Tuliowahi kudanganya tukutane hapa

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Kudanganya au kusema uongo ni kitu cha kawaida sana kwa jamii zetu. Wengine imekua ndio maisha yao.

Lakini kuna uongo mwingine ukiusikia lazima uzimie[emoji1787]

Kuna watu utadhani wana vipaji vya uongo.

Mimi pia niliwahi danganya wakati bado mtoto. Nilibugia maziwa ya unga..

Bi mkubwa ananiuliza nani kabugia maziwa .. nikamwambia kwanza ndio narudi muda huu. Kumbe mdomo sijaufuta vizuri vumbi la maziwa limebakia mdomoni.

Sitaisahau siku ile , nilikuja zinduka nipo zahanati mapaja utadhani yamechomwa moto .[emoji23]


Je, umewahi danganya mke, mchumba, bi mkubwa etc na nini yalikuwa matokeo yake.?
 

Sasa huyo 'bi mkubwa' alikuumiza kwa ajili ya nini wakati maziwa yanafaida mwilini? Au yalikuwa ni ya mdogo wako mdogo ambaye bado alikuwa ananyonya?
Kuna wazazi wengine wangenunua kopo kubwa na kukuambia ulambe mpaka umalize.
 
Sasa huyo 'bi mkubwa' alikuumiza kwa ajili ya nini wakati maziwa yanafaida mwilini? Au yalikuwa ni ya mdogo wako mdogo ambaye bado alikuwa ananyonya?
Kuna wazazi wengine wangenunua kopo kubwa na kukuambia ulambe mpaka umalize.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nadhani ningemwambia ukweli angeniacha.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nadhani ningemwambia ukweli angeniacha.
Hupo sahihi, na angekuambia siku nyingine usirudie au uombe?
Hilo pia lilikuwa ni somo, kwani ukiiba kazini unaishia jela badala ya zahanati.
 
Asilimia kubwa ya waliopitia JKT kwa mujibu wa sheria wakati mafunzo yalikuwa mwaka mmoja kabla ya kuwa miezi sita na kusitishwa kwa muda wamedanganya sana tu?
 
Ngoja nikumbuke...

Nilidanganya tunabaki shule kwa ajili ya michezo, kumbe nilienda kuogelea alafu ilikua kipindi cha baridi kali barafu zinaanguka nje...nikarudi usiku mwingi sana...

Kurudi sikuchapwa, ila niligombezwa sana, nikafungiwa kufanya kila kitu na hakuna kutoka nje week nzima, ni ndani shule, shule ndani... niliteseka sana...



Cc: mahondaw
 
Nilimdanganya simpendi pale aliponitamkia ananipenda na alinipenda sanaa akuweza kuvumilia anikose ili mradi tu awe na aolewe na rafiki angu niliamini atakuwa kweny mikono salama sababu rafki angu ana uwezo wa kumpa maisha mema na bora kuliko mimi ambae nlkuwa apeche alolo wakati huo na isitoshe alikuwa akimpenda sana kwa hyo kumuona na furaha ila inatosha kwangu

Hivo nikadanganya Mimi muhuni naaigiza nimelewa mchana nimeshika chupa ya safari lager ambayo sijanywa Mimi natukana watu mara nashinda kweny vijiwe vya pusha ananiona natembea na wasichana tofauti nimesimama nao akiamini wa kwangu kumbe nilikuwa nawapanga tu.,sijibu sipokei text na simu zake nlkuwa mwanzo kampani kubwa ilikuwa yeye na rfk angu maana wote tulikuwa marafiki nilijitenga nao baadae rfk angu akawa kampani yake kubwa at the end of time aka win moyo wake akamuoa

Nilipata mwaliko kutoka kwa rafiki angu yeye hakuwa na ujasiri wa kunialika ila skuenda nlishinda maskani wahuni waliambia vuta hii uondoe mawazo maana waliniona nina huzuni japo ukwel nishawah kujaribu kuvuta kitambo yan kuonya lakini apo ndo kulinifanya nianze kuvuta rasmi na kuanza ujinga. Kesho yake na kibegi changu nikapotelea zangu huku nyuma walinitafuta wakanikosa rafiki yangu anajua mpaka Leo Mimi muhuni ,bangi nyingi nadanganya binti za watu mm womanizer japo kwa asilimia chache yupo sahihi ila ajui chanzo ni nini ila bibie alikuja kuambiwa na moja ya wadada tuliokuwa tukiigiza tunatoka wote alkuwa rfki ake sjui alikuwa ananionea huruma ? Au mdomo wake mrefu ulikuwa unamuasha au alitaka kutoka kweny hio zambi ya uongo tulioshiriki? Yule binti alivunja urafiki na huyo rafiki ake baada ya kuambiwa ukwel na anamchukia mwenzake kwa alichofanya na mwenzake ananilaumu mm nimesababisha kuvunjika kwa urafiki wake ila sjui ananilaumu nn maana skumtuma aseme .bora mama mwenye ndoa ajui nilipo na rfki pia ambae ndo nina mawasiliano nae ata rfk angu ajui siwez jua atanifanya nn akiniona maana alimwambie rfk ake nimemkatili Sana

Uongo baya haijalishi unamdanganya Nani au kipi unadanganyia uongo utakupa ushindi wa siku moja ila una hasara kubwa baadae

Ila haimaanishi nitaacha kudanganya kwa sasa. sina tena cha kupoteza
 
Nilipokua Mdogo Anko aliniambia Dunia Inazunguka Na Usiku Tukilala Wa Ughaibuni wanakuja Huku na Sisi Tunaenda Kule Asubuhi Tunarudi Kama Kawaida.

Nilikua Nawadanganya Saana Masela Enzi Hizo mambo ya Mitandao Hayajavuma nikiona kitu Naongeza Na Chumvii.
 
Mwenzio huyu hapa
 
Asilimia kubwa ya waliopitia JKT kwa mujibu wa sheria wakati mafunzo yalikuwa mwaka mmoja kabla ya kuwa miezi sita na kusitishwa kwa muda wamedanganya sana tu?

Una “ridanganya ri afande Mwita” kuwa wewe ni selule ili usinyakue kuelekea usawa wa gudulia? [emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…