Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Mimi nimewahi kufundisha shule fulani private. Mkuu wa shule alikuwa na mambo ya kiwaki kisenge.

Sometimes, anaweza kukufokea hata mbele ya wanafunzi.

Ikifikia tarehe za mishahara basi ndio kufoka nje nje. Nyumba niliyokuwa nimepewa ilikuwa karibu na ya kwake, so, sometimes washkaji wakija gheto mkawa mnaongea kwa nguvu mnabishana mnacheka, anawaibukia anafoka Walimuu mnapiga kelele kama watoto wa primary[emoji1787]

Nikawa najisemea tu huyu dawa yake iko jikoni.

Kuna wakati tunakaribia kuchukua mshahara, mwisho wa mwezi akawa anafoka, ooh kama hujaandika scheme of work na lesson plans sikulipi mshahara [emoji1787] (walimu wanaijua hii midude.

Basi nikajipinda nikaandika hayo ma-scheme of works ( plan ya miezi 6 ) na lesson plans, nilivyomaliza nikampelekea.

Akasema poa, nenda kwa Accountant akupe mshahara wako. Nilivyolipwa tu, nitatafuta muda huyo mkuu wa shule hayupo, nikaiingia ofisini kwake nikayaiba hayo scheme of works nikaenda nikayachoma moto halafu nikaacha kazi, nikasepa[emoji1787]. Ilikuwa 2013 hiyo.

Kiukweli mimi kuvumilia dharau nilishashindwa kabisa. Siwezi.

Mimi chuoni nimewahi kumfuata Lecturer ( HoD ) ofisini kwake nikamtukana. Alikuwa ananisumbua sana.

Mimi probably nitakuja kumnyenyekea mtu nikiwa na watoto 6, mmoja ana ugonjwa wa kudumu, nadaiwa kodi ya nyumba, mama ana matatizo.

Hapo nitajitahidi kunyenyekea. Kwasasa nitakuwa muongo. Sitaweza.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji613][emoji613][emoji613][emoji613][emoji613][emoji613][emoji613][emoji613][emoji613][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mimi bhna nimemaliza tu ile chuo narud zangu nyumban iringa mshua kaniconektia kazi ya sheli apo sikua hata na wazo la kufanya kazi sheli kilichotokea bosi akasema bwana huyu leo leo aanze kazi section ya USIKU yaan kuanzia saa 3 usiku hadi asubuhi mi nikasema fresh sasa nafika pale nikapewa dada mmoja nifanye nae kazi yule dada hakuniruhusu niingie usiku akasema nifanye mchana nae bosi alipokuja akamwita yule dada akamfokea kwann unampa kazi mchana huyo ashinde usiku yule dada akasema huyu hajajua hata kushika pampu vzr kwaio anahitaji pole pole nikaanza kuwaza kichwan hapa tayar

Sasa imepita kama wiki hivi nafundishwa na walimu wawili tofaut yule dada na braza mmoja nikifanya kaz na dada sipati loss nikifanya kaz na jombaa utakuta loss elfu 5 mara 3 duuh nikawaza why? Lakin kila nikiwa na dada sipat loss nikajua hapa nachezewa mchezo siku nikiwa na bro siruhusu ashike hela hata 100 mwisho sipat loss akaniuliza vip hapa umekuja kuchukua nafasi ya nan? Nikasema apa nimeletwa tu na mshua aliniombea sa sijui bosi alikua hapend nifanye kazi pale siku napigiwa tu simu ni stop kwanza kazi mpk watakapofanya uchunguzi hua nakopesha mafuta sijui vitu gan basi kazi ikaishia pale
 
Hakuna kitu baadhi ya maboss hawapendi kama kuona unapiga hatua kwa kufanya vitu vya ziada kumzidi yeye au wafanyakazi wengine..binafsi baada ya kufanyiwa figisu nlijikita zaidi kufanya ujasiriamali,japo walishangaa kuona mbona nimeweza kuinvest pesa nyingi kwa muda mfupi ktk biashara yangu siishi nyumba ya kupanga,nausafiri wangu binafsi nafanya biashara yangu kwa amani so wanashangaa kwa nn maisha yanaenda.MUNGU HAKUPI KILEMA AKAKUNYIMA MWENDO NIMESHUDIA nlipata nguvu hii baada ya kuona dalili mapema kwamba naweza nisiwe kazini soon baada ya mkataba kuisha
Nadhani boss wa ofisi yetu alikua amezidi. Yani pale ilifika hatua hata mtu ukifiwa ni bora ulie na wa kwenu lakini sio wafanyakazi waje au boss maana wakifika tu wataanza kuona fan ni ya kwao, taa ni za kwao, nyumba kubwa umetoa wapi kwa mshahara wa laki nane😂😂 pengine hata unapanga lkn unawezaje kupanga nyumba nzuri? Yan furaha kwao ni wewe uwe unaandika vibarua vya kuomba mkopo kwao ambao nao hawatakupa mpk uspecify shida. Yan usiseme huu mkopo ni wa kwenda kutatua matatizo ya kifamilia ila useme yan unga sina ndani au mafuta ndio uupate kesho stafff wote wajue hukua na unga na mafuta
 
