Tuliosoma St. Kayumba unakumbuka haya?

Tuliosoma St. Kayumba unakumbuka haya?

Tuliosoma kijijini hata wakimbizi wana nafuu, kwa siku moja unatumwa kuni, mbolea, kopo la maji, fagio, jembe, mfuko wako wa rambo wa daftari yani ukimwona mwanafunzi kwa mbali mkimbizi chamtoto.
Mie sijasoma Kijijini but enzi hizo shule za mjini nazo ilikuwa kama Kijijini tu, matangazo ya mwl wa zamu, kesho mtakuja na maji, mfagio, mbolea, jembe, maua, jiwe hapo bado mfuko wako wa daftari na bado unatakiwa uwahi namba, kweli tumetoka mbali.
Siku ya kupika sayansi kimu, mnabeba kuni, sahani utayotumia kulia chakula
 
Kuna hii mkuu siku husipohesabu namba mwl anachapa ukihesabu hachapi dha ninoma
 
Mie sijasoma Kijijini but enzi hizo shule za mjini nazo ilikuwa kama Kijijini tu, matangazo ya mwl wa zamu, kesho mtakuja na maji, mfagio, mbolea, jembe, maua, jiwe hapo bado mfuko wako wa daftari na bado unatakiwa uwahi namba, kweli tumetoka mbali.
Siku ya kupika sayansi kimu, mnabeba kuni, sahani utayotumia kulia chakula
Sio tumetoka mbali, haya mambo bado yapo ktk shule nyingi vijijini. Ila nimejiapiza, watoto wangu hawatosoma shule hizo ni bora nibebe bunduki nikaibe.
 
Sio tumetoka mbali, haya mambo bado yapo ktk shule nyingi vijijini. Ila nimejiapiza, watoto wangu hawatosoma shule hizo ni bora nibebe bunduki nikaibe.
Tehtehteh, watoto wa siku hizi wana raha, basi la shule linamfuata hadi getini
Enzi zetu ilikuwa muziki, saa sita na nusu unarudi home kwenda kula unakuta hakuna msosi, unaambulia kunywa maji tu unasepa na jembe lako begani tayari kabisa kwa EK
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] umenikumbusha mbali sana na yote nimepitia
 
Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na haya...

1. Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani
2. Unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio
3. Mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban
4. MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule)
5. MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona sa nne"
6. Wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao
7. Ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika
8. Unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki
9. Vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba
10. Hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule au mwalim hayupo
11. Habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa
12. Mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake
13. Usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule
14. Unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peni
15. Ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati
16. Siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na maji wanakagua kuni au mbolea

Dah shule zetu hizi!!

Ipi umeipitia wewe

Umesahau kuhesabu namba asubuhi kama umewahi,,inapofika muda wa kutoa kibano kwa wachelewaji mwalimu akiita aliyehesabu namba moja watatoka watu kibao kila mtu atang'ang'ania kwamba ni ya kwake.....
 
Kuna siku nilimvizia kaka Mkuu yuko uwanjani anacheza mpira nikaingia darani hakukuwa na mtu nikachana madaftari yake yote katikati. Nilikuwa na hasira nae aliniabisha mbele ya mademu kwakuwa mi kimbaumbau siwezi kumpiga. La sita hapo
 
Tuliosoma kijijini hata wakimbizi wana nafuu, kwa siku moja unatumwa kuni, mbolea, kopo la maji, fagio, jembe, mfuko wako wa rambo wa daftari yani ukimwona mwanafunzi kwa mbali mkimbizi chamtoto.
Ha ha haaa t
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha... Nimecheka sana
 
Nimetoboa watu na bikari sana ,na kioo changu spesho wakati wa paredi ,nimeona sana vyupi vilivyotoboka dah
Hahahahahah, huo mchezo wa kumulikwa na vioo tulifanyiwa kipindi flani skuli, tukawasemea kwa mwalimu wakala kichapo cha mbwa mwizi...

Isije tu ikawa wewe ni mmojawapo UncleBen
 
Hahahahahah, huo mchezo wa kumulikwa na vioo tulifanyiwa kipindi flani skuli, tukawasemea kwa mwalimu wakala kichapo cha mbwa mwizi...

Isije tu ikawa wewe ni mmojawapo UncleBen
Hahahahaha aiseee nilikua na degree ya chabo sikuwahi shitakiwa kwa hilo swala

Halafu kuna nyigine nilikua natembea na lensi sasa jua likiwaka naweka juu ya utosi wa mtu aloo inachoma ile
 
Mwalimu akiwa na mimba visirani vyake vyote anakuja kuwatolea uvivu wanafunzi.

Mnaomba Mungu akizaa hilo litoto lake life...
 
Hahahahaha aiseee nilikua na degree ya chabo sikuwahi shitakiwa kwa hilo swala

Halafu kuna nyigine nilikua natembea na lensi sasa jua likiwaka naweka juu ya utosi wa mtu aloo inachoma ile
Ha ha ha ha ha haaa,ulikuwa na vituko aisee, UncleBen utoto una mengi sana,ya kuchekesha na ya kusikitisha.
 
Ha ha ha ha ha haaa,ulikuwa na vituko aisee, UncleBen utoto una mengi sana,ya kuchekesha na ya kusikitisha.
Hahaha dah kuna wakati natamani ningerudi kwenye miaka 12 hivi ,vioja vyangu vingi vilianza na miaka 12 ,nishapiga paka alikula njiwa wangu ,niliua halafu nikamchuna ,kuona haitoshi bado nikaning'iniza kichwa chake chumbani kwa siku tatu ,hee bi mkubwa anashangaa harufu kuja kushuhudia aisee aliogopa kuanzia hapo akajua huyu jamaa ana hasira mbaya ,tuachane na habari hizi tunajaza uzi wa watu bure
 
Back
Top Bottom