Tuliosoma St. Kayumba unakumbuka haya?

Likizo ukinunuliwa sare mpya unataman shule ifunguliwe wiki hiyo hiyo unaona cku hazisogei kabisa ukalingishie
 
uki nunuliwa daftari inakuwa na kurasa 45 siku zinavyoenda inakuja kubaki na kurasa 12 tu zingine umezichana zimebaki pages zenye vema tu.......kimbembe kinakuja nyumbani ukiomba daftari jipya wanakwambia uwaonyeshe daftari lililo isha! ndiyo balaa inaanzia hapo.
 
daah iyo ya kifutio cha ndala imenikumbusha far kinoma

darasa la tatu tunaanza kutumia pen baada ya pencil bas eti ukikosea kuandika unaforce kufuta na ndala mixer mate... yan nomaaa
 
Kuwahi school bus, ilikua inanisumbua sana
 
Sitosahau tulipewa heka mbili tupande karanga zimepakwa unga ati dawa tusile hata sijui wanafunzi walipata wapi mahindi na tumesimamiwa na walimu, tukala karanga zote tukapanda mahindi mwalim mkuu alipokwenda shamba akakuta mahindi yameota shamba zima na vikaranga kwa mbaali kengele iligongwa tukaambiwa la tano nendeni shamba kila mmoja asimame kwenye tuta lake ilibidi tusimame pembeni maana hakuna tuta la karanga, mkuu akatuangalia akasema rudini darasani
 
Mi namba 7 imewahi kunitokea[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Amesahau kwa tuliosoma shule za Kayumba mjini eti hela ya nauli shilingi kumi unaificha ktk kiatu chako ili usiile
 
Mimi nilikuaga naogopaga fimbo balaa sasa zile kapeti za viatu nilikuaga nachukua kapeti moja nailaza tako la kulia na lingine tako la kushoto ili fimbo nikipigwa sisikii
 
Mambo ya shule ya msingi bwana, tulikuwa tunapenda kushindana idadi ya "tiki"na "vema" kwenye madaftari
 
Hii ilinipa fimbo 3 za moto mstarini, chini ya bendera shule nzima ikishuhudia. Mbolea sikuwa nayo nkajaza udongo mweusi na mbolea kidogo juu, watu walipigwa na kuambiwa waige mfano wangu wa kutii na kuja na mbolea nyingi... Tulipoenda kumwaga kuna bwe.ge aliniona akamwambia mwl mkuu, sitamsahau yule bwe.ge wala mwl mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…