Mm nishafukuzwa kibabe huku mfukoni Nina eflu 2 ya nauli,bank Nina elf 28,na hapo ni ktkt ya mwez,mwisho wa mwez ninatakiwa ada ya mtt private school, nimepewa barua ya kufukuzwa nikasepa,baada ya kuhangaika miez km mitano nikapata kaz mkoa mwingine,kazi ya maana kinyama,mshahara kule nilipofukuzwa ulikua 480k,nikapata kazi ya mshahara 915k take home,baada ya miez mi5 nikarud hom kusalimia,nikaonana na wafanyakaz wenzangu wa mwanzo kule nilipofukuzwa,wengi wanapongeza kuwa eti nimependeza,nimenenepa na kunidadisi nafanya kaz wapi,Mara njiani nakutana na bosi wangu yupo ndani ya gari na wafanyakazi wengine km wa3 HV,bosi akamwambia drv wake asimamishe gar akaniita na kuniuliza eti nafanya kazi gani na wapi?,,

Mara eti dah maisha umeyapatia kweli,naona umependeza km vile MD wa kampuni flani HV,nikamjibu nafanya kazi za ndani kwa mama ako kisha nikasepa zangu,.mpuuzi sana yule jamaa,hadi Leo nafanya kazi hapo hapo na mshara umepanda hadi 1.25m,na ki IST nimenunua na mjengo wangu nimemalizia.ukifukuzwa kazi unapata muda mzuri wa kutafuta kazi nzur maana bila hivyo una relax na kikazi ulichonacho na madeni kila kona
kweli kabisa usemayo hujakosea
 
l
Aisee nakumbuka ilikuwa mwaka 2014 nilipata kaz shule moja ya girls nilikuwa mchapa kaz sn boss alinipenda sn maana nilikuwa nafanya kaz ya records Mambo ya Ada na michango mingne lakini nilikuwa na faida nyngn Kama sekritari hayupo nilikuwa nasmamia show za kuchapa mitihani na Mambo mengine yote ya kuprint na kuchapa sasa alikuja mzungu mmoja mdada kaleta mtoto pale shulen na mi ndo nilikuwa napokea wanafunz nakagua kama wamelipa Ada na michango mingne Yan mi nilikuwa na uwezo hata wa Kimtoa nje mwanafunz ambaye hajakamilisha ada huyo mzungu alipofka akawa ananiangalia vile nachapa kazi kwa kila anayeingia na kutoka akanikubali sana sasa alinikubali zaid pale nilipomsaidia mtoto aliyekuja naye kuingia shulen wakati hakuwa amelipa ada kwan mzungu aliniomba nimpe rist ya ada halafu kesho atanipigia cm nikachukue pesa niitumbukze bank

Kwan ye muda wa kwenda bank amekosa kabisa basi bhana kweli kesho yake alinipa ile pesa lakin akaniulza nalipwa shs ngapi nikamwambia akasema nna mkataba nikamwambia hapana bs akanambia ana kampuni ya kukodisha magari anataka nikafanye kaz kwake anilipe mara mbili ya mshahara nnaolipwa shulen nikamwambia poa
kweli nilihamia huko kwa mzungu kimbembe kilikuwa hivi

Kumbe pale ofsn kulikuwa na mdada wa kimasai anaitwa joyce ndiye alitakiwa atoke pale ofsn ahamie kwny kitengo cha masoko na jamaa wengi madereva pale ofsn walikuwa hawampendi sn daaah aisee dada alikuwa na roho mbaya kama sura yake akawa anaenda kwa waganga ili nifukuzwe kazi maana hakupenda kutoka pale ofsn kwenda kwny masoko

Mara nikute kaz nilizofanya jana yakr zmefutwa kwny pc yan majanga tu boss nae akaanza kunichukia hatari bila sababu

