funzadume
JF-Expert Member
- Jan 28, 2010
- 13,624
- 21,362
Kama kichwa cha habari kinavyosema. Enzi zile tunasoma kulikuwa na list ya wakali wa masomo darasani (kumi bora)ambayo ilikuwa official na pia kulikuwa na list ya wababe katika kupigana kuanzia wa kwanza mpk wa mwisho.
Sasa mie nilikuwa mkali sana darasani ila kwenye kupigana nilikuwa kama wa tano wa mwisho hivi so kuna jamaa mmoja alikuwa nae wa mwisho mwisho akataka kupigana na mie ili apande kwenye chat ya ngumi na pambano likapangwa siku ya kufunga shule
Jamaa alikuwa mfupi kuliko mimi so nilikuwa nina uhakika wa ushindi. Siku hiyo shule ilipofungwa pambano likapangwa uwanja wa mpira na darasa zima walikuwepo. Mchezo ulianza vizuri na niliutumia urefu wangu vizuri nikawa ninampa nakozi za kutosha sasa kuna kipindi nikawa naona naelekea kushinda nikawa napigana style ya Mohamed Ali ile ya kuruka ruka kwa mguu mmoja (wahenga mtakuwa mnaikumbuka hii) kumbe yule mpinzania wangu alikuwa ananilia timing.
Jamaa alinitisha kama ananipiga kwa kushota nilipokwepa alinipa konde moja la paji la uso na kulia niliona nyota kama 100 hivi usoni na wakati natafakari jamaa alinirukia kichwa kimoja cha usawa wa mdomoni na nikajing'ata ulimi na kutoka na damu balaa, wakati nikiwa nimevurugwa jamaa alinipiga mtama mmoja mkali nikadondoka kama gunia.
Ilikuwa bahatu yangu maana jamaa alinidhibiti kwa juu lakini wataalam wakaamulia na kusema zipigwe za juu juu ili tupate mshindi
Tuliposimama huku damu zikinivuja mdomoni kama teja anavyotokwa mate nilicheki watu waliotuzunguka nikaona upenyo mmoja nikatoka baruti kama Juma Ikangaa unaambiwa darasa zima likaanza kunikimbiza huku wakinizomea mpk demu wangu wa utotoni (Pili) nae alikuwepo ktk watu waliokuwa wananizomea na kunikimbiza. Nilitimkia ofisi ya mwalimu mkuu ndipo nilipookokea hapo