Tuliosoma Shule ya Sekondari Tosamaganga tukutane hapa

Waoooo, mmenikumbusha mbali sana mambo ya TOSA, namkumbuka mwalimu mmoja wa O level alikuwa anaitwa baba hamphrey.. aliikuwa mzuri sana wa hesabu , lakini kila anapojaribu kufanya mtihani wa A-level PCM ili ajieendeze alikuwa anapata A ya maths na mengine anafeli, alikuwa anapenda sifa saana. ati kwa kuwa yy anafundisha maths O-level na mkewe maths primary kwahiyo akawa anasema mwanae hamphrey atakuwa hatari zaidi kwa maths. sijui hamphrey aliendeleaje kwa ndotonhiii!...yeah, thse days of half mile, sinagogi.. pale jamaa wanakesha kusali daily!
 
Mugasa! haahhahaaa, I know this man, siku hizi busara kibao!! kumbe alipita huko??

 

phew! anagalau umenipa moyo kidogo, manake nilishaanza kujiona "ancient" fulani hivi manake mi nilipita hapo tosa
1979-1981. nikawa nasita hata kuchangia lol.

sisi pia tulimpoteza mwnafunzi mwenzetu (r.i.p.) yeye alizama kwenye ule mto lupalama (kama sikosei). mwili wake ulipatikana baada ya siku kadhaa ukiwa umeharibika ikabidi azikwe makaburi ya hapo hapo tosa. mshikaji alitumbukia
mtoni wakati akivuka akitokea kupiga kinywaji na washikaji aliokuwa nao hawakutoa taarifa shule kisa wanamuogopa dudu (r.i.p). hata wakati juhudi za kumtafuta mshikaji vijijini wao walibana kimya hadi pale shati la marehemu lilipookotwa pembezoni mwa mto na wanakijiji ndipo juhudi za utafutaji ukahamia mtoni. it was so sad, dah!

hata hivyo tosa ina mengi mazuri ya kukumbuka na kufurahia. hata sisi tulikuwa tunazuka ipamba bana lol
 
I was there A' level 1984 - 86, duuuuuuuuuu inanikumbusha mbali HeadMaster Dudu Second Master bwana mmoja mchaga aliyekuja kuwa HeadMaster Azania


una maana mwl. kwayu? sisi walikuwapo pia akina mwakabanje, charles na bwana mmoja alikuwa rafiki sana wa charles
na alikuwa anacheza mpira pia (nimemsahau jina).
 
Namkumbuka Msalilwa, Mponzi, Mkangwa, Mdalingwa, Makini, Miss Perry, bila kumsahahu Fyudo, yaani we acha tu ndani ya 1999.

Enzi za Marehemu Mpogole "DUDU"

M


Madella Annex



Mabweni Ya Azimio na Mwenge



Madarasa ya Form V PCB na PCM



Madarasa ya Form 6 EGM na CBG




Uwanja wa Basketi picha hii imepigwa kwa juu kule Mandella Annex
 
kwanini hii shule isiwe chuo kikuu?
 
KWELI KABISA, Nilitaka kuandika hivi hivi, mpigaji alikuwa kasimama karibu na shule ya Msukanzi kama sikosei. na Idete shambani ndio lilikuwa eneo salama. mnakumbuka kipindi cha mapera idete na siafu?
Tosa, was always the best place those days!
 
Vitu vya Wagalitia huwa ni Makini sana.
Yaani serikali isingetaifisha Shule hizi wangekuwa mbali zaidi.
Mnaweza kuweka na Madrasa zilizotaifishwa tuzijue?

From 1880s to 1919 Tanganyika was under Germany rule, then after that to 1961 we were under the British mandate- ungelikuwa ni mtu makini japo kidogo ungegundua kuwa hao unaowaita wagalatia makini ndio walioiongoza hii nchi kwa miaka nenda rudi, na kwa sababu ya 'umakini' wao hawakuangaika kujenga hizo Madrasa zilizotaifishwa ambazo leo unataka tukuonyeshe
 
napenda ule wimbo wa shule hasa ukiongozwa na kile kikundi cha skauti. (advance 2001/2003)
 
Hayaaaa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Hujaenda kukosha kwa masista
 
