DOKEZO Tuliosimamia mitihani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hatujalipwa kwa kisingizio cha chuo kukosa pesa

DOKEZO Tuliosimamia mitihani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hatujalipwa kwa kisingizio cha chuo kukosa pesa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari, mimi na wenzangu kadhaa ni mwanafunzi wa shahada za juu shule kuu ya elimu UDSM.

Tulisimamia mitihani ya chuo (UE) ya kufunga muhula wa kwanza 2023/24 baada ya Ndaki ya Sayansi za jamii (College of Social sciences) kutangaza kuomba wanafunzi wa postgraduate kusaidia kusimamia mitihani hiyo kutokana na uhaba wa wafanyakazi wa kudumu.

Tangu mwezi wa pili 2024 hadi sasa chuo hakijatulipa ujira wetu kwa kisingizio kuwa hakuna fedha licha ya kwamba wanafunzi wanalipa ada na shughuli nyingine za chuo zinazohitaji fedha zinaendelea.

Ujumbe huu pia unaweza ukawa unawakilisha wafanyakazi na wanafunzi wengine ambao wanadai fedha kutokana na shughuli mbalimbali.

Ni/tunaamini ujumbe huu utasaidie mamlaka husika na wadau kusaidia kutatua kero hii ambayo imekuwa sugu kwa makundi mbalimbali UDSM.

Asanteni
 
Kufanya kazi na taasisi za serikali kwa ahad yataka moyo .
 
Mkome tu,

Vipi hua mna ona fahari sana kusumbua watu kupata PhD Hadi waende mahakamani.
 
Wasomi wa siku hizi bure kabisa,badala ya kudai haki zenu uko uko,unakuja kufungua Uzi JF,iliiweje ?

Chuo kimejaa chawa tu.
 
Back
Top Bottom