Tuliowahi kukopesha watu pesa na tukazimwa tukutane hapa

Undava undavu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aaha hapo sawaa...nkasema hio hasara si mzee wa watu angefungwaa!! Sema nae alikuwa mkorofi unamdai alafu anajibu shit
Acha mkuu jamaa nindez sana maana nilichukia sana mpaka ikafikia hatua nikasema nailipua gereji naendapo nikifahamika basi nipo tayari kufungwa ila lazima nayeye aonje faida yadharau zake
 
We jamaa komandoo safi sana
 
Mimi nilimkopesha mshikaji wangu laki1 alafu kila nikimuona sound. Kuna Siku nikafumiana nae anananua simu ya laki 3 dukani, nilichofanya baada ya kumsalimu nikaisifia ile simu nzuri sana, alafu nikamuomba niicheki. Nilichotokea ni kusepa nayo alinifuata kwangu baada ya nusu saa na pesa yangu yote huku kanuna.
Zingatia deni lilikuwa limefikisha mwaka na miezi 4
 
Ulichomfanyia awezi kusahau yanii ni fundisho na matapeli wengine wanaosoma huu uzii
Mkuu nilifikia hatua mbaya nikajiambia hili tukio nafanya mwenyewe nanisiri yangu naendapo kama nikigunduliwa basi nifungwe ila kamwe nisingekubali kama nimimi
 
Mkuu nilifikia hatua mbaya nikajiambia hili tukio nafanya mwenyewe nanisiri yangu naendapo kama nikigunduliwa basi nifungwe ila kamwe nisingekubali kama nimimi
yeah kwenye mission za hatari kama hizi hutakiwi kumshirikisha mtu
 
Mbona jamaa aliishajua hadi akajiludi kwenda kulipa deni
Yap alinihisia ila hakujua kama mimi mwenyewe ndio niliingia mchezoni yeye alikuwa anahisi labda nilituma mateja ndiomana hata chakueleza hakuwa nacho
 
Ningependa kufahamishwa hata kwa ufupi hicho ulichofanya.
Huyu bwana mkubwa alikua na biashara zake safi tu sasa nilichofanya ile siku nilikwenda straight kwenye moja ya biashara zake ni ghala la kuhifadhi nafaka.

Sikumkuta yeye nilikuta kijana wake wake wa kazi ambae ananifaham a-z, nikachukua mchele ule super nikapakia kwenye canter gunia kama kumi na moja hivi ambazo thamani yake ilinizidi kidogo pesa niliyomkopesha.

Huku na kule jamaa akaambiwa kua nilifika ofisini kwake kapiga simu yangu kama mara nne sipokei wala nini akatuma text kuuliza nilipo tuyamalize sikujibu wala nini.

Basi jamaa kuona hapati majibu yeyote kesho yake asubuhi sana kadamkia kwenye mishe zangu, ooohh unajua ulichonifanyia sio kizuri yani kaongea mengi sana. Jibu langu lilikua moja na nililitoa nikiwa very aggresive nilimuuliza umekuja na pesa yangu au maneno?

Jamaa alilipa pesa na gharama ya zaida juu hakuamini nilichomfanyia, nasema dawa ya deni ni kulipa sio kubadilisha njia ni hayo tu wakuu.
 
mimi hapa nadai watu wanne, kila deni sio chini ya 50,000 na sioni dalili za kulipwa ila walivyoomba waliniita majina yote sijui brother, ndugu, nk... ila sahivi naona wananilia bati, ila sio mbaya ukishamkopesha mtu af akazingua kulipa hapo ashajifukuzisha mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…