NILIKUWA PALE 1987-89 PCB1, TOSAMAGANGA NI MOJA YA SHULE YENYE NA SIFA YA AINA YAKE KIELIMU NA KINIDHAMU ENZI HIZO, NAMKUMBUKA MWALIMU KASANDA ALIKUWA BALAA KWA FIZIKIA, MIDADI IKIMPANDA ANATUMIA LAB KOTI YAKE KUFUTA UBAO (Alikuwa ni mtaalamu kwelikweli yeye na warusi akina Verichko na Terminov) Kulikuwa na mtaalamu wa Biolojia Mwalimu Kisenime alikuwa -Classification, biochemistry....) Kulikuwa na warussia mume na mkewe Verichko walikuwa wakali sana kwa chemistry, pia na mrusia mwingine alikuwa anaitwa Shabunin. Namkumbuka mwalimu mmoja alitupokea pale anaitwa Mwakabanje...alitutisha sana tulipoingia....Alikuwa ametayarisha reagents lab ameandika instruction ubaoni... Tulipoingia Lab tutasubiri maelekezo.... Akatuuliza kwanini tumeduwaa, ni kweli sisi tumefaulu kusoma pale Tosamaganga ama ni watalii...Alikuwa serious sana yule mwalimu... Bush politician - MKINGA na Mwalimu Chitinde, Mwl Mahenge, Ila kulikuwa na Mwl anaitwa Mgunya alikuwa Noma sana yule Bounsa.... Namkumbuka headmaster Mpogole AKA DUDU alikuwa anasimamia sana suala la elimu, Yeye alikuwa anataka kukuona wakati wote una kijitabu ama karatasi unasoma hata akikukuta Ipamba ukatoa kakijitabu na kujifanya unasoma anakuacha.... Ila kuna time alikuwa anakumezea na ukiona mmeitwa assembly basi ujue kuna wanafunzi anawatafuta either aliwakuta town, ama ipamba, ama njia panda kule mseke, ama kwenye ulanzi huko Msukanzi maana alikuwa na kumbukumbu nzuri sana. Pamoja na mengine yote namshukuru sana MUNGU kusoma pale mbali na matatizo ya kunya uji usio na sukari - Sifongo, Lakini ELIMU YA PALE ILIKUWA KIBOKO....