Tuliowahi kukopesha watu pesa na tukazimwa tukutane hapa

Tuliowahi kukopesha watu pesa na tukazimwa tukutane hapa

Kuna bwana mmoja hivi anagereji yamagari alikuwa mteja wangu sana, akahitaji nimkopeshe elfu 60, nikawa nimemkopesha ilipofika wakati wakulipa akaanza kunizungusha.... Kiukweli alinisumbua sana.

Kuna siku nilimforce anilipe lasivyo sibanduki kijiweni kwake ila alichonijibu kuwa ninaushahidi kuwa namdai? Aiseee roho iliniuma kinoma ila nilichomuuliza2 kwahiyo unamaanisha me sikudai akajibu ndio unidai..... Duh nikasepa zangu kiroho Safi yaani ndio ishazurumiwa hivyo nauteja ukawa umeisha kihivyo ila nilimwaga chozi.

Elfu 60 nihela ndogo sana ila dharau alizonionyesha kunizurumu kibabe kwasababu yeye nimkubwa kwangu nahata vihela pia kanizidi ila2 aliamua kunizurumu kwakujua siwezi mfanya lolote. Nikawaza niende polisi nikajisemea uzembe huu yaani niende polisi wakati kishaniambia ninaushahidi gani kama namdai alafu kingine siwezi kwenda polisi kwahela ndogo kama ile.

Nikalala siku mbili sina raha nawaza nimfanyaje ili nayeye roho imuume au apate hasara.

Chakwanza nikawaza nimvizie usiku nipasue kioo chagari yake ila asijue nani kapasua. Ila hii niliona ningumu kwangu maana naweza tambulika.

Chapili ambacho nilikiwaza naambacho nilikifanya nanikafanikiwa kwaasilimia 100 nikuichoma moto gereji yake pamoja namagari mabovu yaliyomo hapo gereji. Nikachora ramani yangu fresh nakwasababu pale gereji napafahamu vzr. Nikachunguza mlinzi huwa anakaa mara nyingi usiku upande gani nikawa nimepata picha kamili.

Siku yatukio kama kawaida mzee baba mida yamapema sana saa mbili usiku nikaanda zana zangu petrol yakutosha. Kwasababu hiyo gereji ilikuwa nafensi nanyuma yefensi palikuwa nanyumba zawatu namimi ramani yangu ilinionesha natakiwa niruke ukuta kwanyuma ambapo ndio kuna nyumba zawatu, mida saa mbili nilipoenda kuangalia mazingira nilikuta watu wanaoishi kwenye nyumba zanyuma yafensi bado hawajalala so nikapiga chimbo mpaka mida yasaa6 usiku ndio niliponyata nakupalamia ukuta nakumwaga oil maeneo mengi ambayo nirahisi kushika moto nakuambukizana ili usambae haraka. Nikarudi juu yaukuta wafensi nakiberiti changu nikalala kama vile nyoka juu yaukuta nikaripua mambo nikasepa zangu.

Kiukweli moto uliwaka sana nahakuna kilichotoka salama yaani niliteketeza kila kitu maana zima moto walifika ila kwakuchelewa sana. Kesho yake asubuhi ndio habari hiyo maana gereji ilipo namimi napofanyia mishe zangu sio mbali tupo karibu sana so mimi nikawa nimejikausha tuliii. Polisi walipima pima ili kujua chanzo chamoto naikibidi wampate namuhusika ila ndio basi tena mpaka leo hii hakuna kilichoendelea namuhusika nimechili.

Baada yamwezi mmoja toka tukio litokee alinifata nakuniomba msamaha nakunilipa pesa yangu ila niligoma kuichukua nikamwambia me sikudai kama alivyosema mwanzo. Nalile tukio toka litokee anahisi kama ndio mwanzo wayeye kufirisika maana hata lile eneo alifukuzwa nahata wateja wengi wamemuhama.
Wewe jamaa una roho ngumu sana. Hiyo inaitwa komesha watoto.
 
Yap alinihisia ila hakujua kama mimi mwenyewe ndio niliingia mchezoni yeye alikuwa anahisi labda nilituma mateja ndiomana hata chakueleza hakuwa nacho
Pengine wala hakukuhisi wewe. Mtu kama huyo lazima kutakuwa na watu wengi tu wanamdai na anawazungusha. Kwahiyo hapo hakujua mhusika ni nani. Au alihisi ni KARMA pia.
 