Mdada akawa anaomba ruhusa hata ya wiki kumbe anaenda kwa waganga ili nifukuzwe kaz amlete rafiki yake ndo aje awe wa masoko ye arudi ofsn cha ajabu kaz hawez kabsa ila ni ana mdomo hatari mwisho wa sku nilichukia kbs kaz wkend ikiisha nakosa amani kabsa aisee nakumbuka bosi aliniita sku moja mbele ya huyo dada akawa ananifokea eti simuheshimu huyo dada mara huyo dada akawa anatamba eti tatzo mi smjui ye ni nani pale ofsn mmmh bosi akanambia natakiwa kumheshimu joyce sn kama bosi nilishangaa nmuheshimu kvp mbona sielewi aisee wakati ni binti tu kijana kama mimi au nmemkosea nn yan nikawa sjui kbs ndo nikpata taarifa kwa dereva mmoja kwmb joyce anasema mi nafanya sn kaz na bosi ananikubali sn sa uwenda mbele ya safari takuja kuwa mtu mkubwa sana ukizngatia nina elimu kubwa kuliko wafanyakaz wote na nna chapa kaz hatari

Siku moja niliitwa na bosi mbele ya wafanyakaz wote ilikuwa mwisho wa mwezi nashangaa nakabiziwa mshahara wangu by cash na kuambiwa sina kaz tena pale bila sababu za msingi skuumia sn maana nilishaona vitimbwi vya joyce ila niliwambia watu pale ofsn kama Mungu Aishivyo ikiwa nmefukuzwa kaz kisa joyce tena bila kosa lolote bs joyce hatomalza miezi miwili naye atatmuliwa kweli nilipata taarifa joyce alifukuzwa kwa aibu kubwa kwa kosa la kuitia hasara kampuni hata miezi miwili haikufka

Mengne ningesema wakuu baada ya kufukuzwa ilikuaje sema naogopa kuwachosha nyie acheni tu maisha haya maisha haya stasahau nilikuwa natembea kwa mguu toka goba mpk posta au mabibo hostel kwny internet kutafuta kaz nyngn online stasahau kabisa
Tupe kisa chako ili nasi kitupe funzo katika maisha yetu
 
Mimi ni jeuri najijua ila sijawahi kufukuzwa kazi.Huwa naondoka kama naenda msalani ndiyo hawanioni tena.Halafu yalivyo majinga huwa yanalia eti yamenikumbuka.😝😝😝😝😝
Ukianza fanya kazi kwenye makampuni ndo uje uchangie. Hizo za kufanya majumbani mwa watu ndo watoto wakati mwingine wanakulilia...na pia why wewe unakuwa unatumia choo cha nje?
 
Ukianza fanya kazi kwenye makampuni ndo uje uchangie. Hizo za kufanya majumbani mwa watu ndo watoto wakati mwingine wanakulilia...na pia why wewe unakuwa unatumia choo cha nje?
Kwani uliumia sana kwa nilichokiandika awali?Yote kwa yote,yalikuwa zamani hayo.Weye endelea na kufanya kazi kwa Wahindi.Anee chee!Gutroo gasepetoo!
 
Kwani uliumia sana kwa nilichokiandika awali?Yote kwa yote,yalikuwa zamani hayo.Weye endelea na kufanya kazi kwa Wahindi.Anee chee!Gutroo gasepetoo!
Umefanya kazi za ndani kwa wahindi mpaka umejua kihindi.....🤣🤣🤣🤣🤣 Unajisaidia choo cha nje...
 
Nadhani boss wa ofisi yetu alikua amezidi. Yani pale ilifika hatua hata mtu ukifiwa ni bora ulie na wa kwenu lakini sio wafanyakazi waje au boss maana wakifika tu wataanza kuona fan ni ya kwao, taa ni za kwao, nyumba kubwa umetoa wapi kwa mshahara wa laki nane😂😂 pengine hata unapanga lkn unawezaje kupanga nyumba nzuri? Yan furaha kwao ni wewe uwe unaandika vibarua vya kuomba mkopo kwao ambao nao hawatakupa mpk uspecify shida. Yan usiseme huu mkopo ni wa kwenda kutatua matatizo ya kifamilia ila useme yan unga sina ndani au mafuta ndio uupate kesho stafff wote wajue hukua na unga na mafuta
Hii kiboko hiyo sio ofic ni kijiwe cha wachawi 🤣
 
U
Utravet haikuwa mtego,mm sikwenda kwa kuwa tayari nilikuwa na mkataba na LEAD PROJECT,na Niko govt tayr,so nikaamua nimwambie ukweli Yule manager wa utravet ,nakumbuka email yake ilianza kwa jina la laagie.somethin hiv,so nikaamua kum connect jamaa angu aliitwa somebody msoka,from tanga.manager wa utravet akaniambia jamaa yuko vizur nikamwambia yes,akasema mwambie atume maombi kwa email,Ila huyu tutampiga interview tukiona anafaa basi tutampa offer,nikampa contact jamaa angu awasiliane nae,ofcoz jamaa alienda wakampiga interview baadae ,akaenda Nairobi Kenya kwa 2weeks seminar.alipiga nao kazi.
Ultravet ni ya kilimo?
 