NILIKUWA PALE 1987-89 PCB1, TOSAMAGANGA NI MOJA YA SHULE YENYE NA SIFA YA AINA YAKE KIELIMU NA KINIDHAMU ENZI HIZO, NAMKUMBUKA MWALIMU KASANDA ALIKUWA BALAA KWA FIZIKIA, MIDADI IKIMPANDA ANATUMIA LAB KOTI YAKE KUFUTA UBAO (Alikuwa ni mtaalamu kwelikweli yeye na warusi akina Verichko na Terminov) Kulikuwa na mtaalamu wa Biolojia Mwalimu Kisenime mambo ya -Classification, biochemistry....) Kulikuwa na warussia mume na mkewe Silvanorvich walikuwa wakali sana kwa chemistry, pia na mrusia mwingine alikuwa anaitwa Shabunin. Namkumbuka mwalimu mmoja alitupokea pale anaitwa Mwakabanje...alitutisha sana tulipoingia....Alikuwa ametayarisha reagents lab ameandika instruction ubaoni... Tulipoingia Lab tutasubiri maelekezo.... Akatuuliza kwanini tumeduwaa, ni kweli sisi tumefaulu kusoma pale Tosamaganga ama ni watalii...Alikuwa serious sana yule mwalimu... Bush politician - MKINGA na Mwalimu Chitinde, Mwl Mahenge, Ila kulikuwa na Mwl anaitwa Mgunya alikuwa Noma sana yule Bounsa.... Namkumbuka headmaster Mpogole AKA DUDU alikuwa anasimamia sana suala la elimu, Yeye alikuwa anataka kukuona wakati wote una kijitabu ama karatasi unasoma hata akikukuta Ipamba ukatoa kakijitabu na kujifanya unasoma ana kusamehe kama una kosa.... Ila kuna time alikuwa anakumezea na ukiona mmeitwa assembly basi ujue kuna wanafunzi anawatafuta either aliwakuta town, ama ipamba, ama njia panda kule mseke, ama kwenye ulanzi huko Msukanzi maana alikuwa na kumbukumbu nzuri sana. Pamoja na mengine yote namshukuru sana MUNGU kusoma pale mbali na matatizo ya kunywa uji usio na sukari - al maarufu Sifongo, Lakini ELIMU YA PALE ENZI HIZO ILIKUWA KIBOKO....
 
Ninavyo jua, Tosamaganga ni Rusha mawe..... wamissionary walipoomba eneo wajenge, wakapewa hapo kilimani, wakaanza kupasua mawe kwa baruti, yakwa yanaruka , ndio wahehe wakwa wanashanga.... he! he ! hitosamaganga, yaani anarusha mawe!

 
duh safi sana umenikumbusha mbali sana niliwahi kufundisha kwa muda hapo. nakumbuka kuna kesi fulani mwanafunzi wa form six alitoroka kuja dar kutafuta "feki" halafu mwenzie alikua anamuitikia rollcal km kawaida ikatokea bahati mbaya akiwa kwenye daladala huku dar majambazi yalikuwa yanapora mahali wakarusha risasi hewani ikampata akiwa kwny daladala akafa mmmh msala huo ulinikuta mm nikiwa mwl wa zamu!! kaaaazi kweli.
 
Mkuu umemsahau dikteta Mavika.

Usinikumbushe ule mchakamchaka wa saa 11 alfajiri. Wakati ndiyo nimejiunga tu na kidato cha tano, basi kutokana na kile kibaridi cha katikati ya mwaka si nikapitisha muda wakuamka. Basi tukadakwa na Mavika bwana. Adhabu kama kawa ilikuwa ni kulala mbele ya ofisi mpaka saa nne asubuhi.

Basi ukiwa pale inabidi ujifunike gubi gubi O-level wasikuone wakati wa Morning parade. Umenikumbusha mbali sana hasa zile zamu za kuchunga ng'ombe tulikuwa tunapiga Ulanzi kama hatuna akili nzuri kijijini.

HAHAHAHAHAHAHAAAAA JF I will never leave you alone.
 
Mkuu enzi hizo ukichaguliwa kujiunga pale mtaani unaagwa kwa sherehe. Chezea special School wewe. Mkuu hiyo sifongo umenikumbusha mbali sana, chumvi yenyewe ukitaka kuweka ni ya mawe mpaka usage. Dona na maharage daily mboga mboga zinauzwa na mabeki tatu wa walimu pale jikoni kwa chini, nyuma ya bwalo kwa wenye uwezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…