Pengine wala hakukuhisi wewe. Mtu kama huyo lazima kutakuwa na watu wengi tu wanamdai na anawazungusha. Kwahiyo hapo hakujua mhusika ni nani. Au alihisi ni KARMA pia.
Yap yawezekana
 
Kumkopesha pesa jamaa/ndugu muda mwngine kumekuwa na changamoto sana kwenye urudishaji wa deni, nimegundua kwa sehemu kubwa mkopaji huwa akija kukopa kwa upole huku akitia huruma huku akiwa na ahadi za uhakika juu ya siku ya kulipa deni, sasa kimbembe ukisha mkopesha zinapoanza kusogezwa siku za kulipa deni na sababu lukuki zilizo nje ya makubaliano.

Hii tabia imeua sana mahusiano mazuri kati ya ndugu,jamaa na marafiki yaani unakuta watu wanagombana sababu ikiwa mmoja alimkopesha mwezake ila hakulipwa na mkopaji hana dalili za kulipa na muda mwingine nae utakuta analeta ukorofi kwa kujibu vibaya au analeta sababu dhaifu na visingizio visivyo eleweka na wakati mwingine kama upo mbali nae anaweza asiwe ahapokea simu yako kabisa.

Sasa kama wewe ulikutwa na visanga hivi vya kumkopesha mtu na akakusumbua kulipa hadi ukaona upotezee au kugombana nae kabisa na kuvunja urafiki/mahusiano mazuri yaliyokuwepo kabla ya kukopeshana, tupe kisa chako jinsi ilivyokuwa...
Sitamsahau mligo na masiva
 
Hehehehheeee. Kuna mwana mmoja ivi tumesoma wote O'level. Yy hakuendelea mbele akawa mtu mishe town.

Basi bwana mm 2nd yr nkataka nipange gheto na mda huo nilkua field so sikuwepo mjini. Nkachonga na mwana anitafutie gheto mjini nimtumie hela.

Jamaa akaniambia gheto lipo ila kupitia kwa dalali...nkasema poa. Mm dalali simjui nakutumia ww. Akasema poa. Nkamtumia hela ya chumba na dalali. Kumbe mhuni amechonga na wahuni wenzie wa ekt dalali.
Wakawa wamenipiga hela kiivo.

Badae figisu zikaanza. Nkawa napiga simu wananipotezea. Nkawa namsumbua yule jamaa anaejiita dalali. Ikabid afunguke ...ananipa siri kua hakuna cha chumba wala nn na yy sio dalali bali alikodiwa tu.

Basi nkawa nimepata ukweli. Gheto tulipanga tukakae na washkaj zangu ivi.

Akaanza kudai kua alimpa hela dalali ila analeta mizengwe.
Basi bwana mm nkajifnya fara nkamwambia hela yenyewe ya njaa, kwanza mm nna miradi mingi inayoniingizia pesa na boom limetoka kutema tu juzi. Ahahahahahah 😂😁😁😁.

Nkampanga tuktane tukatanue mjini siku mingi hatujaonana. Heheheheh watu wa mjini wanavyopenda ofa vya bure. Si akakubali tuonane. Heheheheeh.
Nkmwambia "T" muhuni wangu mmoja ivi ambae ndo tulkua tunaenda kukaa wote gheto tukazama mtaa wa kuktana.

Kweli bhna jamaa akawa amekuja. Tukaingia restaurant moja iv ktukaanza kupiga vyombo. Chips, soda,samaki, bia. Kula kwa Fujo mingi mingi.

Kabla bill haijaja, kwa kutabasam nkaanza kusifia simu yake kua nzuri. Baadae nkamuomba niiangalie.

Alivyoitoa tu kunipa, nkaanzisha stori za kodi ya nyumba waliyokula. Simu nkampasia mhuni wangu T.

Heheheheh.jamaa kahahaha. Nkampgia yule jamaa ake, akamchana kua J wape hela washkaj. Timbwili timbwili watu wakajaa. Jamaa wakamharass atoe hela la sivyo aende polisi. Jamaa akakubali kutoa hela iliyokua kweny simu. Akaomba simu akachukua pesa akatutumia kwenye simu yetu.

Heheheheheh. Case solved...bill yake akalipa mwenyewe. 😂😁😂😁😁🤸🏾🤸🏾🤸🏾.
Nilicheka sana ujanja wa yule 🐒
 
Unavyomkopesha mtu inamaana hana kitu sasa unategemeaje mtu uliyemkopesha hana kitu akulipe baadae
 
Back
Top Bottom