Binafsi hadi nineisha zoea private nikifanya kazi najua kufukuzwa ni muda wowote tu.

Cha kwanza sinaga kumuogopa mtu awe boss awe nani yani hii hali inaniponza sometimes siwezi kunyenyekea..

Kazi za hospitali kupiga madili huwa kupo tu mala moja moja
Nimefanya kazi Zahanati nyingi sana sitoboi hata nusu mwaka nisha fukuzwa.

Ila nilipofukuzwa mala ya mwisho ndio inachekesha na kutia simanzi.
Nesi mmoja alikua ni mke wa mtu akawa ananitaka, shobo shobo kibao, mala akija job aseme amenimiss na kutaka kunikiss juu, mwamba nagoma.

Bwana hee nikapokeaga elfu 30 ya mgonjwa nikaichapa juu kwa juu.
Huyo nurse akajua, alinichoma kwa bosi live bila chenga.

Kilichoniuma sio kufukuzwa kazi, yani ni kuchomewa na demu ambae nilikua na uwezo wa kumla/ kuchapa mashine na tukashirikiana vizuri kila sector
kaka na mimi nipo private sector nimejishikiza kwa mda , ila niliwahi piga field atachment apo apo wakati nkiwa bado nipo chuo na bosi akawa ameniona akaniita na kunipa ajira sasa, wakati nipo field kuna demu nilimtongoza na nkabatika kumpiga mashine, lakini cha ajabu huyo dada amekua sumu kwangu na kunichongea kwa bosi. alafu zaidi mimi napokea pesa nyingi zaidi ake lakini wakati naajiliwa apa uyo demu alinambia kua ntalipwa elfu hamsini lakini cha kushangaza namzidi mshahara mara mbili zaidi
kwahiyo watu tunao waamini ndio wanakua sumu sana kwetu jamani.
 
Kati ya vitu vinavyouma katika maisha ni kufukuzwa kazi, nakumbuka miaka kadhaa nyuma baada ya kumaliza degree yangu nikabahatika kupata kazi kwenye kitaasisi kimoja hivi.

Nikapiga kazi kwa kujituma sana aliekuwa boss wangu akawa ananichukia mno visa kila siku kikianza hiki kinakuja hiki nikawa Nina stress saana na kazi.

Mara nikajikuta naambiwa nimewatukana staff mate wenzangu yaani balaa juu ya balaa, nakumbuka nilienda likizo ya kawaida kama ilivyo haki ya mfanyakazi yoyote nikiwa likizo watu wa kazini wakanitonya kuwa kuna mtu kaajiriwa anafanya majukumu yangu ni balaa.

Siku narudi kazini namkuta mfanyakazi mpya kakalia kiti changu na anatumia computer yangu nikashindwa nikae wapi na nifanye majukumu gani mzee nikashinda bench siku nzima, baada ya happy tukawa tunafanya kazi kwa kupokezana kwenye computer nlokua natumia Mimi shida hizi jamani.

Basi bhana aliekuwa msaidizi wa boss wangu akaniita kiutu uzima akanambia hapa kazi hamna kama unaweza apply sehemu nyingine wenzio wanakusubiria uteleze kidogo tu wakule kichwa, nikabaki dilemma basi siku moja foleni za mjini hapa nikachelewa kuingia kazini kama dakika kumi hivi boss akawaandikia HR office kama hayupo tayari kufanya kazi na Mimi.

Hr mmoja akanambia kama naweza niandike resignation letter au nisubirie kufukuzwa nikaona maji yamekua mengi nikaandika barua ya kuacha kazi kwa mwezi mmoja boss akaacha kunifatilia tangu siku nlipoandika barua nikawa naingia kazini kiubish mpk mwezi ukaishi nikalipwa mafao yangu mambo yakawa yanasonga.

Ugumu wa kwanza baada ya kuacha kazi ni ile hali ya kuamka asubuhi hujui uende wapi, unajikuta unachukia sehemu ulokuwa unafanyia kazi hata kupapita hutaki tena marafiki wa kazini wanakutenga na wengine wanakupotezea kabisaa majirani na ndugu wanaanza kukusengenya usipojipanga unaweza kujiua.

Nashukuru Mungu niliweza kupambana na maisha bila kazi nimesimama tena nje ya ajira.
Huu Uzi wa siku nyingi lkn
Wee Ni Kama mm tu nilifanyiwa hvyo hvyo
Hadi leo sinaga mzuka wa kupita wakukutana na wafanyakazi wenzangu
 
Dah tutafika tumechoka sana.

NGOJA TUPATE SHUHUDA ZA WATU WALIOWAHI KUFANYA KAZI KWA WAHINDI.
 
Back
Top Bottom