Tuliowahi kudundwa siku ya kufunga shule primary tukutane hapa

Tuliowahi kudundwa siku ya kufunga shule primary tukutane hapa

Miaka hiyo ya mbali mtoto wa mwalimu anaheshimika na kuogopwa kweli.

Akatumia hiyo mbeleko ya utoto wa mwalimu kunirukia juu ya goti wakati mpira naukokotea kwenye unyayo,nikavumilia(kumbuka hapo kumchezea rafu mtoto wa mwalimu ni kama kosa la jinai) nikamsubiria auchukue mpira ili nimlipizie kisasi maana sikukubali lile lipite bure.

Nilimrukia kwenye kifundo cha mguu,alipoanguka akaulania ule mpira tumboni,nikasema hapahapa ndo pazuri,nilimtandika mateke ya tumbo(harakati za kuutoa mpira) akainuka amejaa.

Akitumia utoto wa mwalimu akadhani akinigusa nitamuogopa mama yake,si akanirushia ngumi ya uso,hapo ndio akawa amenipa upenyo wa kumuonesha siogopi utoto wake wa mwalimu. Nilimsukumia ngumi mbili za mdomo(mnajua tena mdomo ukipigwa ngumi unakuwaje) akakaa chini hapo nakampiga mateke ya hapa na pale, wakawa wameshakuja kusawazisha mambo.

Luke utakoma!! Umempiga mtoto wa mwalimu.

Uzuri mwalimu mkuu alikuwa upande wangu baada ya kuona mwenye mtoto anataka kunipa adhabu kwa hisia za uzazi.
 
Enzi hizo ukitaka uwe vizuri inabidi akili zichaji na mpira uwe unaujua,hutasumbuliwa maanake unafit groups zote. Kuna wale manunda shule zero ila mpira balaa hawa utaelewana nao kwasababu ya mpira. Kuna wale watoto wa mama john visomo hawajui mpira so utaelewana nao kwenye masomo! Enzi zangu nilikuwa naombwa nibaki kucheza mechi za madarasa.
Wewe ulikuwa kundi gani kati ya hayo uliyoyataja?
 
Kuna mwalim alikua Kijana Mdogo Mdogo siku ya kufunga shule wanafunzi wakawa wanamvizia basi kila akiingia Darasan kikundi cha wanafunzi wanaenda Nje wanajificha chini ya dirisha Na kuanza kumuimbia "Yassin makamasi, yassin makamasi" halaf wanakimbia...alipowadaka walipigana Makonde..

Nikiwa form1 feza nikitokea St kayumba..aisee nilikula kibano cha mbwa koko toka Kwa jamaa anaitwa Steve, alikua boonge halaf mm njiti dahh sitomsahau Yule umaga !
 
Kuna mkaka nakumbuka tukiwa standard 5 tumeenda uwanjani kwenye mazoezi akanipigia mpira nilimdunda mpaka akazimia ile wanampandisha kwenye school bus akazinduka ikabidi baba aitwee shuleee nilichezea vitasa sitakaaa nisahau kabisaaaaa
Duh! Kumbe Kuna watu watata humu eeh, nilikua mpole nilijaribu mapambano mawili, nikawa na near - miss kwenye mapambano, nikahairisha kuwa mgomvi!
 
Kuna jamaa mmoja alinipiga teke moja la tumbo dah nilidondoka chini na ngumi zikaishia hapo.
Kesho yake shuleni nikawa nataniwa tu,dogo mmoja wa darasa la chini yangu akasema anaweza kunibonda baada ya kusikia nilipigwa(tulikua tunaamini aliyechini ya darasa lako hawezi kukupiga)
Sasa ilikua siku ya kufunga shule hapo battle ilkua ni uwakilishi wa darasa,nlivaa six/njumu siku hiyo aise nilimdondosha chini faster nilimpiga mateke mengi sana usoni,siku ya kufungua shule nilipataga heshima
 
Nlipigwa na katoto kana ngumi nzito ngumu kama mawe, sitaki kumbuka kabisa
 
Back
Top Bottom