Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Ni machungu sana, nayakumbuka, niliyoyapitia, ila ulifanya harakavkuandika barua ya kuacha ungesubiri wao ndo wakuteme.
Hii ndo njia pekee itakayoweka salama kimaisha ya kama unategemea kuwa mwaajiriwa tena,resignation ni nzuri kuliko kufukuzwa ni sawa kuna mafao utayakosa but still unajitengenezea njia bora ya kuajiriwa tena bila CV yako kuchafuliwa na vukuzwavukuzwa.Mimi nimepitia njia hii nadhani ningelikuwa nimefukuzwa huko nilikotoka nadhani nisengelikuwa ajirani tena
 
pole sana
 
Nilivyo sipendi Dharau nimeshaacha kazi kwenye kampuni zaidi ya 3 na zote ni figisu za wafanyakazi wenzangu kazi ya mwisho Nilimtukana mpaka bosi wangu maana alikuwa hajitambui anapelekeshwa na Vilaza wenzake Miaka miwili baadae nimerudi Nimekuta
Wafanyakazi wote wamehama na kampuni Imefilisika!
 
Ulirudi kwenda kufanya nn?
 
Hivi serikalini unaweza fukuzws kazi kweli , je ikitokea taasisi ulifanyia kazi ikafutwa kisheria inakuwaje?
 
Nipe hiyo elimu aisee
 
@@kiteitei Hongera sana
Kiteitei hongera sana.
 
Ila Afika Bhana

Yaani hakuna tunachokifanya kikaenda smooth. Kiukweli tunahitaji kubadilika sana

Just imagine; unaajiriwa ila boss anakutreat kama mnyama vile.... au from nowhere anakuchukia tu ili mradi kazi ikushinde😁😁
Kuna maboss huwa wanahisi watakuwa on pick siku zote especially sekta Binafsi mfano kwenye ma NGO iwe local au International,huwa wanafikiria siku zote utakuwa chini hutainuka siku moja uwe kama wao au kuwazidi,hawafikirii kuna leo na kesho unamkuta uliyemdharau ni somebody somewhere anaweza mfanyia interview hata mwanae..ila maisha haya boss anaaamua tu kukuondoa kazini bila sababu ya msingi uwezo na experience well committed nodham ya kazi unayo ila analetwa mtu mpya asiejielewa wala hana uzoefu wa kazi wala mazingira na analalamikiwa performance still hawaoni..iliwahi nikuta hii najua maumivu yake ila Ma HR na Ma boss wa mashirika Binafsi MUNGU ANAWAONA NA MTALIPWA TU
 
Hakuna kitu baadhi ya maboss hawapendi kama kuona unapiga hatua kwa kufanya vitu vya ziada kumzidi yeye au wafanyakazi wengine..binafsi baada ya kufanyiwa figisu nlijikita zaidi kufanya ujasiriamali,japo walishangaa kuona mbona nimeweza kuinvest pesa nyingi kwa muda mfupi ktk biashara yangu siishi nyumba ya kupanga,nausafiri wangu binafsi nafanya biashara yangu kwa amani so wanashangaa kwa nn maisha yanaenda.MUNGU HAKUPI KILEMA AKAKUNYIMA MWENDO NIMESHUDIA nlipata nguvu hii baada ya kuona dalili mapema kwamba naweza nisiwe kazini soon baada ya mkataba kuisha
 
We jamaa una akili kama zangu kabisa niliwatukana wahindi enzi hizo hawatokaa wanisahau!
Na mpaka sasa sina mpango wa kuajiriwa tena maana naweza mpiga kichwa boss akizingua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…