamke uone matunda kidogo ambayo mwanao ameyapata kutokana na malezi yako mzuri ila unajua haiwezekani ila najua siku ya ufufua nitakuona tena.
Mungu awape ujasiri wale wote waliofiwa na wazazi wao hasa waliofiwa na wazazi wakiwa bado wadogo

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom