Tuliowahi kukopesha watu pesa na tukazimwa tukutane hapa

Tuliowahi kukopesha watu pesa na tukazimwa tukutane hapa

asiyetabirika

Member
Joined
Oct 14, 2019
Posts
46
Reaction score
56
Kumkopesha pesa jamaa/ndugu muda mwngine kumekuwa na changamoto sana kwenye urudishaji wa deni, nimegundua kwa sehemu kubwa mkopaji huwa akija kukopa kwa upole huku akitia huruma huku akiwa na ahadi za uhakika juu ya siku ya kulipa deni, sasa kimbembe ukisha mkopesha zinapoanza kusogezwa siku za kulipa deni na sababu lukuki zilizo nje ya makubaliano.

Hii tabia imeua sana mahusiano mazuri kati ya ndugu,jamaa na marafiki yaani unakuta watu wanagombana sababu ikiwa mmoja alimkopesha mwezake ila hakulipwa na mkopaji hana dalili za kulipa na muda mwingine nae utakuta analeta ukorofi kwa kujibu vibaya au analeta sababu dhaifu na visingizio visivyo eleweka na wakati mwingine kama upo mbali nae anaweza asiwe ahapokea simu yako kabisa.

Sasa kama wewe ulikutwa na visanga hivi vya kumkopesha mtu na akakusumbua kulipa hadi ukaona upotezee au kugombana nae kabisa na kuvunja urafiki/mahusiano mazuri yaliyokuwepo kabla ya kukopeshana, tupe kisa chako jinsi ilivyokuwa...
 
Daah mimi sikukopesha bwana... Ila nilikuwa na pikipiki boda ... Nikawa nimeenda Kenya one time kwa mshikaji tulipiga naye chuo SAUT .... nilipofika kule nikapata mishe moja halafu kipato sina... Nikamwambia jamaaa msela tunapiga naye kazi oyaa sukuma hiyo tuku 1.5M nitumie 1.3 M , laki2 mpe maza house ili tupige gap la kodi halafu 100 baki nayo daaah..... Nilitumiwa 1M tu... Oooh mwanangu aliumwa kikaenda kikarudi nitakutoa tu babu ..... Heeee kidogo jamaa kapata uhamisho wa kujiombea ndio nitoleeee aseeee
 
Daah mi sikukopesha bwana... Ila nilikuwa na pikipiki boda ... Nkawa nimeenda kenya one time kwa mshikaji tulipiga naye chuo SAUT .... nilipofika kule nikapata mbishe moja halafu kipato sina... Nkamwambia jamaaa msela tunapiga naye kazi oyaa sukuma hiyo tuku 1.5M nitumie 1.3 M , laki2 mpe maza house ili tupige gap la kodi halafu 100 baki nayo daaah..... Nilitumiwa 1M tu... Oooh mwanangu aliumwa kikaenda kikarudi ntakutoa tu babu ..... Heeee kidogo jamaa kapata uhamisho wa kujiombea ndio ntoleeee aseeee
Kihisabati umedanganya Bahariaaaa...yaaani boda uuze 1.5 kisha utumiwe 1.3 then mama mwenye chumba apewe 200,000 na jamaa yako abaki na 100,000? Ukijumulisha huoni kama umeshatoka kwenye margin ya 1.5?
 
Kihisabati umedanganya Bahariaaaa...yaaani boda uuze 1.5 kisha utumiwe 1.3 then mama mwenye chumba apewe 200,000 na jamaa yako abaki na 100,000? Ukijumulisha huoni kama umeshatoka kwenye margin ya 1.5?
Sorry, kulikuwa na matairi pia..mapya ya vrubber nilikuwa nataka kuyabadili .... Nayo aliyasukuma tofauti na tuku....
 
Wakija kukopa, mikono nyuma, wanaeleza shida kibao na wanakuhakikishia kukulipa ndani ya muda waliokuahidi au ikiwezekana hata kabla ya huo muda

Ukishamkopesha sasa, wewe ndio inabidi umueleze shida ulizo nazo kama njia ya kumshawishi akurejeshee hela yako

Mimi huwa nakopesha kiwango ambacho nipo tayari kukipoteza, na asiponirudishia bila genuine reason (ambayo mimi kwa mbinu zangu nitakuwa nimethibitisha) , ndio hawezi kupata msaada wangu hata nione anakata roho
 
Mimi Bossi wangu tulipiga hela akanizima ilikuwa tugawane 60/40 akanipa 20% nyingine hadi leo ni sound hadi kastaafu


Saivi nikikukopesha unanipa collateral inayozidi kiasi unachochukua
 
Aaaah hizi mambo za kukopesha pasua kichwa sana jamaa. Nakumbuka 2007 nilimkopesha jamaa aiseee huezi amini jamaa alinizungusha hatari.

Kipindi hicho kila nikikumbushia alipe napigwa sound, mwisho nikaamua kufanya kitu wanaita "unthinkable" alilipa kwa masikitiko. Dawa ya deni ni kulipa no way
 
Aaaah hizi mambo za kukopesha pasua kichwa sana jamaa. Nakumbuka 2007 nilimkopesha jamaa aiseee huezi amini jamaa alinizungusha hatari.

Kipindi hicho kila nikikumbushia alipe napigwa sound, mwisho nikaamua kufanya kitu wanaita "unthinkable" alilipa kwa masikitiko. Dawa ya deni ni kulipa no way
Ningependa kufahamishwa hata kwa ufupi hicho ulichofanya.
 
Wakija kukopa, mikono nyuma, wanaeleza shida kibao na wanakuhakikishia kukulipa ndani ya muda waliokuahidi au ikiwezekana hata kabla ya huo muda

Ukishamkopesha sasa, wewe ndio inabidi umueleze shida ulizo nazo kama njia ya kumshawishi akurejeshee hela yako

😄🤣🤣 ukweli Mchungu huu
 
Jibu moja la mama zetu linaweza kukufanya ukasahau million uliyomkopa.."Nimekuweka tumboni miezi tisa" Bonge la defence mechanism
 
Kuna bwana mmoja hivi anagereji yamagari alikuwa mteja wangu sana, akahitaji nimkopeshe elfu 60, nikawa nimemkopesha ilipofika wakati wakulipa akaanza kunizungusha.... Kiukweli alinisumbua sana.

Kuna siku nilimforce anilipe lasivyo sibanduki kijiweni kwake ila alichonijibu kuwa ninaushahidi kuwa namdai? Aiseee roho iliniuma kinoma ila nilichomuuliza2 kwahiyo unamaanisha me sikudai akajibu ndio unidai..... Duh nikasepa zangu kiroho Safi yaani ndio ishazurumiwa hivyo nauteja ukawa umeisha kihivyo ila nilimwaga chozi.

Elfu 60 nihela ndogo sana ila dharau alizonionyesha kunizurumu kibabe kwasababu yeye nimkubwa kwangu nahata vihela pia kanizidi ila2 aliamua kunizurumu kwakujua siwezi mfanya lolote. Nikawaza niende polisi nikajisemea uzembe huu yaani niende polisi wakati kishaniambia ninaushahidi gani kama namdai alafu kingine siwezi kwenda polisi kwahela ndogo kama ile.

Nikalala siku mbili sina raha nawaza nimfanyaje ili nayeye roho imuume au apate hasara.

Chakwanza nikawaza nimvizie usiku nipasue kioo chagari yake ila asijue nani kapasua. Ila hii niliona ningumu kwangu maana naweza tambulika.

Chapili ambacho nilikiwaza naambacho nilikifanya nanikafanikiwa kwaasilimia 100 nikuichoma moto gereji yake pamoja namagari mabovu yaliyomo hapo gereji. Nikachora ramani yangu fresh nakwasababu pale gereji napafahamu vzr. Nikachunguza mlinzi huwa anakaa mara nyingi usiku upande gani nikawa nimepata picha kamili.

Siku yatukio kama kawaida mzee baba mida yamapema sana saa mbili usiku nikaanda zana zangu petrol yakutosha. Kwasababu hiyo gereji ilikuwa nafensi nanyuma yefensi palikuwa nanyumba zawatu namimi ramani yangu ilinionesha natakiwa niruke ukuta kwanyuma ambapo ndio kuna nyumba zawatu, mida saa mbili nilipoenda kuangalia mazingira nilikuta watu wanaoishi kwenye nyumba zanyuma yafensi bado hawajalala so nikapiga chimbo mpaka mida yasaa6 usiku ndio niliponyata nakupalamia ukuta nakumwaga oil maeneo mengi ambayo nirahisi kushika moto nakuambukizana ili usambae haraka. Nikarudi juu yaukuta wafensi nakiberiti changu nikalala kama vile nyoka juu yaukuta nikaripua mambo nikasepa zangu.

Kiukweli moto uliwaka sana nahakuna kilichotoka salama yaani niliteketeza kila kitu maana zima moto walifika ila kwakuchelewa sana. Kesho yake asubuhi ndio habari hiyo maana gereji ilipo namimi napofanyia mishe zangu sio mbali tupo karibu sana so mimi nikawa nimejikausha tuliii. Polisi walipima pima ili kujua chanzo chamoto naikibidi wampate namuhusika ila ndio basi tena mpaka leo hii hakuna kilichoendelea namuhusika nimechili.

Baada yamwezi mmoja toka tukio litokee alinifata nakuniomba msamaha nakunilipa pesa yangu ila niligoma kuichukua nikamwambia me sikudai kama alivyosema mwanzo. Nalile tukio toka litokee anahisi kama ndio mwanzo wayeye kufirisika maana hata lile eneo alifukuzwa nahata wateja wengi wamemuhama.
 
Back
Top Bottom